Sunday 25 October 2020

NKULILA AUNGURUMA NDEMBEZI, AAHIDI KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI

...

 Mgombea udiwani wa Kata ya Ndembezi (CCM) Manispaa ya Shinyanga David Nkulila akinadi sera za CCM na kuomba kura kwa wananchi

Na Marco Maduhu  Shinyanga. 

Mgombea udiwani wa Kata ya Ndembezi (CCM) Manispaa ya Shinyanga David Nkulila, amewaomba wananchi wa Kata hiyo wamchague kwa awamu nyingine tena kuwa diwani wao, kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu, ili akamilishe miradi ya maendeleo ambayo aliianzisha kwenye kipindi kilichopita. 

Nkulila ametoa ahadi hizo leo kwenye mkutano wake wa kampeni katika mtaa wa Tambukareli, wakati akinadi sera zake kwa wananchi wa Kata ya Ndembezi, kuwa wamchague tena ili aendelee kuwa letea maendeleo ikiwamo kupigania haki za wanyonge. 

Alisema wananchi wa kata hiyo wasije wakafanya makosa siku ya uchaguzi, na kumpigia kura mgombea mwingine wa upinzani, bali wakampigie kura nyingi za ushindi ili aendelee kuwaletea maendeleo, pamoja na kukamilisha miradi mikubwa ambayo aliianzisha ukiwemo wa machinjio ya kisasa na kituo cha afya. 

“Mimi ni diwani mpenda maendeleo na ni mtetezi wa haki za wanyonge, hivyo nipigieni kura nyingi za ushindi siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 28 mwaka huu, pamoja na mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi, na mgombea Urais Dkt. John Pombe Magufuli ili kwa pamoja tuwaletee maendeleo,”alisema Nkulila. 

“Katika kipindi kilichopita cha uongozi wangu kama diwani wa Kata hii, nadhani mmeshuhudia kazi ambazo nilizifanya, ikiwemo kutatua migogoro ya ardhi, na upimwaji wa viwanja, ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Kalogo hadi Bugoyi, ujenzi wa machinjio ya kisasa, kituo cha afya, na awamu ijayo tutajenga kituo cha Polisi,”aliongeza. 

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge, akizungumza kwenye mkutano huo wa kampeni, aliwataka wananchi hao wa Ndembezi siku hiyo ya uchaguzi, wakimaliza kumpigia kura mgombea Urais John Magufuli, Mgombea ubunge Patrobas Katambi, na madiwani wote wa CCM, waondoke kwenye vituo vya kupigia kura na kusubiri matokeo wakiwa nyumbani. 

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mgombea udiwani CCM Kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga David Nkulila akinadi Sera kwa wananchi ili wamchague Oktoba 28 kuwa diwani wao. Picha zote na Marco Maduhu
Mgombea udiwani wa Kata ya Ndembezi (CCM) Manispaa ya Shinyanga David Nkulila akinadi sera za CCM na kuomba kura kwa wananchi
Mwenyekiti wa (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge, akizungumza kwenye mkutano huo wa Kampeni.
Mwenyekiti wa (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge, (kushoto), akimnadi Mgombea udiwani Kata ya Ndembezi David Nkulila kwa wananchi wa Kata hiyo, kuwa siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 28 mwaka huu, wampigie kura za ushindi.
Baadhi ya wenyeviti wa mtaa kutoka Kata ya Ndembezi, wakiwa kwenye mkutano huo wa Kampeni.
Mkutano wa kampeni ukiendelea.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger