Waziri
wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce
Ndalichako leo amewapa siku tano wanafunzi wa chuo kikuu cha St. Joseph
tawi mama lililoko maeneo ya Mbezi Jijini Dar es salaam ili wafanye
mitihani yao ili wafunge chuo na kupisha ukarabati wa baadhi ya maeneo
ambayo yatatumika kwa ajili ya mafunzo stadi ya wanafunzi hao.
Mbali
na kutoa agizo hilo waziri ndalichako alitumia fursa hiyo kuwaomba
wanafunzi wote nchini waache kulalamika bali wasome kwa bidii na kuwa na
nidhamu ya kutosha.
0 comments:
Post a Comment