Saturday 3 December 2016

SERIKALI KUAJIRI WALIMU WAPYA MWAKA WA FEDHA 2016/17

...


Baada ya serikali kusitisha utoaji wa ajira mpya ili kupisha zoezi la uhakiki wa watumishi wa umma nchi nzima.Imepanga kutoa ajira mpya kwa waalimu 35,000 katika mwaka wa fedha wa 2016/2017.

Hayo yamesemwa Disemba 2, 2016 na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Suleiman Jaffo katika kikao cha maelekezo ya utendaji kazi kwa watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Jaffo amesema watakao ajiriwa ni wale waliohitimu kozi za ualimu mwaka jana na waliohitimu mwaka huu.

Kuhusu kikao cha maelekezo kwa watumishi wa umma, amewaagiza Wakurugenzi wa Idara wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Manispaa ya Ilala kuwapangia malengo ya kazi wakuu wao wa idara ili kupima utendaji kazi wao.

“Kila Mkurugenzi hakikisha mnakaa na wakuu wa idara muwekeane malengo ni nini cha kufanya katika mwaka wa fedha husika, wapo watakao tekeleza malengo hayo na wapo wasiotekeleza na kwamba hapo utajua utendaji kazi wao,” amesema na kuongeza.

“Wakuu wa idara pia wakae na watumishi wa chini ili kufanikisha utekelezaji wa malengo hayo. Tunataka utendaji kazi wa watumishi ujibu matatizo na kero za wananchi.”

Aidha, Jaffo amewataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa kujiamini ili kuboresha utendaji kazi wao.

“Wafanyakazi wafanye kazi kwa kujiamini na kutumia elimu zao na wasio waadilifu wawe waadilifu ili kuepusha migogoro wasifike ofisini na kuwaza kutumbuliwa,” amesema.

Kuhusu madeni ya watumishi wa serikali, amesema TAMISEMI imemaliza kuhakiki madeni ya watumishi hao na kwamba hivi karibuni watalipwa fedha zao.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger