Friday 21 February 2020

China Yakanusha Vikali Kwamba Virusi vya Coroni ni Vya Kutengeneza Maabara ( Silaha za Kemikali)

...
China imekanusha vikali madai ya Baadhi ya vyombo vya habari vya nchi za Magharibi vilivyodai kwamba Virusi vya COVID -19 vinavyoendelea kuitikisa Dunia ni vya kutengenezwa Maabara.

Kauli hiyo imetolewa na  Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang  ambapo amesema   China inatumai kuwa wakati jumuiya ya kimataifa inapopambana kwa pamoja kukabiliana na ugonjwa huo mpya wa COVID-19, itaendelea kupambana na kuzuia kwa pamoja "virusi vya njama mbalimbali za kisiasa".

Hivi karibuni, baadhi ya watu na vyombo vya habari vya nchi za magharibi vilidai kuwa virusi vipya vya COVID-19 ni "silaha za kikemikali" ambavyo vilitoka kwenye maabara moja nchini China. 

Bw. Geng amesema, hivi sasa watu wa China wanapambana na virusi hivyo kwa nguvu zote, hali ambayo inajiwajibika na pia inawajibika na usalama wa afya ya umma duniani. 

Amesema kitendo cha baadhi ya watu na vyombo vya habari kutoa kauli kama hizo zinazochochea hofu kina nia mbaya ama kukosa elimu ya kimsingi.

Bw. Geng amesema, hivi karibuni maofisa wa Shirika la Afya Duniani WHO wametangaza mara kwa mara kuwa, hakuna ushahidi wowote kuwa virusi hivyo vilitengenezwa katika maabara au kusababishwa kutokana na utengenezaji wa silaha za kikemikali.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger