Thursday, 20 October 2016

TCU yaongeza muda wa udahili vyuo vikuu

...
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania TCU imetoa muda wa siku 3 kwaajili ya wanafunzi zaidi ya 4000 ambao wamekosa fursa ya kudahiliwa katika hawamu tatu za udahili zilizofanywa na tume hiyo
Kaimu mkurugenzi wa udahili na nyaraka wa TCU Dkt. Kokuberwa Mollel amesema udahili huo utaanza tarehe 24 hadi tarehe 26 mwezi huu kwaajili ya kozi mbalimbali ambazo bado hazijajazwa kwani tayari udahili umekamilika kwa wanafunzi wanaosomea masomo ya udaktari ambapo Jumla ya wanafunzi zaidi ya 2000 wamechaguliwa kati ya wanafunzi zaidi ya 10,000 waliotuma maombi yao
Dkt. Kokuberwa amesema wanafunzi wengi walioachwa kwenye usajili wameshindwa kutofautisha viwango vya ufaulu wao na vigezo vya vyuo husika hivyo wameaswa kuchagua kozi watakazo zikuta katika tume hiyo na kuacha kung'ang'ania kozi ambazo hawajakidhi vigezo vyake.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger