Monday 28 September 2015

MATOKEO YA AWALI KWA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA VYUO VYA AFYA,WANAFUNZI 9306 KATI YA 21228 WACHAGULIWA KUIJUNGA VYUO VYA AFYA 2015/16

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
1. Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu wote walioomba kujiunga na kozi mbalimbali za afya kwa ngazi ya Cheti (Astashahada) na Diploma (Stashahada) kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) kuwa, Uteuzi wa awali umefanyika na waombaji 9306 kati ya 21228 wameteuliwa kujiunga na vyuo mbalimbali. Matokeo ya uteuzi huo yanapatikana katika kurasa binafsi (Profiles) za waombaji.2. Waombaji wote ambao wamechaguliwa katika awamu hii wanapaswa kuthibitisha kuwa wataripoti katika vyuo walivyopangiwa na mwisho wa kuthibitidha ni Ijumaa tarehe 16 Oktoba 2015. Iwapo muombaji hatathibitisha, nafasi hiyo itatolewa kwa mwingine. Kuweza kuthibitisha bonyeza hapa

3. Kwa wale ambao bado hawajapangiwa vyuo, kurasa binafsi zenu zina maelezo yenye sababu za kutopangiwa chuo katika awamu hii na maelekezo ambayo unatakiwa kuyatekeleza ili mfumo utakapochakata uteuzi wa awamu nyingine siku ya Jumatatu 19 Oktoba 2015 idadi kubwa zaidi ya waombaji iweze kupangiwa vyuo kwani hadi sasa nafasi zipatazo 11566 hazijajazwa.

Imetolewa na:

Katibu Mtendaji

Baraza la Taifa la Elimu yaUfundi (NACTE)

27 Septemba 2015
 
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger