Sunday, 22 December 2024

AJALI YA BASI YAUA WATU 11 , KUJERUHI KAGERA



Watu 11 wamefariki dunia huku 16 wakijeruhiwa katika ajali ya basi iliyotokea katika Kijiji cha Kabukome Kata ya Nyarubungo kwenye mlima wa kuanzia pori la Kasindaga lililopo Wilaya ya Biharamulo na Muleba Mkoani Kagera.


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera Blasius Chatanda amelitaja gari hilo kuwa lina namba za usajili T 857 DHW linalofanya safari zake kati ya Kigoma na Bukoba ambapo liliacha njia na kupinduka na hatimaye kusababisha vifo vya Watu 11 kati ya hao Wanaume ni wanne Watu wazima na Wanawake watano, Mtoto wa kiume mmoja na Mtoto wa kike mmoja na miili yote ipo Hospitali teule ya Wilaya ya Biharamulo huku kati ya 16 waliojeruhiwa baadhi yao wanaendelea vizuri na muda wowote wataruhusiwa.


Amesema kuwa chanzo cha ajali ni kufeli kwa mfumo wa gari zima "Gari hili lilipotoka Biharamulo kwenda Bukoba lilimpitiliza kituo cha kushuka Mtoto mmoja sasa Ndugu zake wakapiga simu kuwa wamempitisha, Dereva akakutana na Coaster kwenye mlima ule kwa sababu ya haraka akasimamisha gari mlimani konda akashuka na mtoto ili amuwaishe kwenye gari ambalo linawahi Biharamulo kwa bahati mbaya mfumo wa gari ukagoma, mfumo wa breki mfumo wa gia vyote vikagoma gari likaanza kuserereka na likawa limemshinda Dereva likatoka nje ya barabara na kubinuka na Watu wengi wamepoteza maisha kwasababu walilaliwa na gari"

CHANZO - MATUKIO DAIMA 
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI DESEMBA 22,2024




 
Share:

Saturday, 21 December 2024

TANZANIA, SAUDI ARABIA KUIMARISHA USHIRIKIANO SEKTA YA NISHATI


đź“Ś Waziri Kapinga afanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Nishati Saudi Arabia

đź“Ś Wajadili ushirikiano katika Mafuta, Gesi Asilia, Nishati Jadidifu na Nishati Safi ya Kupikia

đź“Ś Saudi Arabia yaeleza kutambua juhudi za Tanzania kuimarisha Sekta ya Nishati

đź“ŤSAUDI ARABIA

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na Saudi Arabia katika kuimarisha Sekta ya Nishati hususan katika Mafuta na Gesi, Nishati Safi ya Kupikia na Nishati Jadidifu.

Mhe. Kapinga amesema hayo wakati alipokutana na Naibu Waziri wa Nishati wa  Saudi Arabia,         
Mhandisi Mohammed  Albrahim katika Mji wa Riyadh tarehe 19 Desemba, 2024 nchini Saudi Arabia.

Amesema kuwa, Tanzania imekuwa ikishirikiana na nchi hiyo kwa muda mrefu katika Biashara ya Mafuta na Maeneo Mengine ya Maendeleo hivyo mahusiano hayo yanaendelea kuimarika zaidi kwa kuwa mahitaji ya nishati yanazidi kuongezeka   na uwekezaji zaidi unahitajika katika kuendeleza Sekta ya Nishati ikiwemo Mafuta na Gesi Asilia, Nishati Jadidifu na  Nishati Safi ya Kupikia.

"Mahusiano ya Tanzania na Saudi Arabia katika Sekta ya Nishati ni ya muda mrefu, nchi hizi mbili zimekuwa na lengo la kuboresha ushirikiano wao katika kuendeleza sekta ya nishati." Amesema Kapinga

Aidha, ameeleza kuwa Tanzania kama nchi inayoendelea inahitaji kuimarisha zaidi miundombinu yake ya nishati katika maendeleo hivyo imekuwa  ikishirikiana na nchi zenye uzoefu mkubwa katika sekta hizo ili kupata matokeo chanya kwa kuwa nishati ni msingi mkuu wa maendeleo.

Amesema Saudi Arabia imekuwa ikijulikana kwa uwezo wake mkubwa katika uzalishaji wa mafuta na gesi, na imekuwa ikiwekeza katika maeneo mbalimbali ya Dunia, ikiwemo Afrika Mashariki, ambapo kwa upande wa Tanzania yenye rasilimali za Gesi Asilia na viashiria vya uwepo wa Mafuta inapata  uzoefu, ujuzi na teknolojia kutoka Saudi Arabia katika kuchimba, kusafisha na kusafirisha mafuta na gesi pamoja na kuimarisha miundombinu ya rasilimali hizo.

Vile vile, Mhe. Kapinga amesema kuwa kuimarika kwa Sekta ya Nishati nchini kutaiweza nchi kuweza kusambaza Umeme utakaozalishwa nchini kwa nchi jirani ambazo zimeonyesha nia ya kuhitaji Nishati.

Kwa upande wake, Waziri wa Nishati wa Saudi Arabia, Mhandisi Mohammed  Albrahim amesema kuwa nchi yake inajipanga kuwekeza zaidi katika ujenzi wa Miundombinu ya barabara, utunzaji wa mazingira na kuwekeza zaidi katika Sekta ya Mafuta na Gesi,  Nishati Jadidifu na  Nishati safi ya kupikia. 

Amesema, pamoja na kwamba wamegundua mafuta mengi, wanajipanga kuendana na sera za kidunia kwa kuwekeza katika Nishati Safi ambayo inahifadhi mazingira. 

Ameongeza kuwa, Saudi Arabia inatambua  juhudi zinazofanywa na Tanzania kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt
Samia Suluhu Hassan kwa kuwa kinara katika kutekeleza Ajenda wa Nishati safi ya kupikia.

Share:

TBS YAWATAKA WAINGIZAJI WA BIDHAA ZA CHAKULA NA VIPODOZI KUSAJILI BIDHAA ZAO


WAFANYABIASHARA wanaoingiza bidhaa za chakula na vipodozi kutoka nje ya nchi wametakiwa kusajili bidhaa hizo Shirika la Viwango Tanzania (TBS), kwa kuwa kufanya hivyo ni kutekeleza matakwa ya sheria.

Wito huo umetolewa na Meneja wa Usajili wa Bidhaa na Majengo wa TBS kutoka Idara ya Udhibiti Ubora TBS, Habakuki Kalebo, wakati akizugumza na waandishi wa habari, leo Desemba 19,2024 jijini Dar es Salaam.

Amesema usajili wa bidhaa za chakula na vipodozi unafanyika kupitia mfumo wa Online wa TBS ambao unaitwa OAS, ambapo ili mtu aweze kusajili bidhaa zake anatakiwa kujisajili kupitia mfumo huo.

Amesema usajili wa bidhaa na majengo ya biashara ni takwa la kisheria kwa mujibu wa Sheria ya Viwango 2 ya Mwaka 2009 ambayo imefanyiwa mabadiliko katika Sheria ya Fedha ya Mwaka 2019.

Kalebo amesema kwa mujibu wa sheria hiyo mfanyabiashara yeyote yule anatakiwa kusajili bidhaa zake chakula, lakini pia kusajili na majengo.

"Sheria hii inasema mtu yeyote yule haruhusiwi kuzalisha, kuingiza bidhaa ya chakula au vipodozi ndani ya nchi wala kusambaza, wala kuuzwa kabla bidhaa hiyo haijasajiliwa na TBS," amesema Kalebo.

Aidha, amesema sheria hiyo inaeleza kwamba mtu yeyote yule haruhusiwi kuuza, kusambaza au kuhifadhi chakula au vipodozi katika jengo lolote lile ambalo halijasajiliwa na TBS .

Amefafanua kuwa hiyo inafanyika ili kulinda ubora wa bidhaa, usalama na kulinda umma ili uweze kutumia bidhaa ambazo ni salama kwa lengo la kulinda afya za watumiaji.

"Umuhimu wa kusajili bidhaa ni kuhakikisha ubora umezingatiwa na umehakikiwa vizuri na kuhakikisha usalama wa bidhaa hizo umezingatiwa vizuri.

Ikumbukwe kuwa hizo bidhaa watu wanakula zinaingia ndani ya mwili, kwa hiyo zisipokuwa zimethibitishwa ubora wake, kuthibitishwa usalama wake zitakuwa na athari kubwa kwenye afya za watu na zinaweza kupelekea kifo pamoja na magonjwa mengine.

Kwa hiyo lengo la TBS ni kuhakikisha bidhaa zote zinazoingia lazima ziwe zinakidhi hayo matakwa, iwapo mwananchi atanunua bidhaa ambazo hazijatibitishwa anaweza kukutana na madhara ya kiafya." Amesema

Ametoa wito kwa wananchi wanapokwenda kununua biadhaa kuangalia kama bidhaa hiyo ina nembo ya ubora ya TBS. " Lakini bidhaa ambazo tunazisajili kutoka nje ya nchi kuna zile ambazo zina nembo ya ubora na zile ambazo hazina nembo ya ubora," amesema.

Aidha, amesema usajili wa bidhaa ambazo zinazalishwa ndani ya nchi unafanyika kukupitia utaratibu unaoitwa Product Certification kwa kuwapatia leseni wazalishaji yakutumia nemno ya ubora na hapo moja wanakuwa wamesajili kupitia huo utaratibu.

Kwa upande wa majengo, Kalebo amesema yanasajiliwa ili kuhakikisha bidhaa za vipodozi pamoja na bidhaa za vyakula haziathiriwi na mazingira ambayo vinatunzwa .

"Kwa hiyo tunakagua majengo ili kujiridhisha kuwa yana mazingira ambayo ni wezeshi ambayo hayasababisha kuharibika kwa ubora na usalama wa bidhaa husika," amesema Kalebo,

Ameongeza kwamba bidhaa zozote zile ambazo zinagundulika zimeingia nchini kinyemela na zile ambazo huenda zina madhara kwa watumiaji kama vile vipodozi ambavyo vinakuwa na viambato sumu, TBS huwa inahuwisha taarifa hizo kwenye kanzi data yake kila mwezi na kuorodhesha bidhaa zile ambazo zinaonekana zilikuwa na viambata sumu na hazitakiwi kutumika nchini.

Ameongeza kwamba wananchi wanashauriwa kutembelea tuvuti ya TBS kuweza kujua bidhaa ambazo zimesajiliwa na shirika hilo.
Share:

Friday, 20 December 2024

MRADI WA BRT WACHOCHEA URAFIKI KATI YA CHINA NA TANZANIA


Mwakilishi wa Mkandarasi kutoka kampuni ya Ujenzi wa Mawasiliano ya China(CCCC) You Xudong akionyesha namna mradi huo awamu ya nne sehemu ya tatu unaotekelezwa Kivukoni Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Mkandarasi kutoka kampuni ya Ujenzi wa Mawasiliano ya China(CCCC) You Xudong akionyesha namna mradi huo awamu ya nne sehemu ya tatu unaotekelezwa Kivukoni Jijini Dar es Salaam.

Na Hellen Kwavava-DAR ES SALAAM

MRADI wa mabasi yaendayo kwa haraka (BRT) umekuwa ni kichocheo cha ukuaji wa Uchumi katika Jiji la Dar es Salaam pamoja na kurahisisha hali ya usafiri kwa Jamii hiyo.

Meneja Usalama Tawi la Tanzania, kutoka Kampuni ya Ujenzi na Mawasiliano ya China (CCCC), Li Yuling amesema hayo jijini Dar es Salaam alipozungumza na Waandishi wa habari katika kuadhimisha siku ya Jiao Zhu China -Tanzania.

Wakati anazungumzia mradi huo wa BRT, awamu ya nne sehemu ya tatu amesema mradi huo ni sehemu muhimu ya urafiki wa  China na Tanzania, na kwamba sio tu unaboresha usafiri wa umma wa Dar es Salaam ambao ni mji wa kibiashara wa Tanzania.

