
TAARIFA KWA UMMA
TAREHE 11 MACHI 2016
Baraza
la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuutangazia umma kuwa
waombaji wenye Stashahada (Ordinary Diploma – NTA Level 6) wanaoomba
kujiunga na Shahada ya Kwanza zinazotolewa na Vyuo Vikuu (Universities)
au Vyuo Vikuu Vishiriki (Constituent Colleges of Universities)
hawataweza kufanya hivyo sasa. Hii ni kwasababu Tume ya Vyuo Vikuu (TCU)
bado haijafungua rasmi Mfumo wa Udahili wa pamoja (CAS) unaoratibiwa
kwa pamoja kati ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) na Tume
ya Vyuo Vikuu (TCU). Tume ya vyuo vikuu inatarajia kufungua mfumo huo wa
kudahili kwa waombaji wa Shahada ya Kwanza mara baada ya matokeo ya
kidato cha sita kutangazwa na Baraza la Mitihani la Tanzania
kuanzia
mwezi Mei 2016.
Hivyo
basi, ikifika muda huo ndipo waombaji wenye Stashahada (Ordinary Diploma
– NTA Level 6) wanaotaka kujiunga na Vyuo Vikuu au Vyuo Vikuu Vishiriki
kwa ajili ya kusoma Shahada ya Kwanza, wataweza kuanza kuomba
kudahiliwa kwa kupitia kwenye Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS).
Hata
hivyo, tunapenda kutoa taarifa pia kuwa kwa wakati huu, waombaji wenye
Stashahada (Ordinary Diploma – NTA Level 6) wanaotaka kujiunga na
Shahada za Kwanza zinazotolewa na vyuo vya Elimu ya Ufundi au Taasisi
zilizosajiliwa na Baraza (NACTE) waendelee kuomba kudahiliwa na Taasisi
hizo kupitia Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS) unaoratibiwa na Baraza
ambao umezinduliwa tarehe 4 Machi, 2016.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA UDAHILI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
0 comments:
Post a Comment