Saturday 19 November 2016

Obama akutana na viongozi wa Ulaya

...

Deutschland Sechser-Treffen mit Merkel und Obama im Kanzleramt (picture-alliance/dpa/K. Nietfeld)
Viongozi wa Ulaya wako Berlin kutaka kuhakikishiwa na Rais Barack Obama wa Marekani juu ya mkondo ambao yumkini ukafuatwa na rais mteule wa Marekani Donald Trump kutokana na ahadi zake kuweza kutibua mfumo wa dunia,
Rais Obama amekaririwa akisema "Kujitolea kwetu kwa Ulaya ni kwa kudumu na misingi yake iko katika maadili tunayoshirikiana maadili ambayo Angela ameyataja,kujitolea kwetu kwa demokrasia,kujitolea kwetu kwa utawala wa sheria,kujitolea kwa utu wa watu katika nchi zetu na katika dunia. Muungano wetu wa washirika wetu wa NATO umekuwa msingi wa sera ya kigeni ya Marekani kwa takriban miaka sabini katika nyakati mbaya na nzuri na kwa kupitia marais wa vyama vyote viwili na kwa sababu Marekani ina utashi wa msingi kwa utulivu na usalama wa Ulaya."
Rais Barack Obama wa Marekani alitowa kauli hiyo katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mjini Berlin hapo Alhamisi (17.11.2016) ambao pia ilihudhuriwa na mwenyeji wake Kansela Angela Merkel wa Ujerumani.
Fadhaa ya kuchaguliwa kwa Trump imewatia wasi wasi viongozi wa Ulaya kutokana na kiongozi huyo kuhoji mkataba wa usalama uliodumu kwa takriban miaka sabini wa washirika wa Marekani chini ya kivuli cha Jumuiya ya Kujihami ya NATO pamoja na kuahidi kujitowa katika mikataba iliopatikana kwa  tabu ya mabadiliko ya tabia ya nchi na kudhibiti mpango wa nyuklia wa Iran.
Kujipendekeza kwa Putin
Kujipendekeza kwake kwa Rais Vladimir Putin wa Russia pia kumezusha masuali juu ya msimamo wake juu ya hatua ya Russia kumuunga mkono Rais Bashar al Assad katika vita vya Syria na halikadhalika dhima ya Russia katika mzozo mashariki mwa Ukraine.
Kabla ya kufanyika kwa mazungumzo hayo Obama alikuwa na matumaini ya hadhari kwamba Trump anaweza kubadili msimamo wake mara ataposhika wadhifa huo wa urais.Amesema mtu inabidi awe makini akiwa katika wadhifa huo venginevyo hutoweza kudumu kwa muda mrefu kwani matatizo yatakuja kukuumbuwa.
Obama amesema anatumai kwamba rais mteule atakuwa na mtizamo ule ule wa tija kutafuta nyanja ambapo wanaweza kushirikiana na Russia pale maadili yao, utashi wao vinakwenda sambamba lakini rais mteule atakuwa tayari kusimamama dhidi ya Russia pale inapokiuka maadili yao na kanuni za kimataifa.
Kubadilishana mawazo
Mkutano wa leo kati ya Obama na viongozi wa Uingereza, Ufaransa, Ujerumani,Italia na Uhispania ni wa kwanza kufanyika tokea kuchaguliwa kwa Trump.
Mkutano huo utatowa nafasi ya kubadilishana mawazo hadharani kwa njia isio rasmi juu ya masuala muhimu ya kimataifa mathlan mada nzito ya mapambano yanayongozwa na Marekani dhidi ya kundi linalojiita Dola la Kiislamu nchini Syria na Iraq halikadhalika suala la mzozo wa wahamiaji barani Ulaya.
Obama amesema Umoja wa Ulaya unaendelea kuwa mojawapo ya mafanikio makubwa ya kisiasa na kiuchumi duniani mafanikio ambayo hayapaswi kuchukuliwa kijujuu
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger