Serikali mkoani Njombe imeongeza muda wa mwezi mmoja na siku mbili kwa wadaiwa sugu wa vyama vya ushirika kurejesha fedha walizokopa katika vyama hivyo vinginevyo watakamatwa na kufunguliwa kesi za uhujumu uchumi.
Akizungumza na wadaiwa sugu wa vyama hivyo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe Katarina Revokati ambaye ni katibu tawala mkoani humo anasema hadi kufikia disemba 18 fedha iliyorejeshwa ni mil 6.6 kati ya bil 6.4 ambazo zilikopwa katika vyama 336 miaka kadhaa iliyopita na kueleza kuwa serikali imeongeza muda ili kuepusha sababu hatua zitakapoanza kuchukuliwa
“Mpaka tarehe 21 mwezi wa kwanza wale watu wawe wamelipa kwa amani,kama unahisi kwamba taarifa haziko sawa utumie huu muda kurekebisha hizo taarifa na wale waliokupotosha ukishirikiana na kamati”alisema Katarina
Katika zoezi la kurejesha fedha hizo mkuu wa mkoa wa Njombe ameunda vikosi kazi vidogo vinavyoongozwa na wakuu wa wilaya ambavyo vinakwenda kushirikiana na kikosi kazi cha mkoa kukusanya madeni hayo,huku wakuu wa wilaya wakiwa tayari kupambana na kurejeshe fedha hizo
“Jambo hili limesababisha baadhi ya waliokopa kukimbia nyumba zao sahizi kuna watu wamekimbia,mmoja ameshajiua lazima hela za wananchi awe mtu amekufa ziludishwe”alisema Adrea Tsere mkuu wa wilaya ya Ludewa
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa anasema fedha ya umma haiwezi kuliwa na wajanja wachache hivyo wanakwenda kuifanya kazi ipasavyo ili kunusuru ushirika.
“Swala hili ni swala ambalo liliundwa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi sasa limefikia wakati halijawasaidia wananchi,tunaomba maelekezo sheria zipo utaratibu upo sisi tupo tayari kufanya hiyo kazi kwa kushirikiana na idara zingine katika kufuatilia hayo madeni”alisema Hamis Issa
Katika madeni hayo wadaiwa wa vyama vya ushirika kutoka wilaya ya Njombe wanadaiwa kiasi cha zaidi ya bil 5.3,Ludewa mil 191, Makete mil 498 wakati Wanging'ombe ikiwa ni zaidi ya mil 383 .
0 comments:
Post a Comment