 "Mradi huu unajumuisha ujenzi wa vituo muhimu vya usafiri, vituo vya mabasi na vifaa vingine vya trafiki. Unalenga kuboresha ufanisi wa usafiri wa mijini, kupunguza msongamano na kuimarisha hali ya usafiri ya wakazi wa eneo hilo," amesema.

Li amesema nia yao kubwa katika kuadhimisha siku hii ni kuonyesha watanzania juu ya dhamira ya makampuni ya Kichina katika maendeleo ya miundombinu inayoyafanya.

"Ili kuendeleza mafanikio hayo na kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Tanzania, kampuni ya ujenzi ya China tawi la Tanzania imekutana na waandishi wa habari, kuzungumzia mafanikio hayo," amesema.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkandarasi katika mradi huo, You Xudong amesema mradi huo unaendelea katika eneo la Kivukoni, utachukua miezi 18.

Amesema wanajenga jengo la ulinzi, choo, jengo la tiketi namba moja na jengo la tiketi namba mbili.

Pamoja na hayo Mradi huo unaoendelea katika eneo la kivukoni jijini Dar es Salaam umeweza kushirikisha wanafunzi wazawa wanaosomea uhandisi kutoka Taasisi ya teknolojia Dar es Salaam(DIT).

Kwa upande wake Mwalimu Alvin Rujweka kutoka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam ( DIT), amesema wamekuwepo na wanafunzi wao wanaosomea uhandisi kwa ajili ya masomo ya vitendo katika kampuni hiyo ya kichina ya CCCC.

"Wanafunzi wanaoandaliwa kuwa wahandisi, wanapewa elimu ya vitabu na vitendo.  Njia nyingine tunawapeleka kwenye miradi mbalimbali inayoendelea nchini, tunawaunganisha na soko kupitia fani walizosomea, " amesema.

Naye Mhitimu wa Diploma  DIT mwaka huu 2024, Benson Mbilinyi amesema amepata nafasi ya kujiunga na kampuni hiyo ya CCCC na anafanya kazi kama mhandisi msaidizi Jambo ambalo anajivunia kupata nafasi hiyo hasa kwa vitendo.


Hata hivyo Mhitimu huyo ameendelea kutoa Ushauri kwa wanafunzi kujitokeza kwenye fursa mbalimbali zinazojitokeza ili kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondoa utegemezi katika Jamii.

Share:

Wednesday, 18 December 2024

KAPATA MCHUMBA ILA KIFAFA KINAMZUIA ASIOLEWE JAMANI

Naitwa Pendo Ambani kutoka Ruvu, Tanzania, kwa muda mrefu tulikuwa tunazunguka na ndugu yetu ambaye alikuwa anaugua ugonjwa wa kifafa ambao ni hatari sana kwa sababu mtu anaweza kuanguka popote pale hata eneo la hatari.

Huyu ndugu yetu ambaye ni mtoto wa shangazi yangu, tulimpeleka Hospotali za kiserikali na kibinafsi ili aweze kupata tiba ila ikawa anapata nafuhu kwa wakati fulani kisha kinarudi tena kwa nguvu kubwa ajabu.  

Tuliamua kumtafutia dawa za mitishamba kutoka wa waganga mbalimbali lakini bado hakupona licha ya waganga kutuambia angepona moja kwa moja lakini kadiri siku zilizovyokuwa zinasonga tulijikuta kama famili tunazidi kutoa fedha nyingi bila kupata majibu yaliyo sahihi.

Ugonjwa huu ulitufanya baadhi ya ndugu tushindwe kujikita katika shughuli za uzalishaji mali maana ilikuwa ni lazima mtu mmoja kubaki nyumbani kumuangalia asije akaangukia maeneo hatari kama kwenye moto na umeme wa ndani.

Kilichoumiza zaidi ndugu yetu huyu alikuwa amefikia umri  wa kuoa kabisa na tayari alishapata mchumba lakini ugonjwa huo ndio ukawa ni kikwazo kwake, wasichana wote wa rika lake tayari walishaolewa.

Kuna siku nikiwa natokea mjini katika kutafuta zangu riziki niliamua kuingia mtandaoni kusoma kiundani kuhusiana na ugonjwa wa kifafa na tiba yake ya uhakika ni ipi.

Katika kusoma kwangu niliweza kubaini Dr Bokko anatoa tiba ya ugonjwa huo na mengine kama kisukari, upungufu wa nguvu za kiume, presha, kisonono, kaswende, miguu kuwaka moto n.k.

Mara moja niliwasiliana na Dr Bokko kwa namba zake +255618536050 na akapendekeza tumpeleke mgonjwa ofisini kwake kwa ajili ya tiba, tulipofika alitupokea vizuri, alimfanyia matambiko yake.

Ndani ya siku chake ndugu yetu afya ilizidi kuimarika ingawa tulikuwa na wasiwasi kuwa anaweza kurejea kwenye hali yake ya kawaida lakini haikuwa hivyo hata mara moja.

Baada ya miezi mitatu ndugu yetu alionyesha kupona kabisa na yeye mwenyewe akasema anataka kuanza kazi.

Kweli akaanza kwenda kazini kwa mara ya kwanza baada ya muda mferu, huko kazini kwake aliweza kumpata mchumba ambaye hivi karibuni walifunga ndoa na tukawafanyia sherehe kubwa sana.

Sisi kama familia tunamshukuru sana Dr Bokko na ndugu yetu kasema sehemu ya vitu alivyozawadi kama zawadi atampatia iwanga kama zawadi kwa kumponya.

Sisi pia kama familia tumepanga kukutana tuzungumze tuone ni kwa namna gani tunaweza kumpatia chochote kitu Dr Bokko kama shukrani yetu kwake. Mpigie kwa namba +255618536050.

Mwisho.


Share:

BILIONEA MULOKOZI ANUNUA NDEGE BINAFSI, ATUA MANYARA



Na Ferdinand Shayo ,Manyara .


Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited David Mulokozi amenunua ndege binafsi aina ya Helkopta ambapo ametua kwa mara ya kwanza katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa Stedium akiwa ameambatana na familia yake.

Mulokozi anaingia miongoni mwa Watanzania wachache wanaomiliki ndege binafsi ambapo amesema kuwa kampuni yake imekua ikikua siku hadi siku na kuonyesha vitu vya tofauti .

“Hakuna Mtu alitegemea kuwa Manyara kunaweza kuwa na helkopta ni mambo mengi yanaanza ,Wafanyabiashara wengi wanajifunza, kila mtu anaruhusiwa kumiliki chombo hichi inawezekana” Anaeleza David Mulokozi.

Amesema kuwa ndege hiyo itasaidia katika utoaji wa huduma katika kampuni yake inayojihusisha na uzalishaji wa vinywaji changamshi.

Mulokozi ameiomba serikali ijenge kiwanja cha ndege ili ndege nyingi zaidi ziweze kutua mkoani Manyara .

Kwa upande wao wakazi wa mkoa wa Manyara waliofika na kushuhudia helkopta hiyo ikitua akiwemo Melkiori Enyasi anaelezea furaha yake baada ya kuona ndege binafsi ya kwanza ya mkazi wa mkoa wa Manyara ikitua katika ardhi nyumbani.

Enyasi amempongeza Mulokozi kwa kununua ndege binafsi itakayochochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi .




Share:

REA YATENGA FEDHA KUHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI TANGA

Na Hadija Bagasha Tanga,

WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) imetenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa wa miradi ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ikiwemo gesi katika maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji lengo likiwa ni kuwezesha huduma ya nishati safi ya kupikia na hatimaye kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa inayosababisha mabadiliko ya tabia Nchi.

Hivyo kupitia mpango huo itatoa mitungi ya gesi 26,040 kwa wilaya nane za mkoa wa Tanga zitakazokuwa na thamani ya shilingi milioni 455.7 ambazo zitagawiwa wananchi kwa lengo la kukabiliana na changamoto ya uharibifu wa mazingira unaotokana na watu kutumia nishati ya mkaa.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa uuzwaji mitungi ya gesi ya LPG ya uzito wa kilo sita kwa bei ya ruzuku katika mkoa wa Tanga Mkurugenzi wa Teklonojia za Nishati Jadidifu na Mbadala, wa REA Mhandisi Advera Mwijage katika hafla fupi ya kumkabidhi mradi huo Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt. Batilda Burian, alisema kila wilaya za mkoa huo utapatiwa mitungi 3,255.

Alisema mitungi hiyo ambayo wananchi watalazimika kununua kwa kiasi cha sh, 17,500 na serikali itaongeza sh. 17,500 na msambazi katika mkoa wa Tanga itakuwa kampuni ya Manjis ambao wataisambaza kwa wakala watakaowachagua hasa katika maeneo ya vijijini.

Alisema Tanzania ina uwezo wa kuhakikisha upatikanaji wa nisahati safi, bora na rafiki wa mazingira katika maeneo ya vijijini, lakini pia idadi kubwa ya watu wanatumia mazao yanayotokana na misitu kupikia hivyo kuleta uharibifu mkubwa wa mazingira.

Mhandisi Mwijage alisema utafiti uliofanywa mwaka 2016 unakadiriwa kuwa watu 33,024 hufariki dunia kabla ya wakati kila mwaka ambayo ni sawa na asilimia 8.49 ya vifo vyote nchini kutokana na magonjwa ambayo yanachangiwa na uchafuzi wa hewa ndani ya nyumba wakati wa upikaji kwa kutumia nishati isiyo safi na salama.

“Hivyo serikali kupitia wakala wa nishati vijiji REA umetenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ikiwemo gesi LPG katika maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji kupitia mradi wa ufadhili unaotegemea matokeo (RBF) lengo ni kukukuza, kuchochea, kuwezesha na kuboresdha upatikanaji wa nishati safi na salama.

Mhandisi Mwijage alisema utekelezaji wa mradi huo unaenda sambamba na malengo ya makakati wa Kitaifa wa matumizi ya nishati safi ya kupikia ya mwaka 2024-2034 uliozinduliwa Mei 2024 na Rais Dkt Samia Sukuhu Hassan  ambao unalenga kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia kufikia asilimia 80 ya Watanzania wote wanaotumia nishati hiyo ifikapo mwaka 2034.

Akipokea mradi huo Mkuu wa mkoa wa Tanga, Balozi Burian wa unaendelea kumpongeza Rais Dkt Samia kwa kuendelea kuwa kinara wa maono baada ya kuzindua mpango huo ambao utasaidia wananchi kutunza mazingira kwa ajili ya nchi. 

Alisema mkoa huo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wametoa elimu kwa wananchi ili waweze kuachana na matumizi ya nishati za kuni na mkaa badala yake waweze kutumia nishati safi na salama na wameweka mpango kuhakikisha ziara ya rais hivi karibuni mkoani hapa watagawa mitungi hiyo kuendelea kuwahamasisha wananchi matumizi ya nishati hiyo.

Hata hivyo, Mkuu wa mkoa huyo alitoa rai kwa REA kuhakikisha wanatoa elimu kwa vijana ili waweze kutengeneza majiko makubwa ya gesi ambayo yatatumika na wananchi hasa mamantilie ambao mitungi ya gesi inayosambazwa haiwezi kukidhi mahitaji yao ya kupika chakula na mboga.

“REA kaeni na taasisi hizi,  vijana wetu hawana ajira wabuni na watengeneze majiko yatakayowasaidia mamantilie kuweza kupika chakula na mboga kwa wakati mmoja, lakini pia hakikisheni mnatengeneza mitungi ya gesi ya lita tatu ili wananchi wetu vijijini waweze kumudu kununua,” alisema Balozi Burian.



Share:

Tuesday, 17 December 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO DESEMBA 18, 2024

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger