Mkutano wa Nne wa Bunge umemalizika huku ukiacha sintofahamu baada ya Ukawa kushindwa kukutana na Spika wa Bunge, Job Ndugai kujadili mgogoro kati yao na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson.
Kikao cha Bunge cha Mei, Ukawa walisusia vikao vyote vilivyoongozwa na Naibu Spika wakidai alikuwa akiminya demokrasia.
Hali hiyo, ilitokea wakati Spika Ndugai alipokuwa nje ya nchi kwa matibabu na aliporejea aliahidi kufanya maridhiano kati ya Ukawa na Dk Tulia kwenye Bunge lililomalizika jana.
Jana, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisema maridhiano yaliyokuwa yafanywe na Ndugai kati ya Ukawa na Dk Tulia hayakufanyika, kwa kuwa aliyeahidi hakuitisha kikao chochote.
Alisema kurejea kwao bungeni kulitokana na nasaha za viongozi wa dini waliokutana nao kabla ya vikao vya Bunge.
“Tukarudi bungeni na kufanya shughuli zetu katika mazingira hayohayo magumu,”alisema Mbowe.
0 comments:
Post a Comment