Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu waombaji wote wa kozi za Ualimu kupitia Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS) na Umma kwa ujumla kuwa matokeo ya waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya Ualimu vya Serikali yamekamilika. Aidha, Majina ya waombaji waliochaguliwa kwa kila kozi itolewayo na chuo husika yameshakabidhiwa vyuoni na yanaweza patikana pia kupitia kurasa (Profile) zao binafsi pia kupitia mfumo wa Matokeo kwa kubonyeza hapa.
Kwa wale ambao hawakuchaguliwa wanaweza pata sababu za kutochaguliwa kwao kupitia kurasa zao binafsi (profile) kama vile:
- Sifa za muombaji kuwa pungufu kulinganisha na sifa za chini za kozi husika;
- Nafasi za mafunzo katika chuo na kozi husika kujaa kutokana na ushindani wa waombaji wenye sifa za juu zaidi; na
- Kutoambatanisha vyeti vya matokeo ya masomo kwa baadhi ya waombaji.
Waombaji ambao hawakuchaguliwa wanashauriwa kusoma kwa makini sababu hizo na kufuata ushauri unaotolewa ili kuweza kuchaguliwa katika uteuzi unaofuata bila gharama ya ziada.
Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji
NACTE
Tarehe: 14 Septemba, 2016
0 comments:
Post a Comment