Monday, 8 April 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE APRILI 9, 2024

Share:

Video Mpya : NELEMI MBASANDO - SHULE


Hii hapa ngoma mpya ya The Big Trump 'Nelemi Mbasando' inaitwa Shule
Share:

JINSI NILIVYOSHINDA KESI YA UBAKAJI AMBAYO NILISINGIZIWA!

 


Jina langu Abduli kutokea Kigoma, Tanzania, mimi ni yatima, sasa nakumbuka nikiwa na miaka kama 20 hivi, alitokea mama mmoja mzungu ambaye alikuwa na taasisi ya kusaidia watoto na vijana wenye uhitaji.

Kumbe yule mama wa kizungu, alikua anatumia ile taasisi kuwatapeli wazungu wenzie, wanafadhili kituo kwa ajili ya kuhudumia watoto wenye uhitaji, yeye anaweka pesa mfukoni na kufanyia mambo yake.

Basi akatokea mfadhili mmoja ambaye alikuwa na nia ya dhati ya kunifadhili masomo na mahitaji yote, lakini kila nikifuatilia lile suala, yule mama mzungu ananizungusha.

Kumbe pesa ameshakula, kwa kua nilikua na kiu ya kutoboa basi nikawa nafanya jitihada nyingi sana kuufuatilia ule ufadhili, kumbe namuudhi.

Basi ikawa vita kubwa hadi ikafikia mahali nikasingiziwa nimembaka binti ambaye tulikua naye mle ndani kituoni, ile kesi ilinisotesha sana kwenye mikono ya sheria, yaani mahakama.

Siku moja nikiwa kwenye mitandao ya kijamii niliona tangazo la Kiwanga Doctors kuwa anaweza kusaidia watu kushinda kesi ambazo wamesingiziwa katika mahakama.

Basi nilichukua namba yake ambayo ni +254 769 404965 na kuwasiliana naye, nilimueleza kila ambalo nimekumbana nalo.

Aliweza kunifanyia ganga ganga zake za tiba asili na kunipa hakikisho kuwa naenda kushinda kesi hiyo, hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi.

Siku ya hukumu ilifika nami nikajongea hadi mbele ya mahakama, nashukuru Jaji alisema mimi sina hatia yoyote, hivyo nikaachiwa huru.

Kwa sasa naendelea na maisha yangu ila yule mama kamwe hawezi kusahau jinsi nilipambana naye hadi kuja kumshinda mahakamani na sasa amefunga kituo chake.

Siku zote kumbuka Kiwanga Doctors anatoa huduma kama kusafisha nyota, kusuluhisha migororo ya ndoa, mahusiano, mapenzi na familia, kumfunga mume au mke asitoke nje ya ndoa, anatoa tiba kwa wanaotafuta watoto.

Vilevile anatoa huduma ya kukusaidia kupata kazi au ajira, kupandishwa cheo na mshahara kazini, kuwasaidia wenye urahibu wa dawa za kulevya, sigara na pombe, kwa wanaotafuta mume au mke pia anawasaidia tena ndani ya siku chache.

Anatibu magonjwa kama kisukari, msukumo wa damu (BP), upungufu wa nguvu za kiume, miguu kuwaka moto n.k, pia anaweza kuisadia biashara yako kunawiri, na huduma zote hizi unaweza kuzipata bila kufika ofisini kwake.

Basi chukua hatua ya kuwasiliana na Kiwanga Doctors kwa namba; +254 769 404965.

Mwisho.

 


Share:

MBUNGE MTATURU ALIA NA UJENZI MADARAJA SINGIDA MASHARIKI


SERIKALI inatambua umuhimu wa vivuko na madaraja katika Jimbo la Singida Mashariki ambapo kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini imeweka katika mpango wake kwa mwaka wa fedha 2024/2025, jumla ya Shilingi Bilioni 1.11 kwa ajili ujenzi wa madaraja katika Wilaya ya Ikungi.

Naibu Waziri,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI),Zainab Katimba amesema hayo Aprili 8,2024,Bungeni Jijini Dodoma,wakati akijibu swali la Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu.

Katika swali lake Mtaturu ametaka kujua ni lini serikali itajenga Maradaja kwenye Barabara za Misughaa-Kikio na Matongo - Mpetu - Singida.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri Katimba amesema katika mwaka wa fedha 2023/2024,jumla ya Shilingi Milioni 435 zimetumika katika ujenzi wa madaraja katika barabara ya Mpetu-Matongo, Misughaa-Msule-Sambaru, Mungaa-Ntuntu-Mang’onyi na Lighwa-Ujaire na utekelezaji wake umefikia asilimia 90.

Amesema katika barabara za Misughaa-Kikio na Matongo-Mpetu kuna uhitaji wa jumla ya madaraja matatu ambayo ni Daraja la Mto Matongo lenye urefu wa mita 65, Daraja la mto Isanja lenye urefu wa mita 45, na Daraja la mto Siuyu lenye urefu wa mita 30.

Aidha,kutokana na ukubwa wa madaraja hayo usanifu wa kina unahitajika kufanywa ambapo TARURA imeanza kutekeleza kazi ya usanifu wa Madaraja haya kwa lengo la kupata gharama halisi za ujenzi wake.

Katika swali la nyongeza Mbunge wa Viti Maalum Martha Gwau akiuliza kwa niaba ya Mtaturu ametaka kujua kwa kuwa Bajeti ya TARURA wilayani ni ndogo,je nini mpango wa serikali kujenga madaraja ili kukamilisha kazi nzuri inayofanyika kuunganisha barabara za vijiji na vijiji,kata na kata na hatimaye Wilaya na wilaya?

" Pia kwakuwa barabara bila madaraja haikamilki na kwakuwa tathimini ya madaraja barabara ya matongo-mpetu,Misughaa-Ntuntu,Misughaa-Kikio,Kimbwi na Ighuka imeshafanyika ni lini serikali itatenga fedha kujenga madaraja hayo?,amehoji Mbunge Gwau kwa niaba ya Mtaturu.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri Katimba amesema serikali ina mpango wa kuhakikisha kwamba inajenga na kuboresha miundombinu maeneo yote nchini.

Amesema mtandao wa barabara nchini una kilomita 144.429 na ni mtandao mkubwa hivyo unahitaji bajeti kubwa.

"Mh Mbunge Mtaturu tumekuwa tukiwasiliana mara kwa mara na amenieleza changamoto za miundombinu katika jimbo lake,Mh Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akichukua jitihada mbalimbali ikiwemo kuongeza bajeti ya TARURA kutoka Bilioni 275 hadi Bilioni 710 mpaka sasa,"amesema Katimba.

Amemuhakikishia mbunge kuwa pale inapotokea dharura serikali inapeleka fedha kwa ajili ya kuhakikisha mawasiliano hayakatiki na kusisisitiza dhamira ya serikali ya kufanyia kazi ujenzi wa madaraja na miundombinu yote ambayo ni muhimu kwa ajili ya wananchi.

"Niwahakikishie kuwa bajeti ya dharura imeongezwa kutoka Bilioni 21.2 hadi Bilioni 52.6,yote hii kwa sababu serikali inataka pale inapotokea dharura waweze kutatua dharura hiyo,"amesema.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRILI 8 , 2024

Magazeti
Share:

Sunday, 7 April 2024

MARIAM ULEGA AKABIDHI SIMU KUFANIKISHA USAJILI WANACHAMA KIELETRONIKI MKOANI PWANI



MJUMBE wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT)Taifa na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa jumuiya hiyo Marima Ulega amekabidhi simu za mkononi tisa kwa ajili ya kufanikisha usajili wanachama kieletroniki ndani ya Mkoa wa Pwani.

Akizungumza na wana UWT Mkoa wa Pwani wakati wa hafla ya kukabidhi simu hizo Mariam Ulega amesema kwa sasa wanaona na wanaendelea kujivunia matunda ya uongozi wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan na hakika amekuwa mwananmke shupavu na mwenye mapenzi makubwa na wanawake wa Tanzania hasa UWT.
Amesema siku za hivi karibuni walipatiwa semina na viongozi wa UWT Taifa wakiongozwa na Mwnyekiti wao Mary Chatanda na katika semina hiyo walieleza masuala mbalimbali hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji na kubwa zaidi wamehimizwa kufanya kazi.

“Sisi wana UWT tufanye kazi na tupite kwa wananchi tukielezea mazuri yaliyofanywa na Rais.Hatuwezi kufanikiwa kama hatuna ongezeko la wana chama hivyo tunatakiwa tuwavute wanachama wapya , tusajili wanachama wapya kieletroniki na hiyo itatusaidia.
“Tunafahamu wapo akina mama wenzetu wanaojishughulisha na mama lishe, wajasiriamali na wapo waliopo katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo.Hivyo sisi kama jeshi la mama Samia tunatakiwa tutoke kuhakikisha tunavuna wanachama wengi,”amesema.

Amefafanua kuna mtandao wa UWT ambao umeanzishwa unaosajili wanachama keletroniki na Mkoa wa Pwani kuna wilaya moja ndjo inaonekana inasajili wanachama.Hata hivyo kunachangamoto ya vitendea kazi.
“Hivyo nimeamua na nimedhamiria kwa dhati kusaidia jumuiya hii, hivyo nimeamua kuleta simu kwa ajili ya kufankisha usajili wa kieletroniki katika mkoa wetu ili taarifa za usajili zinapotunwa na mkoa wetu uwepo .

“Makatibu wa UWT naaawamini hivyo tuhakikishe tunahamasisha wanachama wapya kwa kuwasijili sambamba na kuwaelezea UWT ni nini na inafanya kazi zipi na iwapo watajiunga nayo watapata faida zipi.


“Mwenyekiti wetu wa UWT Taifa tunamuona anahimiza usajili, tukiwa na wanachama wengi tutasonga mbele hivyo simu janja ninazokabidhi zinakwenda kurahisisha shughuli za usajili.”
Mariam Ulega amesema anatambua mkoa wa Pwani una wilaya nane lakini amegawa simu tisa kwani moja itakuwa simu ya mkoa ambayo itatumika kwa shughuli za usajili wa wanachama kama ambavyo itakuwa ikifanyika wilayani.“Hivyo twendeni tukaongeze wanachama kwa kasi ya 4G.”

Share:

WAKENYA WAIKUBALI NGURUWE PROJECT KATIKA KIJIJI CHA NGURUWE DODOMA

DODOMA;  Idadi ya wawekezaji wa Kigeni wenye dhamira ya kufanya uwekezaji katika kijiji cha Nguruwe imezidi kuongezeka katika kijiji cha Mayamaya wilayani Bahi Mkoani Dodoma baada ya wafugaji kutoka nchini Kenya wakiongozwa na Paulo Kimanya kufika kitongoji cha Zamahero kujifunza juu ya ufugaji wa kisasa wa Nguruwe na kisha kuonyesha nia ya kuwekeza katika mradi huo uliyochipuka kwa kasi miezi michache iliyopita.

Wakizungumza mara baada ya kufanya ukaguzi na kisha kuridhishwa na mazingira ya utekelezaji wa Nguruwe Project wenye nguruwe zaidi ya 800 wawekezaji kutoka nchini Kenya akiwemo Kimanyi wamesema wana kila sababu ya kuwekeza katika kijiji cha Nguruwe kwasababu ufugaji wake umezingatia sheria za mazingira na haki za wanyama hivyo wana amini watakwenda kunufaika na kitakachowekezwa.

"Sisi tumekuja hapa kijiji cha Nguruwe kwasababu tumeona taarifa za mradi huu na kwakuwa ulaji wa nyama ya nguruwe unazidi kushika kasi na mikataba haina shida kwa wawekezaji hivyo tunakwenda kuandaa fungu ili kuja kufanya uwekezaji",alisema Paul Kimanyi.

Awali mwanzilishi wa Kijiji cha Nguruwe katika kitongoji cha Namahero ambaye pia ni mkurugenzi wa Kijiji cha Nguruwe Project Simon Mkondya amesema wazo la kuanzisha mradi huo lilikuja baada ya kuona uhitaji wa kitoweo hicho unaongezeka na kwamba hadi sasa kuna nguruwe zaidi ya 800 wakubwa na wadogo waliozaliwa siku chache zilizopita.

Mkondya amesema shauku yake kubwa ni kuona kijiji hicho kinakuja kuwa kusanyiko kubwa la Nguruwe dunia na kuchangia pato kubwa la taifa kupitia mauzo ya mifugo na tozo ya utalii ambapo mtalii wa ndani atapaswa kulipa dola moja na mtalii wa nje kulipa dola 10 kutembelea na kisha kujionea maajabu ya kijiji hicho hivyo kila uchwao wawekezaji wanaongezeka na kutengeneza fedha .

Hadi sasa kijiji cha Nguruwe kimepokea watalii zaidi ya 1400 wa ndani na nje ya nchi ikiwemo Venezuela,Colombia,China,Ufaransa,Kenya na mataifa mengine mengi ambao wamekuwa chachu kubwa ya kuinua uchumi wa kijiji cha Mayamaya kupitia biashara ndogondogo zinazofanyika hapo.

"Tumetengeza mfumo wa Rent to Own ambao mtu anawekeza fedha yake,kwa mfano laki saba anapata faida mara tatu katika kipindi cha miezi sita na muwekezaji atakuwa analipwa kila siku hadi miezi sita kuisha",alisema Mkondya.

Akieleza aina za nguruwe wanaofugwa katika kijiji hicho Muwekezaji huyo amesema ni aina tatu akiwemo Large White mwenye mafuta Mengi ambae hunenepa sana na hupendwa sana akina dada, Duroc ambaye tabia yake ni kuwa na nyama nyingi na mafuta machache pamoja na Landrace.

Ukiachana na wakenya ,kijiji cha Nguruwe kimetembelewa pia na viongozi wa serikali za vijiji vya karibu na mradi huo akiwemo Joseph Mchami mwenyekiti wa mtaa wa Sekondari kata ya Makutupora ambaye anasema amelazimika kufika ili kujionea uwekezaji uliofanyika na kisha kumuomba muwekezaji kuona namna ya kwenda kuwekeza pia katika mtaa wao.

Wengine ni Fadhili Hawadhi Juma na Mohamed Choku maarufu Muarabu ambao baada ya kukagua mazingira ya mradi wameonyesha kuridhishwa na utekelezaji wake huku pia wakisema faida kubwa ipo kwenye kutengeneza ajira za vijana na kuinua uchumi wa kijiji cha Namahero.

Katika hatua nyingine Mradi huo umetembelewa na watumishi wa umma akiwemo Atupele Mwakalinga ambae anasema wamejifunza hatua zote za ufugaji wa nguruwe,changamoto za ufugaji na Mazingira ya Mradi na kisha kuondoka na imani kubwa ya kuja kuwekeza katika kijiji cha Nguruwe.

"Tumekuja hapa kujifunza kila kitu kuhusu nguruwe hivyo wanaondoka wakiwa hawana shaka yoyote ya kuja kuwekeza hivyo wanakwenda kujipanga na kurudi Namahero" ,alisema Mwakalinga.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger