Wednesday, 31 August 2022

BENKI YA NBC, KOLA PRODUCTS WATOA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA VIJANA WA DON BOSCO

Na Mwandishi Wetu - Malunde 1 blog

Benki ya Taifa ya Biashara ya NBC kwa kushirikiana na Kola Products wametoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana wa Wasalesia wa Don Bosco wanaotoka mikoa saba ya Tanzania.

Elimu hiyo imetolewa leo Jumanne Agosti 30,2022 wakati wa Kongamano la Vijana wa Wasalesia wa Don Bosco (Salesian Youth Movement - SYM) lililofanyika katika shule ya Don Bosco Didia mkoani Shinyanga ambalo limehudhuriwa na vijana Wanaotoka mikoa ya Shinyanga, Dodoma, Arusha , Kilimanjaro, Morogoro, Dar es Salaam na Iringa pamoja na wawakilishi kutoka Kenya ambako nyumba za Don Bosco zinapatikana.

Meneja wa Benki ya NBC tawi la Shinyanga Joyce Chagonja amewaomba vijana hao kuchangamkia fursa ya mikopo yenye gharama nafuu kutoka kwenye benki yao ili kuweza kujikwamua kiuchumi na kuingiizia mapato serikali.


Naye Meneja Biashara wa Benki ya NBC Fedrick Rutta amewasihi vijana hao kuhakikisha wanakwenda kufanya kwa vitendo mafunzo ya ujasiriamali waliyopewa ili kuweza kujipatia kipato na hatimaye kuweza kuajiri watu wengine ili kutatua changamoto ya ajira.

Akifundisha kwa vitendo juu ya utengenezaji wa sabuni za maji, Mkurugenzi wa Kola Products , Josephine Charles amewasihi vijana hao wachangamkie fursa ya utengenezaji sabuni kwa sababu ni rahisi kuitengeneza, mtaji ni mdogo naa soko ni rahisi kupatikana.

Mkuu wa shule ya Sekondari Don Bosco Didia Fr. Felix Wagi ameishukuru Benki ya NBC na Kola Products kwa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana hao.


Aidha amesema kongamano hilo hufanyika kila baada ya Miaka 2 kwa lengo la kuwaleta vijana hao wa madhehebu mbalimbali ya kikristo pia waislamu kuweza kujifunza mambo yanayohusu Maisha, wito, uchumi na hali ya Utandawazi.


"Kongamano hili ambalo mara zote hufanyika kwa siku tano, huratibiwa na kufadhiliwa na shirika la Don Bosco wakisaidiana na wadau mbalimbali pia michango ya ushiriki kutoka kwa vijana.Mwaka huu kongamano hili limefanyika mkoa wa Shinyanga katika shule ya Don Bosco Didia na kuhudhuriwa na Vijana 285 na walezi wao", amesema Fr. Wagi.
Meneja wa Benki ya NBC tawi la Shinyanga Joyce Chagonja akizungumza wakati wa Kongamano la Vijana wa Wasalesia wa Don Bosco (Salesian Youth Movement - SYM) lililofanyika katika shule ya Don Bosco Didia mkoani Shinyanga. Wa kwanza kushoto ni Afisa Mauzo wa Benki ya NBC Patrick Mashenene akifuatiwa na Meneja Biashara wa Benki ya NBC Fedrick Rutta
Meneja wa Benki ya NBC tawi la Shinyanga Joyce Chagonja akizungumza wakati wa Kongamano la Vijana wa Wasalesia wa Don Bosco (Salesian Youth Movement - SYM) lililofanyika katika shule ya Don Bosco Didia mkoani Shinyanga.
Meneja Biashara wa Benki ya NBC Fedrick Rutta akizungumza wakati wa Kongamano la Vijana wa Wasalesia wa Don Bosco (Salesian Youth Movement - SYM) lililofanyika katika shule ya Don Bosco Didia mkoani Shinyanga.
Mkurugenzi wa Kola Products , Josephine Charles akizungumza wakati wa Kongamano la Vijana wa Wasalesia wa Don Bosco (Salesian Youth Movement - SYM) lililofanyika katika shule ya Don Bosco Didia mkoani Shinyanga.
Mkuu wa shule ya Sekondari Don Bosco Didia Fr. Felix Wagi akizungumza wakati wa Kongamano la Vijana wa Wasalesia wa Don Bosco (Salesian Youth Movement - SYM) lililofanyika katika shule ya Don Bosco Didia mkoani Shinyanga 
Kongamano la Vijana wa Wasalesia wa Don Bosco (Salesian Youth Movement - SYM) likiendelea

Kongamano la Vijana wa Wasalesia wa Don Bosco (Salesian Youth Movement - SYM) likiendelea

Mkurugenzi wa Kola Products , Josephine Charles (kulia) akifundisha kwa vitendo juu ya utengenezaji wa sabuni za maji. 
Mkurugenzi wa Kola Products , Josephine Charles (kulia) akifundisha kwa vitendo juu ya utengenezaji wa sabuni za maji.
Mkurugenzi wa Kola Products , Josephine Charles (kulia) akifundisha kwa vitendo juu ya utengenezaji wa sabuni za maji.
Vijana wakitengeneza sabuni za maji.
Vijana wakitengeneza sabuni za maji.
Share:

KEMIKALI SUMU KATIKA TUMBAKU HUSABABISHA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA : ADAM FIMBO

 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Adam Fimbo akionesha orodha ya Kemikali sumu zinazopatikana katika Bidhaa za Tumbaku alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika maonesho ya Kimataifa ya wadau wa bidhaa za afya ya Afrika Mashariki katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Afrya Naibu Waziri wa Afya Dr.Godwin Mollel (wa pili kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Adam Fimbo (wa kwanza kulia aliyevaa suti) alipokuwa akizungumzia juu ya Kemikali sumu zinazopatikana katika Bidhaa za Tumbaku wakati waziri huyo alipotembelea katika banda la Mamlaka hiyo kwenye maonesho ya Kimataifa ya wadau wa bidhaa za afya ya Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.

Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma,wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),Gaudensia Simwanza (kulia) akifurahia jambo na Baadhi ya wadau wa Sekta ya Dawa waliotembelea kwenye Banda la Mamlaka hiyo kweye maonesho ya Kimataifa ya wadau wa bidhaa za afya ya Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.

 Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Bw. Adam Fimbo amesema kuwa Mamlaka hiyo imefanya uwekezaji katika mitambo ya kisasa inayoweza kubaini  kemikali sumu zilizopo kwenye bidhaa za tumbaku kwa lengo la kulinda afya za wananchi wanaotumia Bidhaa hizo.

Ameyasema hayo kwenye mahojiano maalumu yaliyofanyika kwenye Banda la Taasisi hiyo katika  maonesho ya Kimataifa ya wadau wa bidhaa za afya ya Afrika Mashariki yaliyoanza leo agosti 30,2022Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa bidhaa za tumbaku zenye kemikali hizo zinaweza kusababisha magonjwa yasiyombukiza na kwamba  TMDA imeweka orodha ya Kemikali zinazopatikana kwenye bidhaa za hizo ikiwemo sigara kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi mbalimbali wanaotembelea maonesho hayo.

"kwa upande wetu sisi tunashiriki kwenye maonesho haya kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi wanaotembelea na hapa tumeleta orodha ya kemikali ambazo zipo kwenye bidhaa za tumbaku, Tunachokifanya sisi ni kupima bidhaa za tumbaku zikiwemo sigara ili kuhakikisha hizi kemikali haziwepo kwenye bidhaa hizo "

"Hii ni horodha ya Kemikali sumu ambazo zipo kwenye Bidhaa za Tumbaku, horodha hii ya Kemikali ndizo zinazosababisha madhara  kwa binadamu ukisikia magonjwa kama kansa ya koo, shinikizo la damu na magonjwa mengi yasiyoambukiza ambayo yanatokana na utumiaji wa tumbaku" Ameeleza Fimbo.

Ameongeza kuwa Mamlaka hiyo imefanya uwekezaji mkubwa  kwenye mitambo kwaajili ya kupima na kubaini uwepo wa kemikali hizo  kwenye bidhaa za tumbaku ili kuhakikisha kemikali hizo haziwepo kwenye bidhaa hizo.

"Tunataka hizi kemikali zisiwepo kwenye sigala kwa hiyo kazi yetu kubwa ni kuhakikisha kila sigara hazina hizi kemikali zilizopo hapa" ameongeza. 

Share:

Tuesday, 30 August 2022

GGML WATOA MAGODORO 50 KWA KITUO CHA WAZEE BUKUMBI

Afisa Mwandamizi wa Mahusiano ya Jamii kutoka GGML, Shunashu Musa (kulia) akimkabidhi magodoro 50 msimamizi wa Kituo cha Wazee Bukumbi, Jonas Tarimo. Anayetazama ni Afisa Mahusiano wa Jamii wa GGML, Fredrick Musa (wa kwanza kulia).
Sehemu ya wazee wa Kituo cha Wazee cha Bukumbi wakisubiri msaada wa GGML.

Na Mwandishi wetu - Mwanza

KATIKA kuunga mkono juhudi za Serikali kuwajali na kuboresha maisha ya wazee nchini, Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Dhahabu Geita (GGML) imetoa msaada wa magodoro 50 kwa Kituo cha Wazee Bukumbi kilichopo mkoani Mwanza.


Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada huo jana mkoani Mwanza, Ofisa Mwandamizi wa Mahusiano ya Jamii kutoka GGML, Shunashu Musa alieleza kuwa msaada huo unalenga kuboresha makazi bora na hali ya maisha ya wazee wanaoishi katika kituo hicho.


Aliongeza kuwa baadhi ya wafanyakazi wa GGML na wenzao wamekuwa wakisaidia kituo hicho kwa nyakati tofauti na kuchangia baadhi ya vifaa vya matumizi. Kipindi hiki menejimenti ya kampuni hiyo imeamua kusaidia kituo hicho kwa kuchangia uboreshaji wa vyumba vya kulala vya wazee hao.


“Tulipokea ombi la kufikiria kusaidia kituo hiki kwa njia mbalimbali. Tunafahamu kituo hicho kilianzishwa miaka mingi iliyopita hivyo baadhi ya miundombinu na vifaa vinahitaji maboresho ndiyo maana uongozi uliamua kuchangia magodoro 50.

"Kama sehemu ya AngloGold Ashanti, moja ya maadili ya biashara ya GGML ni kwamba jumuiya na jamii tunakofanyia kazi lazima ziwe na maisha bora. Tunatumaini magodoro haya yataboresha maisha ya wazee zaidi ya 50 wanaoishi hapa,” alisema.



Aidha, Msimamizi wa Kituo cha Wazee cha Bukumbi, Jonas Tarimo alishukuru GGML kwa msaada huo na kuongeza kuwa utasaidia kutoa huduma za malazi bora na salama kwa wazee wa kituo hicho.



“Hiki ndicho kituo pekee cha kuishi wazee kilichopo karibu na mikoa ya Geita na Mwanza. Tumebahatika kuungwa mkono na Mgodi wa Dhahabu wa Geita ndio maana tunaona wakazi wengi wanafurahia msaada huu,” alisema.


GGML imekuwa kinara wa uwekezaji katika jamii tangu ilipoanzishwa mwaka 2000, huku vipaumbele vikubwa vikiwa ni miradi ya afya, elimu, maji, barabara, miradi ya maendeleo na miradi mingine ya kijamii inayolenga kuboresha ustawi wa jamii inayowapokea.


Mapema mwaka huu, Kampuni ilitangazwa kuwa mshindi wa jumla wa makampuni yaliyofanya vyema katika sekta ya madini nchini Tanzania kwa mwaka wa 2020/2021 baada ya kushinda tuzo za uwajibikaji wa kampuni kwa jamii, mazingira, usalama, mlipakodi bora na maudhui ya ndani.

Share:

BENKI YA CRDB YAFUNGUA RASMI TAWI LAKE WILAYANI LUSHOTO , TANGA

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Omary Mgumba (katikati) kwa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Prof. Neema Mori (wapili kushoto), Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa (kushoto) wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa tawi la Benki ya CRDB lililopo wilayani Lushoto mkoani Tanga, jana Agosti 29, 2022. wengine pichani ni Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga, Suleiman Mzee (wa pili kulia), Mkuu wa wilaya ya Lushoto, Kalist Lazaro (kulia), pamoja na Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Lushoto, John Mtani.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Omary Mgumba (kulia) kwa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Prof. Neema Mori wakifungua kitambaa kwenye jiwe la msingi kuashiria ufunguzi rasmi wa tawi la Benki ya CRDB lililopo wilayani Lushoto mkoani Tanga, jana Agosti 29, 2022.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Omary Mgumba akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi rasmi tawi jipya la Benki ya CRDB lililopo wilayani Lushoto mkoani Tanga, jana Agosti 29, 2022.
Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi rasmi tawi jipya la Benki ya CRDB lililopo wilayani Lushoto mkoani Tanga, jana Agosti 29, 2022.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Omary Mgumba ameongoza sherehe za ufunguzi rasmi wa tawi jipya la Benki ya CRDB lililopo wilayani Lushoto na kuwataka wananchi wa Wilaya hiyo kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi zitolewazo na Benki hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mhe. Mgumba alisema "Wakazi wa Lushoto na vitogoji vyote vinavyozunguka wilaya hii, niwape rai ya kuitumia benki hii kama chachu ya maendeleo wilayani hapa, haswa katika kutumia huduma za kibenki lakini pia kujipatia mikopo mbalimbali iltolewayo na benki hii ya CRDB".

Aidha, Mgumba aliendelea kusema "Serikali kwa kushirikiana na wadau imedhamiria kuwawezesha wananchi kiuchumi ndio maana inasogeza huduma zikiwamo za kifedha jirani yenu. Kila mmoja aangalie fursa zilizopo kukuza uchumi wake," alisisitiza.

Kwa upande wa Afisa Mkuu wa Biashara Benki ya CRDB, Boma Raballa alisema, wakazi wa Lushoto na vitongoji vyake sasa wanayo fursa ya kulitumia tawi hilo ambalo kwa sasa limeondoa changamoto ya kufuata huduma za kibenki wilayani Korogwe, kwa kusogeza huduma kwa wananchi na leo tumefika Lushoto,

Naye Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Profesa Neema Mori alisema, wataendelea kushirikiana na Serikali kufanikisha shughuli mbalimbali za kiuchumi nchini hasa katika kuhakikisha wananchi wanapata fursa zitolewazo na benki ya CRDB ikiwemo mikopo nafuu ya kilimo ambayo kwasasa riba yake ni asilimia 9 tu. Hivyo aliwataka wanalushoto kuchangamkia fursa hiyo na kuhakikisha wanainua uchumi wa mtu mmoja mmoja lakini pia katika vikundi na kufanikisha miradi ya maendeleo.
Share:

HAYA NDIYO MADHARA YA KULA CHIPS


KIUKWELI katika vyakula vitamu duniani na vinavyopendwa haswaa na watu duniani usiposema chipsi utakuwa mtu waajabu sana. Chipsi haziliki bongo tu ata ughaibuni chips zinalika sana na zinapendwa haswaa, chipsi zinaenda na vitu vingi kama chipsi yai, chipsi kuku na kadhalika.

Hizi ndio athari za ulaji wa chipsi.

Husababisha magonjwa ya moyo

Kwa kuzingatia ukweli kwamba zimekaangwa sana katika mafuta ya hidrojeni, chipsi huja na kiasi kikubwa cha mafuta, ambayo huongeza cholesterol yako mbaya na kupunguza cholesterol yako nzuri. Athari kubwa ya hii ni kwamba utaongeza hatari ya ugonjwa wa moyo.

 Hupunguza kinga ya mwili

Kulingana na utafiti uliochapishwa katika jarida la Current Opinion in Clinical Nutrition & Metabolic Care, kula chakula chenye mafuta mengi na vyakula vya kukaanga vingi unaweza kuwa unaharibu utumbo wako kwa kuongeza bakteria wasio na afya na kupunguza bakteria wa afya ya mwili wako. Kwa kuzingatia jukumu la utumbo katika kusaidia kufahamisha mfumo wa kinga ya mwili wako, unaweza kuwa unaweka mwili wako hatarini kupata magonjwa.

Huongeza uzito wa mwili

Vyakula vya kukaangwa katika mafuta, huwa mabomu ya kalori, na kusababisha kupata uzito. Utafiti uliochapishwa katika jarida la The American Journal of Clinical Nutrition uligundua kuwa kula vyakula vya kukaanga kunahusishwa moja kwa moja na unene kupita kiasi.


Imeandikwa na Peter Nnally kwa msaada wa mitandao.
Share:

JAMAA WA MIAKA 46 AMBAKA MTOTO WA MIAKA 8 KISHA KUMPA SH. 500


Mtoto aliyebakwa

Mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina la Sunday (46), mkazi wa mtaa wa Mkudi, Kata ya Nyamanoro Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza, anadaiwa kumbaka mtoto wa 8 (Pichani) na kumsababishia maumivu makali ikiwemo kumharibu kisaikolojia.

Mtoto huyo akizungumzia tukio hilo amesema mwanaume huyo alimuita wakati akiwa anacheza na kumvutia ndani.

"Nilikuwa nacheza ndipo Sunday akaniita akanivuta ndani akaniambia naomba nikubake nikakataa, nilivyokataa nikataka kupiga kelele akaniziba mdomo akanitishia kisu, akanivua nguo akanibaka kisha akanipa shilingi mia tano akamaliza akafunga mlango akaondoka baada ya mama kujua nimebakwa akamuita bibi ndipo tukaenda polisi", ameeleza mtoto huyo

Wakizungumza kwa uchungu wazazi wa mtoto huyo wameviomba vyombo vya dola kuwasaidia kutokana na mtoto wao kuharibiwa na kuambulia kupata maumivu makali huku akitakiwa kutumia dawa mwezi mzima ili kumuepusha na maambukizi ya virusi vya Ukimwi lakini wanashangaa mtuhumiwa akiwa nje kwa dhamana licha ya kumfungulia kesi ya ubakaji na ushahidi kuwepo.

Share:

Monday, 29 August 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE AGOSTI 30,2022



Magazetini leo Jumanne August 30 2022





















































Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger