Thursday 28 January 2021

SILINDE : TAMISEMI TUTAPAMBANA NA WANAOWANYANYASA MACHINGA

...

Naibu Waziri wa TAMISEMI David Silinde amesema Wizara ya TAMISEMI imejikita kwenye Kuondoa kero na kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara Wajasiriamali wadogo wadogo almaarufu kama Machinga.

Ameyasema hayo leo Mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa Kongamano la Machinga lililo fanyika jijini Dar es Salaam likiwa na lengo la kuwashukuru kwa kuiamini Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli na kutatua kero na changamoto zinazowakabili Machinga

"Kama Wizara ya TAMISEMI Tumepokea na kusikiliza changamoto za Machinga na tunazifanyia kazi. Changamoto ya Mikopo tumetoa nafasi kwa Machinga wakiwa na vitambulisho vya ujasiriamali mkajiunga vikundi mnapewa mikopo",amesema Silinde

Pia amegusia Tatizo la unyanyasaji wa Wafanyabiashara hao unaofanywa na Mgambo na kuahidi kulifanyia kazi.

"Kuna kero pia ya Mgambo kuwasumbua Machinga na sio kwamba wanatumwa na Serikali kuwanyanyasa wananchi bali ni hulka zao binafsi. Serikali ya Rais Magufuli haitavumilia wananchi wake kunyanyaswa tutashuka na kuwashughulikia",amesema.

Pia ameagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinafanya mikutano ya Hadhara kila mwaka na Machinga ili kusikiliza kero zao na kuzitatua.

"Machinga wamekuwa wakiomba mikutano na viongozi wa wilaya ili kusikiliza Changamoto na kero na tumeahidi kila mwaka mikutano miwili hadi mitatu ili kuwaskiliza",amesema Silinde.

 

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger