Friday 4 November 2016

Serikali ya Mkoa wa DAR kusomesha wanafunzi wa sayansi bure mikoa mingine igeni

...

Image result for paul makondaSERIKALI ya mkoa wa Dar es Salaam imeamua kuwasomesha wanafunzi wa kidato cha nne watakaofanya vizuri katika masomo ya sayansi na kuchaguliwa kuendelea na kidato cha tano na sita.
Kwa sasa wanafunzi wa kidato cha nne wanaendelea kufanya mtihani wao wa kumaliza elimu kwa ngazi hiyo. Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda (pichani) alieleza kuhusu uamuzi huo wakati akipokea msaada wa madawati 200 yenye thamani ya Sh milioni 20 kutoka kwa shule za Almuntazir jijini humo.
Alisema ofisi yake imeona ni vyema kuanza kwa kuwasomesha wanafunzi hao ili kuongeza idadi ya wataalamu wa sayansi katika sekta mbalimbali nchini.
Alisema pia walimu waliowafundisha wanafunzi hao watapewa fedha taslimu Sh milioni mbili kila mmoja na kupelekwa kutalii katika mbuga za wanyama na mke au mume wa mwalimu husika.
Akizungumzia mgogoro wa baadhi ya wazazi wa shule hiyo, Makonda aliwataka kutumia taratibu za kupeleka malalamiko inavyopaswa kwa kuanzia maofisa elimu wa wilaya na mkoa na si kwenda moja kwa moja wizarani. Pia, aliwashauri mawaziri kutofanyia kazi malalamiko yanayopelekwa moja kwa moja kwao.
Mwenyekiti wa Bodi ya Jumuiya ya Khoja Shia Ithna Asheri Jamaa (KSIJ), Imtiaz Lalji, inayomiliki shule hizo alisema wanampongeza Rais John Magufuli kwa juhudi zake za kukuza sekta ya elimu nchini.
“Ilikuwa aibu kubwa kwa nchi yenye misitu mikubwa kusafirisha magogo nje ya nchi huku watoto wakisota kwenye sakafu za vumbi katika mbio za kutafuta elimu,” alisema.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger