Friday 4 September 2015

POLISI WAMTIA MBARONI TAPELI SUGU..ANATEPELI WASTAAFU NCHI NZIMA

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
MTU mmoja aliyejulikana kwa jina la David Makali maarufu kama Peter Mabula amekamatwa na jeshi la polisi na kufikishwa mahakamani kwa kuwatapeli wastaafu nchini.

Kamanda wa polisi mkoani Dodoma, David Misime aliwaambia waandishi wa habari kuwa, mtuhumiwa huyo alikuwa akiwatapeli wastaafu kwa kujifanya yeye ni mtumishi wa Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

“Mtuhumiwa pia amekuwa akijifanya ni mtumishi wa Mfuko wa pensheni wa Serikali za Mitaa (LAPF), Mfuko wa Pensheni wa PSPF na Mtumishi wa ofisi ya Katibu Mkuu wizara ya Afya na kufanikiwa kuwaibia fedha kwa njia ya mtandao wastaafu kutoka katika mikoa mbalimbali.
“Wanachofanya watu hawa hupiga simu Idara mbalimbali na kujifanya wapo TAMISEMI au wizara nyingine na kuwataka wawatumie orodha ya wastaafu wa mwaka fulani pamoja na namba za akaunti zao za simu,” amesema Kamanda Misime.
Amesema kwa njia hiyo matapeli hao wamefanikiwa kupata orodha ya wastaafu kutoka katika mikoa takriban 15 hususan kutoka kwenye idara ya afya.
“Wakishapata orodha ya majina ya wastaafu na namba zao za simu, humpigia mstaafu na kujitambulisha anatokea wizarani na kwamba anashughulikia wastaafu ambao inaonekana walipunjwa kwenye mafao yao na inaonesha naye amepunjwa milioni fulani,” amesema Kamanda Misime.
Amesema watuhumiwa hao hutumia mwanya huo kuwatapeli fedha wastaafu kwamba watume fedha ili wawasaidie waweze kupata fedha zao walizopunjwa na baada ya mstaafu husika kutuma hizo fedha, mtu huyo anakuwa hapatikani tena katika simu.
Kamanda Misime amewatahadharisha wastaafu kutokubaliana na watu wa aina hiyo na idara mbalimbali zichukue tahadhari na kila mara wahakikishe kinachohitajika kinatoka katika idara husika na kwa mtu sahihi.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger