Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Magufuli ameagiza Bodi
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kutumia Sheria zilizopo kuongeza
kasi ya ukusanyaji wa madeni kwa wahitimu walionufaika na mikopo.
Rais
Magufuli ametoa agizo hilo leo jijini Dar es salaam wakati akiweka jiwe
la msingi la mradi wa ujenzi wa hosteli za wanachuo katika Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam unajengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa
gharama ya shilingi bilioni 10.
Amesema kuwa Serikali inadai takribani shilingi trilioni 2.6 kwa wahitimu walionufaika na mikopo ya Elimu ya juu.
“Serikali
inawadai wahitimu walionufaika na mikopo ya Elimu ya juu takribani
shilingi trillion 2.6 ambazo wanatakiwa kuzirudisha ili ziweze kutolewa
kama mikopo kwa wanafunzi wapya na waliopo vyuoni” alifafanua Dkt Magufuli.
Aidha
Dkt. Magufuli ameitaka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo
ya Ufundi kusimamia ipasavyo suala la utoaji wa mikopo kwa wanafunzi kwa
kuzingatia vigezo vilivyopo kwani lengo la mikopo hiyo inawalenga
watoto maskini.
Alisema
kuwa kumekuwa na baadhi ya malalamiko ya kuwa Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu inafanya zoezi la ugawaji wa mikopo hiyo kwa
upendeleo hivyo kuzitaka uongozi wa Wizara kushughulikia suala hilo.
Mbali
na hayo Rais Magufuli amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kutimia mikopo
hilo kwa malengo mazuri katika kujinufaisha na masuala ya Elimu.
Naye
Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce
Ndalichako alisema kuwa mradi wa ujenzi wa hosteli hizo utasaidia
kuwahudumia wanafunzi 3,840 ambapo unatarajiwa kuisha mwishoni mwa mwezi
Desemba 2016.
Katika
hatua hiyo Prof. Ndalichako alisema kuwa wanafunzi waliodahuiliwa kwa
mwaka huu wapo 58,000 hivyo suala la wanafunzi 66,000 kukosa mikopo hiyo
ni upotoshaji unaofanya na baadhi wa watu.
Mradi
wa Ujenzi wa Hosteli za wanachuo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
wenye majengo 20 kila jengo gorofa nne zenye vyumba 12 unatarajiwa
kukamilika mwishoni mwa Desemba mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment