Saturday, 17 September 2016

MPYA:WANAFUNZI 24,616 KATI YA 55,347 WAMEKOSA NAFASI YA KUCHAGULIWA KATIKA AWAMU YA KWANZA,PCB,CBG,PCM WAONGOZA

...
 
 Wanafunzi  24,616 kati ya 55,347 waliomaliza kidato cha sita wamekosa nafasi ya kujiunga na vyuo vikuu kutokana na ushindani kwenye baadhi ya kozi, jambo lililoilazimu  Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kuongeza muda wa udahili.
Uamuzi huo wa TCU, unakuja siku moja baada ya kulegeza vigezo vya wanafunzi wa stashahada kujiunga na shahada ya kwanza katika vyuo vikuu mbalimbali nchini.
Kaimu Katibu Mkuu wa TCU, Eleuther Mwageni alisema wanafunzi waliokosa nafasi walikuwa na sifa stahiki, hivyo tume inaongeza muda wa siku 11 kuanzia Septemba 12 hadi 23 ili kutoa nafasi kwa waliokosa vyuo kufanya maombi upya kwenye kozi tofauti na za awali
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger