Saturday 1 August 2015

Makinda kutogombea ubunge

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
 

SPIKA wa Bunge, Anne Makinda amesema amekuwa mbunge kwa miaka 40, hivyo ameamua kuwaachia wengine na kuwaonya wanawake wanaogombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi mkuu ujao kutolia au kulalamika jukwaani kwani ni udhaifu mkubwa.


Hivyo amewaeleza kuwa hata wanapokumbana na changamoto mbalimbali majukwaani, wapambane na kulia usiku lakini wanakuwa ameonesha kuwa wanawake wanaweza.

Makinda alisema hayo jana wakati akifungua maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Afrika yaliyoandaliwa na Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika (WiLDAF) na kusema ifikapo Oktoba atakuwa amefikia miaka 40.

Alisema maadhimisho hayo ya mwaka huu yana kauli mbiu kuwa “Uchaguzi 2015: Zingatia Usawa wa Kijinsia kwa Mabadiliko Chanya” hivyo ni vema serikali, vyama vya siasa na jamii kuzingatia usawa wa kijinsia hasa katika nfasi za uongozi wa juu katika serikali na sekta mbalimbali.

Alisema kuna changamoto kwa wagombea na wapigakura wanawake lakini wanapaswa kuwa imara kwa kuwa na maneno kidogo, lakini vitendo vingi vyenye uhakika.

“Hata kama unakumbana na changamoto yoyote wanawake ni marufuku kulia jukwaani kuwa wananionea kwa kuwa mimi mwanamke, ni vema kulia usiku ambako watu hawakuoni lakini siyo mbele za watu kwani ni udhaifu mara ishirini,” alionya.

Makinda alisema katika utawala wake bungeni, Bunge limekuwa kielelezo cha usawa wa kijinsia kwani katika mabunge 140 Bunge la nchini limekuwa la 21.

Alisema kwa upande wa Afrika Bunge hilo katika masuala ya usawa wa kijinsia, wanawake walikuwa wanane na ikiwa ingepita katiba pendekezwa wangekuwa nafasi nzuri zaidi. Alisema kati ya wanawake wenye majimbo mwaka 2005 walikuwa 12 lakini sasa wamefika 21 na matarajio yake ni kuwa katika uchaguzi ujao wataongezeka zaidi.

Awali Mkurugenzi wa shirika hilo, Dk Judith Odunga alimpongeza Spika kwa kuwapa heshima wanawake kwa kuwa mwanamke wa kwanza kuwa spika wa bunge nchini na kumaliza kipindi cha miaka 10 salama, licha ya changamoto mbalimbali.
 
CHANZO: HABARI LEO
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger