Wednesday 27 January 2021

ATUPWA JELA KWA KUMTWANGA CHUPA KICHWANI MWENZAKE DAR

...
Mahakama ya Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam, Tanzania, imemuhukumu kwenda jela miezi sita Mkazi wa Chang'ombe, Oscar Sanga baada ya kukiri kosa la kumshambulia kwa chupa na kumjeruhi kichwani Justa Paskal.

Hukumu hiyo imesomwa leo Jumatano Januari 27, 2021 na Hakimu Mkazi, Amos Rweikiza baada ya mshtakiwa huyo kukiri kosa lake.

Hakimu Rweikiza amesema Desemba 19, 2020 maeneo ya Temeke Sokota, mshtakiwa huyo alimshambulia kwa chupa na kumjeruhi Justa kinyume na kifungu cha 231 cha makosa Sheria namba 16 rejeo ya mwaka 2019.

Amesema kutokana na mshtakiwa kukiri kosa lake, mahakama hiyo imemkuta na hatia.

Via Mwananchi
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger