Saturday 26 June 2021

CHADEMA YATANGAZA KUTOSHIRIKI UCHAGUZI MDOGO WA MARUDIO KATA YA CHONA, JIMBO LA USHETU - SHINYANGA

...


 

TAARIFA KWA UMMA.

KUTOKUSHIRIKI  UCHAGUZI MDOGO WA MARUDIO KATA YA CHONA, JIMBO LA USHETU - SHINYANGA.


Ndugu Wanahabari na Watanzania.


Tunapenda kuutaarifu umma kuwa, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Shinyanga, hakitashiriki katika uchaguzi mdogo wa marudio, ambao umetangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kufanyika Mwezi Julai, 2021 katika kata ya Chona, Halmashuri ya Ushetu. Mkoa wa Shinyanga.


Aidha, tunapenda kuutaarifu kuwa; mpaka sasa, Chama hakijafanya mchakato wowote wa ndani ya Chama (utoaji fomu, kura za maoni)  na wala hakuna kikao chochote cha Kikatiba cha ngazi yoyote, kwa maana ya Kata wala Jimbo kilichoketi kupitisha  Mgombea udiwani, katika Kata ya Chona kama ambavyo  Katiba ya Chama  ya mwaka 2006, Toleo la 2019, ibara ya 7.3.9 (a) na 7.4.10 (a) zinavyotaka.


Hata hivyo, tumepata taarifa za kushangaza kuwa kuna Mtu mmoja, ambaye hajulikani makazi wala anwani yake, ameghushi muhuri wa Chama,  saini ya viongozi na kwenda kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea Udiwani kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata hiyo ya Chona.


Kwa hatua za awali, Chama tumekwisha kumuandikia barua rasmi Msimamizi Msaidizi wa Kata ya Chona, Barua yenye KUB CDM/USHT/01/2021.Pamoja na mambo mengine tumemtaka amuondoe mara moja Mtu huyo kwenye orodha na asitumie Jina na Nembo za CHADEMA . Kwa kuwa CHADEMA tumeazimia kutokushiriki Uchaguzi wowote wa marudio mpaka tutakapopata Tume Huru ya Uchaguzi Nchini.


Mwisho, Viongozi Mkoa na Taifa pamoja na Wanasheria wanafuatilia suala hili kwa uzito wake Tume ya Taifa ya Uchaguzi.


Pamoja na Salamu za Chama


Imetolewa leo 25.06.2021 na;


Emmanuel Ntobi


Mwenyekiti CHADEMA Mkoa Shinyanga

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger