Wednesday 30 June 2021

FAINALI ZA KIHISTORIA UMISSETA 2021 ZAUNGURUMA MTWARA

...

A.  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbasi (aliyejishika kidevu)

akiangalia  mechi ya nusu fainali baina ya timu ya Mtwara na Dodoma ambapo Mtwara imeshida bao 1 na Dodoma 0. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya kuchoto ni Mkurugenzi wa Michezo nchini Yusuph Singo

A.  Mechi ya nusu fainali ikiendelea baina ya Dodoma (nyekundu) na Mtwara(nyeupe) ambapo Mtwara imeshida bao 1 dhidi ya Dodoma 0.


Penati ikipigwa na mchezaji wa Pemba (kijani) kwa golikipa wa Geita (nyekundu) ambapo timu ya Pemba imeshinda penati 4 dhidi ya penati 3 za Geita.


Mwandishi Maalum, Mtwara

Michezo inayoendelea kwenye Mashindano ya Taaluma na Michezo kwa Shule za Sekondari (UMISSETA) yanafikia fainali Julai 1, 2021 kwenye viwanja mbalimbali vya mjini Mtwara ambapo mashindano hayo yatafungwa rasmi Julai 2,2021.

Kwa mujibu wa Msemaji wa mashindano hayo, John Mapepele fainali ya soka kwa wavulana itakuwa baina ya timu ya Pemba na Mtwara na itachezwa siku ya kufunga mashindano hayo Julai 2, 2021 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona wakati mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu soka utachezwa kesho baina ya timu ya mkoa wa Dodoma na Geita.

Amesema mchezo wa Soka kwa upande wa wasichana utakuwa baina ya timu ya mkoa wa Mwanza na Tabora ambao utachezwa mchana Julai 1,2021 ambapo hadi sasa mshindi wa tatu ni mkoa wa Arusha.  

Pia fainali ya Mpira wa Pete itakuwa dhidi ya timu ya mkoa wa Mwanza na Songwe

Kwa upande wa mpira wa Wavu fainali wasichana itachezwa baina ya mkoa wa Dar es Salaam na Mtwara wakati wavulana itakuwa kati ya Dar es Salaam na Arusha.

Mpira wa mikono fainali wasichana itakuwa baina ya mkoa wa Songwe na Morogoro na kwa upande wa wavulana Unguja watakipiga na Tabora.

Kwa upande wa mpira wa kikapu fainali kwa wanaume itakuwa baina ya Unguja na Dar es Salaam wakati kwa upande wa wanawake itakuwa baina ya Dar es Salaam na Mwanza.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger