Monday, 8 July 2024

WADAU WA LISHE BUKOBA DC WAKUTANA KUJADILI NAMNA YA KUENDELEZA MAPAMBANO DHIDI YA UDUMAVU




Na Mariam Kagenda _Kagera

Wadau mbalimbali halmashauri ya Bukoba mkoani Kagera wamekutana pamoja kujadili jinsi ya kuongeza bidii katika suala la kupambana na changamoto ya udumavu na utapiamlo kwa wananchi.

Wadau hao kutoka maeneo tofauti tofauti wamekutana Julai 4, 2024 katika kikao kazi cha lishe kikilenga zaidi taathimini ya utekelezaji wa mradi walishe uliokuwa ukitekelezwa na Shirika la PANITA kilichofanyika Manispaa ya Bukoba ambapo katika majadiliano hayo suala la elimu ya lishe limebainika kuwa bado ni changamoto inayowakabili wananchi walio wengi.

Wamefafanua kuwa kutokana na jamii kuwa na uelewa mdogo juu ya ulaji wa vyakula mchanganyiko na vyenye virutubishi imepelekea baadhi ya wananchi kutokukubali kubadilika nakuendelea kutumia vyakula kwa mazoea ambapo wametoa mfano jamii inavyokula chakula aina ya ndizi kwa wingi bila ya mchangayiko wa chakula kingine.

Joseph matope ni kaimu afisa elimu awali na msingi wilaya amesema kuwa Bukoba na Kagera kwa ujumla vyakula vipo vya kutosha lakini matumizi yamekuwa ni hafifu mno.

"Vyakula wanavyo magimbi yapo, maharage yapo, mboga za majani zipo, mihogo na vingine vingi vipo lakini hawavichanganyi wakati wa ulaji, watoto wanawapa ndizi pekee kuanzia asubuhi, mchana na kuendelea, tubadilike wote ili kuyafikia malengo, amesema afisa Joseph Matope"

Afisa huyo pia ameeleza kuwa sekta ya elimu jitihada zimefanyika nakuhakikisha shule nyingi halmashauri hiyo zinatoa huduma ya uji na chakula kwa wanafunzi japo shule zinazotumia unga uliorutubishwa ni chache kutokana na mashine zinazosindika unga wa lishe kuwa chache maeneo ya Bukoba.

Jambo jingine lililoelezwa kuchochea udumavu nipamoja na baadhi ya wazazi kutokuwa tayari kupokea maelekezo muhimu kutoka kwa watalaamu wa afya juu ya utekelezaji wa lishe, maelezo ambayo yametolewa naye mwalimu Paschal Ngaiza.

"Tunapolisimamia suala hili la lishe tujitowe ufahamu wazazi hawa wengine ni wakorofi wamekuwa wagumu hata kuchangia chakula cha watoto shuleni, hii lishe imekuwa pasua kichwa kwa hiyo tunatakiwa wote kujikakamua na kujipanga vilivyo kuibadilisha jamii yetu hii" mwalimu Paskal akisisitiza.

Hata hivyo kwa upande wao PANITA ambao ni mwavuli wa mashirika ya kijamii yanayoshughulika na masuala ya afya na lishe kwa kushirikiana na Gain pamoja na Sanku wanaotekeleza mradi wa urutubishaji chakula shuleni .

Kupitia Afisa mradi Lubango Charles wamezitaja shughuli za miradi ya lishe zilizoteketezwa kwa Bukoba DC ikiwemo ya kukutana na viongozi wa halmashauri na wadau wa lishe, kukutana na viongozi wa kata hasa kata ya Kemondo, kuhamasisha uanzishwaji wa bustani za mbogamboga shuleni, wamezifikia shule tano.

Nyingine ni kuwajengea uwezo watalaamu wa afya ngazi ya jamii, kuelimisha jamii matumizi ya vyakula vilivyorutubishwa, usimamizi shirikishi katika utekelezaji wa maazimio ya mradi na nyinginezo.

Akihitimisha taarifa Afisa Lubango amesema mradi huo kwa sasa umefika kikomo, hivyo ametoa wito akiwasihi wadau wote kupitia nyadhifa zao kujimudu na kuibeba kwa dhati dhana nzima ya lishe kwa kuifuatilia jamii ili kuona kama yanayoelimishwa yanatekezwa kwa ufanisi.

Kaimu afisa lishe wilaya Donald Kalenzo amebainisha na kusema kuwa lishe bora ni jambo ambalo limekuwa likipambaniwa zaidi katika halmashauri ya Bukoba ili kuhakikisha udumavu na utapiamlo unapungua kwa kiwango kikubwa na jamii ibakie kuwa salama kama yalivyo makusudi ya serikali.

Amewahimiza wadau wote kuungana pamoja kuupiga vita udumavu ili kuwalinda watu wote nakuwa na jamii yenye lishe bora kuanzia wanawake wajawazito na watoto.

Joanitha Jovin ni afisa lishe mkoa akipongeza juhudi za PANITA kwa kazi kubwa waliyoifanya Kagera amewakumbusha wadau kuwa udumavu ni adui ambaye anapaswa kutokomezwa ili kuinua afya ya jamii kwani Kagera ni mkoa wenye neema ya vyakula hivyo haina sababu ya kuwa katika hali ya udumavu kama ilivyo kwa sasa.

Licha ya pongezi na shukrani ametoa ombi kwa shirika hilo kurejea tena Kagera kwa miradi mingine ya lishe ili kuzifikia wilaya zote za mkoa kwani awamu hii ilizihusisha halmashauri tatu za Bukoba DC, Manispaa ya Bukoba na Muleba.
Share:

BENKI YA CRDB YATUMIA MAADHIMISHO YA SIKU YA USHIRIKA DUNIANI 'SUD' KUONESHA FURSA ZA UWEKEZAJI


Benki ya CRDB imeshiriki maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani (SUD) duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Tabora katika Viwanja vya Ipuli.

Maadhimisho hayo yaliyoanza tarehe 29 Juni 2024 na kuhitimishwa leo tarehe 6 Julai,2024 yalifunguliwa na Naibu Waziri wa Kilimo Mh. David Silinde na kufungwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko.

Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Abdulmajid Nsekela aliungana na wafanyakazi wa Benki ya CRDB kutoka Makao Makuu wakiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Kilimo Biashara, Maregesi Shaaban, pamoja na wafanyakazi wa Kanda ya Magharibi wakiongozwa na Meneja wa Kanda hiyo, Jumanne Wagana.

Benki ya CRDB ikiwa ni mdau mkubwa wa sekta ya ushirika nchini, Benki ambayo pia ndio mdhamini mkuu  imetumia maadhimisho hayo kuonesha fursa za uwezeshaji zinazotolewa kwa wateja wake waliopo kwenye mnyororo wa thamani katika sekta za kilimo, uvuvi, ufugaji, viwanda na usafirishaji.

#CRDBBank
#UlipoTupo




Share:

WAZIRI JAFO : KAMILISHENI JENGO LA VIWANDA NA BIASHARA KWA WAKATI


WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo akikagua ujenzi wa jengo la Wizara hiyo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma 

Na Mwandishi Wetu_DODOMA

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo amekagua ujenzi wa jengo la Wizara hiyo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma na kuwataka wakandarasi kuhakikisha unakamilika kwa wakati.

Akizungumza Julai 8, 2024 baada ya kukagua ujenzi huo, Waziri Jafo ameridhishwa na kazi inayoendelea na matarajio ifikapo Septemba 30, 2024 ujenzi uwe umekamilika.

"Niwatake wasimamizi wa ujenzi huu ambayo ni Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) wasimamie vizuri pamoja na mkandarasi kuhakikisha kazi unakamilika ndani ya muda uliopangwa, imani yetu itakapofika Septemba 30, 2024 sisi watumishi tuweze kuhamia kwenye jengo hili."

"Nimefarijika na mapokezi katika Wizara hii, jambo kubwa ambalo tumejiwekea malengo ni kuhakikisha mchakato wa majengo unakamilika katika hii awamu ya pili na watumishi wote wanahamia,"amesema.

Aidha amewataka watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa bidii na ushirikiano.

"Ili tuweze kufikia Malengo ya Wizara yetu lazima tufanye kazi kwa bidii na Ushirikiano Ili tuendelee kumsaidia Rais wetu Mhe Dk.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania", amesisitiza
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo,akikagua ujenzi wa jengo la Wizara hiyo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo,akitoa Maelezo mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo la Wizara hiyo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Share:

Wimbo Mpya : JABHUKI - NANGONGOLE


Huu hapa wimbo mpya wa Msanii Charlz Ndela ' Jabhuki' unaitwa Nangongole

Share:

Sunday, 7 July 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU JULAI 8, 2024

Share:

WAZIRI MAKAMBA AONGOZA KIKAO CHA MAWAZIRI 15 WA EAC


WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb) ameongoza Mkutano wa faragha wa Mawaziri wa Mambo ya Nje na Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Afrika Mashariki katika Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika Zanzibar.

Akizungumza katika Mkutano huo wa siku tatu ambao yeye ni mwenyekiti, Mhe. Makamba amesema Tanzania imejidhatiti kuhakikisha Jumuiya ya Afrika Mashariki inakuwa imara, yenye umoja na inayofikia malengo yake.

“Madhumuni ya mkutano huu ni kuifanya familia yetu kuwa imara, kuifanya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutekeleza majukumu yake vizuri, Tanzania kama moja ya waanzilishi wa Jumuiya hii tumejidhatiti kuona jumuiya ikiwa na umoja, imara na yenye kufanikiwa” alisema Mhe. Makamba

Naye Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Musalia Mudavadi ameipongeza Tanzania kwa kukubali kuwa mwenyeji wa mkutano huo na kuongeza kuwa ni wakati muafaka kwa nchi wanachama kuhakikisha wanatumia fursa mbalimbali ndani ya jumuiya kwa manufaa ya wananchi.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Rebecca Kadaga ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuwa mwenyeji wa mkutano huo na kupongeza juhudi za kuimarisha jumuiya.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri Mhe. Deng Alor Kuol amesema kufanyika kwa mkutano huo ni jambo jema hasa ikizingatiwa kuwa utaangalia masuala ya amani, usalama na mtangamano wa jumuiya ikiwa ni hatua za kuifanya jumuiya kusonga mbele.

Mkutano huo wa faragha unajadili taarifa ya Mwenyekiti wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya; hali ya amani, usalama, siasa na uhusiano kati ya nchi wanachama; kutathmini na kujadili mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na masuala yanayokwamisha ufikiwaji wa malengo ya programu na miradi inayopangwa.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger