Tuesday 25 February 2020

Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak Afariki Dunia

...
Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak ambaye aliitawala Misri kwa takribani miaka 30 kabla ya kuondolewa kwa nguvu, amefariki Dunia Hospitalini, Cairo akiwa na miaka 91.

Televisheni ya taifa imesema Mubarak amekufa hospitali mjini Cairo ambako alikuwa akifanyiwa upasuaji. Hakuna maelezo yaliyotolewa kuhusu upasuaji huo.

Hosni Mubarak alikuwa kiongozi wa Misri ambaye kwa karibu miaka 30 alikuwa nembo ya uthabiti katika eneo la Mashariki ya Kati kabla kulazimishwa na jeshi kujiuzulu.

Alilazimishwa kufanya hivyo kufuatia siku 18 za maandamano ya nchi nzima yaliyokuwa sehemu ya vuguvugu la mapinduzi ya msimu wa mapukutiko katika nchi za kiarabu mnamo mwaka 2011.

Televisheni ya taifa imetangaza kuwa Mubarak amefariki akiwa na umri wa miaka 91. 

Muda wote wa utawala wake, alikuwa mshirika wa karibu wa Marekani, akipambana vikali dhidi ya uasi wa makundi ya itikadi kali za kiislamu na mlinzi wa mkataba wa amani kati ya Misri na Israel.

Lakini kwa maelfu na maelfu ya Wamisri vijana walioandamana kwa siku 18 mabarabarani katika uwanja wa Tahrir mjini Cairo na kwingineko mwaka 2011, Mubarak alikuwa kama farao.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger