Aliuawa na kundi la watu walioingia katika nyumba yake kwa madai kuwa walitaka kupangisha chumba katika nyumba yake jijini Dhaka.
Alijulikana kwa kuandika taarifa za kutoamini kuwepo kwa mwenyezi Mungu na kwa kuwakosoa waumini waislamu wenye itakadi kali.
Mkewe aliyesikitishwa na mauaji hayo alisema kuwa Bangladesh kwa wakati huu ni taifa lililoko mikononi mwa Waislamu wenye itikadi kali.
Bi Chatterjee anasema kuwa laiti serikali ingetaka kuwepo kwa uhuru wa kujieleza ingeliwaadhibu waliomwua mumewe.
Hata hivyo Asha Moni alisisitiza kuwa wao pia wana haki ya kuishi nchini humo licha ya imani zao kinzani na ya waliowengi.BBC
0 comments:
Post a Comment