Sunday, 20 November 2016

SERIKALI KUBORESHA MAZINGIRA RAFIKI YA BIASHARA NCHINI

...

mich1
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohammed Kiganja akiongoza Wachezaji wa timu ya Taifa ya mchezo wa kabadi walipowasili jijini Dar es salaam wakitokea nchini India kwenye mashindano ya mchezo huo uliofanyika hivi karibu nchini humo .
mich2
Wachezaji wa timu ya Taifa ya mchezo wa kabadi wakiwasili jijini Dar es salaam wakitokea India kwenye mashindano ya mchezo huo uliofanyika hivi karibu nchini humo ambapo Tanzania imetolewa kwenye mashindano hayo .
mich3
mich4
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohammed Kiganja akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam wakitokea nchini India kwenye mashindano ya mchezo wa kabadi uliofanyika hivi karibu nchini humo .
Na Ally Daud-Maelezo.
SERIKALI imekusudia kuboresha mazingira rafiki ya biashara nchini ili kuwezesha utashi wa Serikali ya Awamu ya Tano katika kuifanya Tanzania kuwa nc hi ya uchumi unaoongozwa na viwanda kama inavyoelekeza Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2025.
Akizungumza hayo wakati wa uzinduzi wa kamati ya kuboresha mazingira ya biashara Tanzania jijini Dar es salaam Waziri wa Viwanda ,Biashara na uwekezaji Charles Mwijge amesema kuwa Serikali imejidhatiti kuweka mazingira rafiki kwa maendeleo ya biashara nchini.
“Ili kuweza kufikia malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi unaoongozwa na viwanda kama inavyoelekeza Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2025 ni lazima kuboresha mazingira ya biashara ambayo ni rafiki kwa wawekezaji” alisema Mwijage.
Aidha Waziri Mwijage amesema kuwa maboresho ni  kusaidia kupata mikopo kwenye mabenki na taasisi za kifedha zitakazosaidia uwekezaji na uzalishaji wenye tija kwa maendeleo ya uchumi wa taifa letu.
Waziri Mwijage amesema kuwa Serikali itahakikisha inaboresha mazingira rafiki ya biashara ili kufikia lengo kwa kurahisisha utoaji wa vibali vya ujenzi wa viwanda kwa wawekezaji wa nje na wa ndani ili kufanya sekta ya viwanda kua endelevu Zaidi.
Mbali na hayo Waziri Mwijage amesema kwamba kwa kuwa Serikali imeamua kujenga uchumi wa viwanda  basi itahakikisha inarahisisha suala la uboreshaji wa mazingira rafiki ya biashara nchini .
Kamati hiyo iliyozinduliwa rasmi na Waziri Mwijage ina kazi ya kufanya uchambuzi wa kina katika mazingira ya kufanya biashara nchini na kutoa mapendekezo kwa Serikali juu ya kuboresha mazingira rafiki ya biashara nchini
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

TANGAZO LA TOUR MBUGA YA SAADAN

TANGAZO LA TOUR MBUGA YA SAADAN

FUNGUA PAZIA

NDOA ZA UTOTONI

Narudi nyumbani

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger