Wednesday 19 February 2020

Mahakama yahalalisha mlinzi aliyemtaka waziri kupanga foleni kufukuzwa kazi

...
Mahakama nchini Kenya imehalalisha aliyekuwa mlinzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Daizy Cherogony kufukuzwa kazi kutokana na kumtaka aliyekuwa Waziri wa Elimu, Fred Matiang'i kukaa kwenye foleni akaguliwe. Cherogory alifungua kesi baada ya kufukuzwa 2017.

Mahakama imetoa uamuzi huo na kusema kwamba kitendo cha dhihaka alichofanya Daizy Cherogony dhidi ya Dkt Matiang’i kinatosha kwa mwajiri wake, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (KAA), kuchukua hatua za kinidhamu dhidi yake.

Cherogony alifungua kesi dhidi ya KAA kwa madai kuwa kitendo cha yeye kufukuzwa kazi hakikufuata sheria, na pia alidhalilishwa na mwajiri huyo na kutaka alipwe fidia KSh milioni 2.4 (TSh milioni 55).

Amesema katika siku ya tukio, Aprili 5, 2017 abiria uwanjani hapo walikuwa wakipiga kelele, na alipomuona Waziri Matiang’i alimtaka apange foleni kwa ajili ya ukaguzi, na kwamba kitendo hicho hakikukiuka sheria wala taratibu yoyote ya KAA.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger