Tume ya
Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imeongeza muda wa udahili wa wanafunzi
wanaotarajia kujiunga na vyuo vikuu mwaka wa masomo 2016/2017 ili kuwapa
fursa waombaji ambao wana sifa lakini hawakupata vyuo kutokana na
ushindani wa vyuo na kozi walizozichagua.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa TCU Prof. Eleuther Mwageni
alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya mwenendo mzima wa
udahili kwa mwaka wa masomo 2016/2017, leo Jijini, Dar es Salaam.
“ Tume
imekamilisha awamu ya kwanza ya udahili kwa waombaji wenye sifa ya
kidato cha 6, ambapo jumla ya waombaji wote ilikuwa 55,347, waombaji
wenye sifa ni 47,203 sawa na asilimia 85.3 ya waombaji wote. Katika
waombaji hao wenye sifa waliopata vyuo ni 30,731 sawa na asilimia 65 na
waombaji 16,472 ambao wana sifa sawa na asilimia 35 hawajapata vyuo hadi
sasa, waombaji waliokosa sifa ni 8,144,” alifafanua Prof. Mwageni.
Amesema
kuwa Tume imeamua kuongeza muda wa udahili kuanzia Septemba 12 mpaka
Septemba 23, 2016 ili kuwapa nafasi waombaji wenye sifa, fursa ya kuomba
tena vyuo na kozi zenye nafasi kutokana na wengi wao kuomba vyuo na
kozi za aina moja.
Prof.
Mwageni alivitaja vyuo ambavyo vimeombwa na waombaji wengi na tayari
vimeshajaa kuwa ni Chuo cha Ardhi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo
Kikuu cha Kikatoliki cha Afya na Sayansi Shirikishi, Chuo Kikuu cha
Kikristo cha Tiba Kilimanjaro(KCMUCo) na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi
Shirikishi Muhimbili.
Pia
alizitaja kozi ambazo zimechaguliwa na waombaji wengi kuliko nafasi
zilizopo kuwa ni kozi ya Ualimu, Udaktari wa Binadamu, Ufamasia,
Uhandisi, Sayansi ya Uthamini wa Ardhi na Sheria. Alitoa mfano wa kozi
ya Ualimu Chuo Kikuu Kishiriki cha Ualimu Dar es Salaam ilikuwa na
waombaji 15,803 wakati nafasi ni 1,000.
Hivyo
amewashauri waombaji waliokosa nafasi kuomba vyuo na kozi zisizo na
ushindani ili waweze kupata nafasi kwa awamu hii ya pili.
Aidha
Tume hiyo imepunguza viwango vya udahili kwa waombaji wenye sifa ya
stashahada kutoka GPA 3.5 mpaka 3.0. Hivyo wamewataka waombaji wenye
vigezo hivyo kuomba vyuo na kwa wale waliomba awamu ya kwanza
hawatatakiwa kuomba tena bali kusubiri matokeo ya waombaji wenye sifa ya
stashahada
0 comments:
Post a Comment