Wednesday 21 September 2016

Aliyemuua Trafiki Afikishwa Mahakamani

...

Mkazi wa Mbezi Africana Dar es Salaam, Amani Elikana (32), amefikishwa   katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni akituhumiwa kumuua Askari wa Usalama Barabarani, Sajenti Mensali wa Kituo cha Polisi Mabatini – Kijitonyama.

Akisoma hati ya mashtaka jana mbele ya Hakimu, Caroline Kiliwa, Wakili wa Serikali, Amani Mghamba alidai  mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Julai 22 mwaka huu eneo la Kijitonyama.

“Mtuhumiwa inadaiwa kwamba siku hiyo kwa makusudi  ulimuua askari mwenye namba D. 8254 Sajenti Mensali kinyume cha sheria ya Jamhuri ya Muungano,” alidai Mghamba.

Hakimu Kiliwa alisema mtuhumiwa hapaswi kujibu kitu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo hivyo shtaka hilo liliahirishwa  hadi Oktoba 4 mwaka huu litakapotajwa tena.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger