Na Eleuteri Mangi-Maelezo
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameridhia
na kusaini Miswada mitano kutumika kama Sheria kamili za nchi.
Hayo
yamesemwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job
Ndugai mara baada ya kufungua Mkutano wa nne wa Bunge la 11 leo mjini
Dodoma.
Miswada
iliyoidhinishwa na Rais ni pamoja Sheria ya Fedha na Matumizi ya mwaka
2016, Sheria ya Fedha namba 2 ya mwaka 2016, Sheria ya Marekebisho ya
Sheria Mbalimbali ya mwaka 2016, Sheria ya Marekebisho ya Sheria
Mbambali namba 2 na 4 ya mwaka 2016 na Sheria ya Marekebisho ya Ununuzi
ya Umma namba 5 ya mwaka 2016.
Aidha,
Mhe. Spika amewakumbusha Wabunge kusoma na kuelewa kila kinachokuja
Bungeni ili waweze kutekeleza majukumu yao ya kibunge ipasavyo kwa niaba
ya wananchi waliowatuma kufanya kazi hiyo ili kuwaletea maendeleo.
Wabunge
wametakiwa kutekeleza majukumu hayo ya uwakilishi wa wananchi ili
waweze kujadili masuala mbalimbali kwa kuzingatia haki, ustahimilivu,
busara, hekima na kutumia lugha ya staha katika mijadala ya Bunge.
Vile
vile Mhe. Spika amempongeza Naibu Spika Dkt. Tulia Akson kuongoza vema
mkutano wa tatu wa Bunge ulioanza Aprili 19 na kumalizika Juni 30 mwaka
huu kwa kushirikiana na wenyeviti wa Bunge Andrew Chenge, Mussa A. Zungu
na Najima Giga.
Katika
hatua nyingine Mhe. Spika amemshukuru Rais Dkt. Magufuli, Wabunge wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Watanzania wote walimuombea
alipokuwa kwenye matibabu nje ya nchi pamoja na Madaktari waliomhudumia
akiwa kwenye matibabu na kumshukuru Mungu kwa kumwonesha upendo
alipokuwa kwenye mapito ya kuugua.
Katika
mkutano huo wa Bunge yameulizwa maswali 14 ambayo yalielekezwa kwenye
Wizara mbalimbali na kujibiwa kwa llengo la kutolea ufafanuzi masuala
yanayotekelezwa kwa Serikali.
0 comments:
Post a Comment