Monday 26 December 2016

MAOMBI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU,SERIKALI KUFANYA UPYA UHAKIKI WA FOMU ZA MAOMBI

...



Serikali imesema inaanza uhakiki upya, kwa kupitia fomu zote za maombi zilizowasilishwa na wanafunzi kwenye bodi ya mikopo, baada ya kubaini kuwa idadi kubwa ya wanafunzi walioomba mikopo ya elimu kupitia bodi ya mikopo nchini wamejaza taarifa za uongo.

Profesa Simon Msanjila ambaye ni Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia amesema haya wakati wa mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya , akisema serikali imeanza uhakiki mara moja kwa kupitia fomu zote zilizowasilisha kwenye bodi ya mikopo , na atakaye bainika kuwa amejaza taarifa zisizo sahihi atafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Katika mahafali haya wanafunzi zaidi ya 800 wanehitimu kozi mbalimbali zikiwemo za uhandisi, usanifu wa majengo, umeme na tehama.

Awali Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya Profesa Mark Mwandyosa ameandaa mhadhara ulioshirikisha wanazuoni na wasomi mbalimbali ,na kumtaka Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Joseph Msambichaka kufundisha watanzania sayansi na teknolojia, na sio teknolojia pekee, ili kuandaa wanasayansi ukilinganisha na wahitimu wengi wanaohitimu chuoni hapo ambao wanajikita zaidi kwenye teknolojia.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger