Wednesday 14 December 2016

TAARIFA MUHIMU KUTOKA JKT KWA WANAFUNZI WA FORM 6 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA JKT AWAMU YA PILI 2016

...


TAARIFA KWA UMMA
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linapenda kutoa ufafanuzi kwa umma, juu ya vijana waliohitimu kidato cha sita mwezi Mei mwaka 2016 na kutakiwa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria Opereshani Magufuli awamu ya pili.
Vijana wa Mujibu wa Sheria wanaotakiwa kuripoti kwenye makambi ya JKT waliyopangiwa  ni wale wanafunzi wote waliomaliza kidato cha sita mwezi Mei mwaka 2016, ambao hawakuchaguliwa kwenye mafunzo ya JKT Mujibu wa Sheria Operesheni Magufuli awamu ya kwanza na hawakupata nafasi ya kujiunga na vyuo vya elimu ya juu.
Iwapo kuna muhitimu yeyote ambaye jina lake limetajwa kwenye orodha ya vijana wanaotakiwa kujiunga na mafunzo ya JKT Mujibu wa Sheria Operesheni Magufuli awamu ya pili na tayari ameshajiunga na chuo cha elimu ya juu, anatakiwa kuandika barua ya kuomba kuhairisha kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria, akiambatisha  vithibitisho vya yeye kuwa mwanachuo wa chuo cha elimu ya juu.
Barua hiyo itumwe kwa Mkuu Jeshi la Kujenga Taifa, Makao Makuu ya JKT, Sanduku la Posta 1694, Dar Es Salaam au iwasilishwe kwa mkono Makao Makuu ya JKT.
Aidha, JKT inaukumbusha umma tena, hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa kijana yeyote ambaye amechaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria Operesheni Magufuli awamu ya pili na amekaidi kuhudhuria mafunzo hayo bila ya sababu zilizotajwa hapo juu.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya JKT
Tarehe 13 Desemba 2016
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger