Saturday, 1 August 2015

MATOKEO UCHAGUZI WA KURA ZA MAONI WABUNGE CCM 2015

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Leo ni August 1,2015 Wanachama wa chama cha Mapinduzi (CCM) nchi nzima wanakusanyika katika maeneo ya matawi yao
kuchagua mgombea mmoja atakayeshindana na wagombea wengine kutoka vyama tofauti na CCM.
Mchakato wa kampeini katika mkoa huu zimetawaliwa na vituko,udhalilishaji kwa baadhi wa wagombea hivyo hata upigaji kura za maoni utakuwa hivo hivyo,hii ndiyo sababu inatufanya tufuatilie live kura hizi.Chama cha CHADEMA wao walikwisha maliza ngwe hii kwa wagombea wao nchi zima.

Kutoka Mkoani Kagera nakuletea LIVE UPDATES ikiwemo na matokeo kadri nitakavyoyapata.

Historia kidogo
Mkoa wa Kagera una majimbo tisa ya uchaguzi ambapo wabunge wawili tu wametangaza kung’atuka ambao ni Deogratias Ntukamazina wa Jimbo la Ngara na Bw Esutace Katagira wa jimbo la Kyelwa.

Saa 12:02 Adhuhuri
Hizi ni baadhi ya picha kutoka vituo mbalimbali katika kata zilizoko manispaa ya Bukoba.
wengine kutoka vyama tofauti na CCM.







Saa 10:38 Asubuhi
.Wanachama wa CCM wanaendelea na upigaji kura ingawa katika maeneo mbalimbali ya kata ya Kanyigo wilyani Missenyi wasimamizi wanalalamikia kuwepo kadi za ccm ambazo hazipo katika kitabu cha orodha ya wanachama

.Kata ya Nshambya Bukoba Mjini na maeneo mengine ya mji wa Bukoba zoezi linaendelea ingawa kuna wanachama wachache sana katika vituo.

.Mgombea mmoja katika jimbo la Bukoba(jina lake nitalitaja baada ya kupiga kura)jana aligoma kusaini makubaliano ya kutaka kila mgombea kukubaliana na matokeo na kuwa tayari kumuunga mkono atakayepitishwa .

.Wilayani Karagwe wanachama bado hawaamini macho wao kukuta wagombea wawili maarufu Gosbert Blandes(mbunge wa sasa) na Karimu Amri ambao walidaiwa kujitoa majina yao hayamo katika orodha ya wanaotakiwa kupigiwa kura.Hivyo hao wanachama siyo wagombea,baadhi ya akina mama wamegoma kupiga kura baadhi ya maeneo kwa kukosekana wagomea hao.


Saa 07:37 Asubuhi
Quote By Mathias Byabato View Post
Wagombea kwa kila Jimbo
Bukoba Mjini:
Wagombea ni
1:Balozi Khamis Kagasheki,
2:Bw.George Rubaiyuka,
3:Bw. Josephat Kaijage,
4:Bi.Elieth Projestus
5: Dr.Anathory Amani,
6:Bw.Philbert Katabazi,
7:Bw.Mujuni Katarahiya
8: Bi.Celestina Rwezaura.

BukobaVijijini
Wagombea ni
1:Bw.Jasson Rweikiza ,
2:Bw. Nazir Karamagi
3:BW.Nelson Itagasa.

Muleba Kaskazini
Wagombea ni
1: Charles Mwijage
2: Bw.Ambrose Nshala.

Muleba Kusini
Wagombea ni
1:Profesa Anna Tibaijuka,
2:Dr Adam Nyaruhuma,
3:Bw.Stivin Tumaini,
4:Bw.Flavius Kahyoza,
5:Mhandisi Buruani Rubanzibwa,
6:Muhaji Bushako
7:Kaino Mendesi
8: Bw. Erick.

Jimbo la Ngara
Wagombea ni
1:Syprian Gwassa,
2:Dr Philemon Rugumiliza,
3:Bi.Helen Adrian n
4:Bw.Wilbald Ede
5: Bw.Alex Gashaza,
6:Bw.Jelard Muhile,
7:Johakim Nchunda ,
8:Bw.Issa Samma
9: Bw.Ladslaus Bambanza.

Jimbo la Nkenge
Wagombea
1:Asumpta Mshama,
2:Diodorous Kamala,
3:Dr Mazima,
4:Bw Frolent Kyombo,
5:Bw Julius Rugemalira
6:Bw......

Jimbo la Kyerwa
Wagombea ni .
1.Innocent Seba Bilakwate,
2.Stephano Edward Katemba
3.Lameck Chacha Ng’ang’a
4.Norbeth Kobwino
5.Sinsibath Kashunju Runyogote
6.Pancrace Shwekelela
7.Awaam Ahamada Ngalinda

Jimbo la Karagwe.
1.Mwalimu Dagobati Deogratias
2.Audax Christian Rukonge
3.Innocent Luga Bashungwa
4.Gosbert Begumisa Blandes
5.Alfred Rujwahuka
6.Amoni Chakushemeire Eustad
7.Karimu Amri
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger