Friday, 15 January 2021

ALIYESHIKA NAFASI YA KWANZA KITAIFA MATOKEO KIDATO CHA NNE 2020 ANATOKA FAMILIA YA WASOMI

...
Mwanafunzi aliyeshika nafasi ya kwanza kitaifa katika mtihani wa kidato cha nne mwaka 2020, Paul Luziga aliyekuwa akisoma shule ya sekondari Panda Hill ya jijini Mbeya anatoka familia ya wasomi.

Paul ni mtoto wa tano katika familia ya Luziga na ndugu zake wawili wamehitimu chuo kikuu na wengine wawili wanasoma katika vyuo vikuu mbalimbali nchini.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Ijumaa Januari 15, 2021 mama mzazi wa mwanafunzi huyo, Lucy Mwogela amesema siri ya watoto wake kufanya vizuri shuleni ni kumwamini Mungu.

Watoto hao wote wamefika chuo kikuu wakisomea fani mbalimbali.

“Mtoto wa kwanza alimaliza shahada ya kwanza yuko Dar es Salaam anafanya kazi. Wa pili ni wa kike amemaliza shahada ya uzamili, watatu na wa nne ni mapacha wapo chuo kikuu na huyu Paul ndiyo wa mwisho.”

“Siri ni kumwamini Mungu tu, hakuna ujanja wowote ninaoweza kufanya,” amesema Lucy.

CHANZO - MWANANCHI

Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger