Sunday 27 November 2016

SERIKALI KUNUNUA NDEGE ZA KISASA KUIMARISHA ULINZI HIFADHI ZA TAIFA

...


SERIKALI imepanga kununua ndege za kisasa ili kuimarisha ulinzi katika Hifadhi za Taifa nchini.
Hayo yamesemwa jana na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi wakati akihojiwa na kipindi maalumu cha TUNATEKELEZA kinachorushwa hewani na kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC1).
Meja Jenerali Milanzi anasema Serikali imeweka mfumo maalumkatika  kulinda hifadhi zilizopo na ili kuweza kukabiliana na ujangili unaojitokeza katika hifadhi mbalimbali nchini.
“Sekta ya Utalii nchini inachangia pato la taifa kwa takribani asilimia 17.5 na kutoa ajira kwa zaidi ya watumishi milioni 3 katika sekta mbali mbali ya utalii nchini, hivyo ni vyema tukaweka mikakati madhubuti katika kulinda vyanzo vilivyopo” alisema Meja Milanzi.
Aidha, alisema kuwa Serikali itaendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wote watakaobainika kujihusisha na ujangili pamoja na biashara ya magogo ili kulinda hifadhi za Taifa na kuweza kuvutia watalii nchini.
Aidha Meja Jenerali Milanzi aliitaka jamii kwa ujumla kuona umuhimu wa kutumia nishati mbadala ili kulinda misitu iliyopo kwa kutunza mazingira na hifadhi za taifa.
Mbali na hayo Meja Jenerali Milanzi alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazovutia watalii wengi kutoka Marekani na Uingereza hivyo kuwataka wananchi kuzingatia sheria na kanuni zinazosimamimia Hifadhi za Taifa ili kuzudi kuvutia watalii nchini.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger