Thursday 3 March 2016

Wanasheria Waaswa Kutumia Taaluma ili Kulinda Maslahi ya Waajiri wao

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Wanasheria waaswa kutumia taaluma kulinda maslahi waajiri wao
Mkuu wa wilaya ya Nzega Bi. Jackline Liana amewataka Wanasheria wanapokuwa wakisimamia mashauri mbalimbali kutumia taaluma zao na kuweka weledi wa kutosha ili kulinda maslahi ya waajiri wao.
Akifungua kikao kazi cha Wanasheria wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichofanyika katika ukumbi wa Chama Cha Walimu Nzega tarehe 18 Februari,2016, Bi. Liana aliwaasa Wanasheria kuacha kuuza kesi kwani alisema kufanya hivyo ni kuwaumiza wananchi. Bi. Liana aliwataka wanasheria kuwa wazalendo zaidi kwa kujitoa na kujitolea wakati wanaposimamia mashauri mahakamani pamoja na kusimamia ipasavyo mikataba na kujiepusha na rushwa.
Aidha, Mkuu wa Wilaya aliwataka wanasheria kujiepusha na migongano ya kisheria kwakuwa wengi wao ni mawakili wa kujitegemea na kutambua kuwa wana wajibu mkubwa wa kulinda maslahi ya waajiri wao. Mafunzo hayo yalihudhuriwa na Wanasheria kutoka Halmashauri za Mji/Wilaya za Urambo,Tabora,Nzega,Uyui,Mkoa wa Tabora, Nzega, Sikonge, Igunga na Kaliua.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger