Wednesday, 23 November 2016

TAARIFA KWA UMMA: KUONGEZWA KWA MUDA WA KUFANYA MAOMBI YA UHAMISHO KATIKA KOZI ZA ASTASHAHADA (CHETI) CHA UALIMU ELIMU YA MSINGI NA AWALI NA STASHAHADA (DIPLOMA) YA UALIMU ELIMU YA SEKONDARI KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

...

 
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
TAARIFA KWA UMMA

KUONGEZWA KWA MUDA WA KUFANYA MAOMBI YA UHAMISHO KATIKA KOZI ZA ASTASHAHADA (CHETI) CHA UALIMU ELIMU YA MSINGI NA AWALI NA STASHAHADA (DIPLOMA) YA UALIMU ELIMU YA SEKONDARI KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017


Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu Waombaji wote waliochaguliwa katika kozi mbalimbali za Astashahada (Cheti) na Stashahada (Diploma) na Umma kwa ujumla kuwa dirisha la maombi ya uhamisho lilifungwa mnamo tarehe 21 Novemba 2016 ili kuruhusu uteuzi wa awamu ya tatu kwa waombaji wa uhamisho.

Hata hivyo, Baraza linapenda kutoa taarifa kuwa muda wa maombi ya Uhamisho kwa kozi za Astashahada (Cheti) ya Ualimu Elimu ya Msingi na Awali na Stashahada (Diploma) ya Ualimu Elimu ya Sekondari zinazotolewa kwenye Vyuo vya Ualimu vya Serikali umeongezwa kuanzia tarehe 23 Novemba 2016 hadi 27 Novemba 2016. Mwombaji aliyechaguliwa ataweza kuomba uhamisho kutoka chuo ama kozi moja kupitia kwenye ukurasa wake binafsi (profile) tu. Uhamisho huu utategemea nafasi zilizopo na ushindani. Orodha ya Vyuo na Programu zenye nafasi inapatikana hapa.

Baraza pia linawahimiza wale wote walioomba kozi nyingine kupitia Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS) na hawakuchaguliwa na wana sifa za kujiunga na mafunzo haya ya Ualimu, kutuma maombi mapya kwenye vyuo na kozi hizo kupitia kurasa zao binafsi (profile). Mwombaji anaweza kufanya maombi haya kwa kubofya kitufye cha “Change Category/Badilisha Kada” kilichopo kwenye ukurasa binafsi wa mwombaji. Maombi haya yatapokelewa hadi tarehe 27 Novemba 2016.

Hatua za kuomba uhamisho:
 1. Ingia kwenye ukurasa wako binafsi (profile) kwa kutumia jina la mtumiaji (Username) na neno la siri (Password) ulivyopewa wakati wa usajili
 2. Bofya kitufe kilichoandikwa “Transfer Request/Kuomba Uhamisho”, na punde ukurasa utafunguka
 3. Utafunguka ukurasa unaokuonesha chuo na kozi uliyochaguliwa awali
 4. Chagua kada unayohitaji kuhamia
 5. Chagua chuo unachohitaji kuhamia
 6. Chagua kozi unayohitaji kuhamia
 7. Mfumo utatathmini kama una sifa za kujiunga na kozi uliyochagua.
 8. Iwapo una sifa za kujiunga utaonyeshwa kitufe kilichoandikwa “Confirm Transfer Request/Kamilisha Maombi”. Bofya kitufe hicho.
 9. Utapewa muhtasari wa maombi yako ya uhamisho pamoja na kutumiwa ujumbe mfupi wa maandishi kwenye namba ya simu ya mkononi uliyoweka wakati wa usajili na barua pepe kukujulisha kwamba umekamilisha maombi.
Angalizo (Disclaimer)
 1. Kuhama chuo na kozi si lazima.
 2. Uhamisho utafanyika kwa kozi zile tu zenye nafasi na kwa vyuo ambavyo bado havijafunguliwa na kuanza masomo.
 3. Uhamisho ni kwa wale waombaji waliokwisha kuchaguliwa kupitia mfumo wa pamoja wa udahili tu.
 4. Maombi ya uhamisho yanaweza kufanyika MARA MOJA na kwa kozi moja tu.
 5. Iwapo umefanikiwa kupata uhamisho, majibu yataonekana kwenye ukurasa wako binafsi (Profile). Majibu haya pia yatatumwa kwenye namba yako ya simu kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi na kupitia barua pepe baada ya tarehe ya mwisho ya maombi (27 Novemba 2016).
 6. Uhamisho utategemea ufaulu wa waombaji na nafasi zilizopo. Hii inamaanisha kwamba wenye ufaulu wa juu ndio wenye uwezo mkubwa wa kukubaliwa kuhama.
 7. Maombi yatakayotumwa kwa barua au barua pepe hayatoshughulikiwa.
 8. Waombaji waliomba uhamisho na kukosa awamu iliyopita wataruhusiwa kuomba tena bila malipo mapya.
 9. Maombi haya ni kwa wale wanaohitaji kuhamia kwenye kozi za Astashahada (Cheti) ya Ualimu Elimu ya Msingi na Awali na Stashahada (Diploma) ya Ualimu Elimu ya Sekondari katika Vyuo vya Serikali tu.
Imetolewana
Ofisi ya Katibu Mtendaji
Baraza laTaifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)
Tarehe: 22 NOVEMBA 2016
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

TANGAZO LA TOUR MBUGA YA SAADAN

TANGAZO LA TOUR MBUGA YA SAADAN

FUNGUA PAZIA

NDOA ZA UTOTONI

Narudi nyumbani

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger