Monday, 25 September 2023

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI APONGEZA UBORESHWAJI WA MIUNDOMBINU YA BANDARI UNAOFANYWA NA MAMLAKA YA BANDARI NCHINI-TPA

 


Na Mwandishi wetu Pwani

Naibu Waziri wa uchukuzi Mhe David Kihenzile amepongeza jitihada mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini(TPA) za uboreshwaji wa miundombinu ya Bandari za bahari na maziwa.


Mhe Kihenzile ameyasema hayo wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua bandari ndogo ya bagamoyo, eneo la Mbegani itakapojengwa bandari mpya ya bagamoyo na bandari kavu ya kwala vyote vilivyoko Mkoa wa Pwani tarehe 25 Septemba,2023.



“Nimepata fursa ya kutembelea bandari ndogo ya bagamoyo, kukagua eneo la mbegani itakapojengwa bandari mpya ya Bagamoyo na bandari ya kwala uwekezaji uliofanyika tayari na unaotarajia kufanyika ni mkubwa na utaongeza mapato ya TPA,wananchi , pato la taifa na utasaidia kukuza utalii ikiwa ni jitihada za kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuifungua nchi kimataifa” amesema kihenzile


Mhe Kihenzile amesema ujenzi wa Bandari mpya ya Bagamoyo yenye eneo la ukubwa wa Hekta 887 unaotarajiwa kuwa na gati 24 ambapo kwa kuanzia imeshatangazwa tenda ya kumpata mkandarasi kwa ujenzi wa Gati tatu zenye urefu wa mita mia tatu kila moja ni miongoni mwa miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita ikiwemo ujenzi wa SGR,ununuzi wa ndege, vichwa vya treni na mabehewa ili kutanua wigo wa kuhudumia mizigo ya ndani na ya nchi jirani zinazotuzunguka ambazo zina mzigo mwingi zaidi.



“Nchi jirani zinazotuzunguka mahitaji yake ya mzigo kwa mwaka ni metric tani mil 40 na uwezo wa bandari zetu kwa sasa ni kuhudumia metric tani mil 8, hivyo ujenzi wa bandari hii utakapokamilika sambamba na maboresho ya bandari zetu zote za bahari, maziwa na bandari kavu za kwala,katosho,ferana ihumwa tutakuwa na uwezo wa kuhudumia mzigo wa metric tani mil 50 kufikia mwaka 2030 hivyo kulihudumia vyema soko la kimataifa” amesisitiza Kihenzile


Akitoa maelezo ya mradi Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Nchini Mha Juma Kijavara amesesma eneo la mbegani inapotarajiwa kujengwa bandari mpya ya Bagamoyo lina ukubwa wa hekali 887 na zoezi linaloendelea sasa ni ukamilishaji wa ulipaji wa fidia na kuwahamisha wananchi ili kupisha mradi na tayari tenda imeshatangazwa ya kumpata mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa gati tatu zenye mita mia tatu kila moja.



“zoezi linaloendelea sasa ni ulipaji wa fidia ambapo mpaka sasa shilingi Bil 49 zimeshalipwa kati ya bil 57 zilizofanyiwa tathmini na tenda imeshatangazwa ili kumpata mkandarasi kwa ujenzi wa gati tatu z mita mia tatu na tunaendelea kupokea maombi” amesisitiza Mha Kijavara


Kuhusu uwekezaji bandari kavu, Mha Kijavara amesema uendelezaji wa bandari kavu nchini ni mkakati wa kurahisisha upakiaji na upakuaji wa mizigo bandarini ili kuondoa msongamano na kuongeza ufanisi na kuhudumia mizigo zaidi kwa kuliona hili mamlaka ya Bandai nchini ilianzisha bandari kavu ya kwala yenye hekta 502 ambapo na Nchi jirani zimepewa maeneo, bandari kavu ya Katosho,Fera,Isaka,Iihumwa,Korogwe na Tunduma maongezi yanaendelea ya kupata hekta 500 na maeneo mengine upembuzi unaendelea.


Awali akimkaribisha Naibu Waziri wa Uchukuzi Mkoa wa Pwani,Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Bw. Shauri Selenda ameishukuru Wizara ya Uchukuzi na Serikali ya awamu ya sita kwa uwekezaji unaoendelea kufanywa mkoa wa Pwani hususan wilaya ya Bagamoyo unaohusisha ujenzi wa Gati mpya ya mita mia tatu kwenye eneo la bandari ndogo ya bagamoyo na ujenzi wa Bandari mpaya ya bagamoyo kwenye eneo l a Mbegani na Serikali ya Mkoa itatoa ushirikiano wa dhati kipindi chote cha utekelezaji wa miradi hiyo.
Ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile ya kutembelea,Kujifunza na Kukagua Bandari ndogo ya Bagamoyo, Eneo la Ujenzi wa Bandari mpya ya Bagamoyo na Bandari Kavu ya Kwala vyote vilivyopo Mkoa wa Pwani, Kwa ajili ya kujionea miradi inayoendelea chini ya Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) Tarehe 25 Septemba, 2023
Ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile ya kutembelea,Kujifunza na Kukagua Bandari ndogo ya Bagamoyo, Eneo la Ujenzi wa Bandari mpya ya Bagamoyo na Bandari Kavu ya Kwala vyote vilivyopo Mkoa wa Pwani, Kwa ajili ya kujionea miradi inayoendelea chini ya Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) Tarehe 25 Septemba, 2023
Ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile ya kutembelea,Kujifunza na Kukagua Bandari ndogo ya Bagamoyo, Eneo la Ujenzi wa Bandari mpya ya Bagamoyo na Bandari Kavu ya Kwala vyote vilivyopo Mkoa wa Pwani, Kwa ajili ya kujionea miradi inayoendelea chini ya Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) Tarehe 25 Septemba, 2023
Ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile ya kutembelea,Kujifunza na Kukagua Bandari ndogo ya Bagamoyo, Eneo la Ujenzi wa Bandari mpya ya Bagamoyo na Bandari Kavu ya Kwala vyote vilivyopo Mkoa wa Pwani, Kwa ajili ya kujionea miradi inayoendelea chini ya Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) Tarehe 25 Septemba, 2023
Ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile ya kutembelea,Kujifunza na Kukagua Bandari ndogo ya Bagamoyo, Eneo la Ujenzi wa Bandari mpya ya Bagamoyo na Bandari Kavu ya Kwala vyote vilivyopo Mkoa wa Pwani, Kwa ajili ya kujionea miradi inayoendelea chini ya Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) Tarehe 25 Septemba, 2023
Ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile ya kutembelea,Kujifunza na Kukagua Bandari ndogo ya Bagamoyo, Eneo la Ujenzi wa Bandari mpya ya Bagamoyo na Bandari Kavu ya Kwala vyote vilivyopo Mkoa wa Pwani, Kwa ajili ya kujionea miradi inayoendelea chini ya Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) Tarehe 25 Septemba, 2023
Ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile ya kutembelea,Kujifunza na Kukagua Bandari ndogo ya Bagamoyo, Eneo la Ujenzi wa Bandari mpya ya Bagamoyo na Bandari Kavu ya Kwala vyote vilivyopo Mkoa wa Pwani, Kwa ajili ya kujionea miradi inayoendelea chini ya Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) Tarehe 25 Septemba, 2023
Ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile ya kutembelea,Kujifunza na Kukagua Bandari ndogo ya Bagamoyo, Eneo la Ujenzi wa Bandari mpya ya Bagamoyo na Bandari Kavu ya Kwala vyote vilivyopo Mkoa wa Pwani, Kwa ajili ya kujionea miradi inayoendelea chini ya Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) Tarehe 25 Septemba, 2023


Share:

WANANCHI WANAKARIBISHWA KATIKA BANDA LA TPA KATIKA MAONESHO YA TEKNOLOJIA YA MADINI

Watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania- TPA, wameendelea kutoa Elimu kwa Wananchi kuhusu Huduma zinazotolewa na TPA Katika Maonesho ya sita ya kimataifa ya Teknolojia ya Madini 2023, yanayoendelea katika Viwanja vya EPZ Bombambili Mkoani Geita.
Share:

CHUO CHA BAHARI DAR ES SALAAM CHAINGIA MAKUBALIANO NA CHUO CHA KOREA KUSINI

 

Balozi wa Korea ya Kusini Kim Yong Jung akiwa na Mjumbe wa Bodi ya Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) Capt. Adrew Matilya akishuhudia utiaji Saini wa Makubaliano ya Mafunzo kati ya chuo Bahari ya Dar es Salaam (DMI) na chuo cha Korea Istitute of Maritime and Fisheries Technology (KIMFT), Makubaliano hayo yameingiwa kati ya Mkuu wa chuo cha DMI Dkt. Tumaini Gurumo na Mwakilishi wa chuo cha KIMFT Dkt. Min Jung. Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa chuo cha Baharia Dar es Salaam (DMI) Dkt Tumaini Gurumo na Mwakilishi wa Chuo cha Korea Istitute of Maritime and Fisheries Technology (KIMFT) Dkt. Min Jung (kulia) wakionyesha nyalaka ya Mkutaba wa Makubaliano walioyaingia katika vyuo hivyo katika kubadilisha uzowefu.

Na Mwandishi wetu Dar es Salaam

Mkuu wa chuo cha Bahari Dar es Salaama (DMI) Dkt Tumaini Gurumo amesema chuo hicho kimeingia makubaliano ya miaka mitano ya kubadilishana uzoefu wa elimu ya Ubaharia na Ujenzi wa Meli na Chuo cha Korea Institute of Maritime and Fisheries Technology ambayo yatawezesha kunufaisha pande zote mbili za vyuo hivyo kwa walimu na wanafunzi .

Dkt. Gurumo amesema kuwa makubaliano hayo ni muhimu kwa maendeleo ya chuo cha DMI kwa ujumla. “Chuo cha Korea Istitute of Maritime and Fisheries Technology (KIMFT) kimeendelea kwa Teknologya ya Ujenzi wa Meli na Elimu ya Ubaharia na wana vifaa vya kisasa hivyo ni muhimu sana kwa chuo cha DMI kupata nafasi hiyo muhimu ya kushirikiana na chuo hicho” Alisema Dr. Gurumo.

Gurumo alisema kuwa makuabaliano hayo yatawezesha wanafunzi wa chuo DMI kwenda chuo cha KIMFT nchini korea kujifunza elimu ya Vitendo ili wanafunzi hao waendandane na soko la Dunia pamoja na wanafunzi kutoka KIMFT ili kuja kujifunza DMI kuhusu Elimu inayotolewa katika chuo cha DMI.

Kwa upande wake Balozi wa Korea nchini Tanzania Ndugu Kim Yong Jung amesema kuwa makuabaliano hayo yana manufaa makubwa na yatawezesha wanafunzi wa DMI kwenda nchini Korea kupata mafunzo muhimu ya vitendo katika chuo kikubwa na Teknologia ya hali ya juu.

Naye Mwakilishi wa chuo cha KIMFT Dr. Min Jung amesema kuwa anayofuraha kwa kuingia makubaliano na chuo cha DMI kwani wanafunzi na walimu watapata uzoefu mkubwa katika kuhudumia Meli na maswala yote ya ubaharia .

“ KIMFT ni chuo cha kwanza kwenye Teknologia na Ujenzi wa Meli katika nchi ya Korea, hivyo naamini chuo cha DMI kitapata uzoefu Mkubwa kwa wanafunzi na walimu kwenda Korea kujifunza” Alisama Dkt. Jung

Makubaliano hayo yameingiwa katika chuo cha DMI jijini Dar es Salaam ambapo Balozi wa Korea nchini Tanzania pamoja na viongozi wa chuo cha KIMFT na Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya DMI , Uongozi wa Chuo cha DMI na Wanafunzi walihudhuria.

Share:

DK. BITEKO : SERIKALI ITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA GGML, MPENI USHIRIKIANO MAVUNDE

Makamu Rais wa AngloGold Ashanti anayeshughulikia miradi endelevu Ghana na Tanzania, Simon Shayo (kushoto) akimpatia maelezo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko kuhusu ushiriki wa kampuni ya GGML katika maonesho hayo ya sita ya teknolojia ya madini yanayoendelea katika viwanja vya Bombambili-EPZ mjini Geita. Kulia ni Waziri wa Madini, Anthony Mavunde.
Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong akihutubia washiriki wa maonesho ya sita ya teknolojia ya madini Geita yanayoendelea katika viwanja vya Bombambili-EPZ mjini Geita.


Na Mwandishi wetu 
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko ameahidi Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwamba Serikali itaendelea kuwaunga mkono ili kuifanya sekta ya madini kukua na kuwafanya Watanzania wafaidike na rasilimali ambayo Mungu amewajalia.

Pia ametoa wito kwa uongozi wa kampuni hiyo kumpa ushirikiano wa kutosha Waziri mpya wa madini, Anthony Mavunde ili atimize malengo aliyojiwekea hasa ikizingatiwa GGML ndio mgodi mkubwa wa madini ya dhahabu kuliko migodi yote iliyopo nchini.

Dk. Biteko ametoa kauli hiyo tarehe 23 Septemba 2023 alipotembelea banda la GGML katika maonesho ya sita ya teknolojia ya madini Geita pia katika hotuba yake ya kufungua maonesho hayo yanayoendelea katika viwanja vya Bombambili -EPZA Geita mjini.

Awali akizungumza katika banda la GGML, Dk. Biteko amesema kampuni hiyo imekuwa mshirika mkubwa wa serikali lakini pia anafarijika kwa kuwa mwekezaji hai kupitia mpango wa uwajibikaji kwa jamii.

“Hata mkuu wa mkoa wa Geita (Martin Shigela) amesema ninyi ndio wadhamini wakuu wa maonesho haya kwa hiyo tunawapongeza sana,” amesema.

Amesema kwa kuwa sasa sekta hiyo inaye waziri mpya, yeye inawezekana alikuwa waziri mpole kidogo lakini sasa amekuja waziri Mavunde ambaye ni mkali hivyo apewe ushirikiano.

“Mpeni ushirikiano ili sekta hii tuitoe izidi kukua kwa sababu mgodi wa GGML ndio mfano wa migodi yote nchini kwa hiyo tusipofanya vizuri Geita na migodi mingine haitafanya vizurim tukifanya viziru migodi mingine itafanya vizuri. Lakini nawapongeza sana,” amesema Dk. Biteko.

Aidha, akizungumza katika ufunguzi wa maonesho hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kuboresha mazingira rafiki kwa wawekezaji nchini.

Strong amesema jitihada Rais Samia kufuatilia kwa umakini sekta binafsi na sekta ya madini na kutatua changamoto zke, zimeibua matumaini katika eneo wadau wengi wa sekta hizo nchini.

“GGML inaweza kuwa mfano wa kuigwa kutokana na ari hii mpya, baada ya kupata ushirikiano wa kutosha kutoka Serikalini mathalani katika utekelezaji wa sheria mpya ya madini” amesema.

Amesema sheria hiyo imetoa mwongozi wa usimamizi wa sekta ya madini kuhusu masuala ya kodi, malipo ya mrabaha, na matumizi ya fedha za uwajibikaji wa kampuni kwa jamii, huku pia ikisisitiza ujumuishaji wa uchumi wa ndani.

“Tunafarijika kusema kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, GGML imeshirikiana kwa kiasi kikubwa na Serikali ya mkoa wa Geita, kwa kutenga zaidi ya Sh bilioni 46 kupitia Mfuko wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR). Fedha hizi zimesaidia kutekeleza miradi kadhaa inayolenga jamii ikiwemo ujenzi wa soko la kisasa na vituo vya huduma ya afya ikiwemo miundombinu ya elimu inayolenga mahitaji ya ndani,” amesema.

Pia amesema maonesho hayo ambayo mwaka huu GGML ni mdhamini mkuu, kampuni hiyo inajihisi faraja kuona yanapiga hatua na kuwa kitovu kkuu cha biashara na uwekezaji hasa baada ya GGML kutumia uboreshaji wa eneo hilo la Mamlaka ya Maeneo ya Uzalishaji Bidhaa kwa Mauzo ya Nje (EPZA) yenye ukubwa wa ekari 200

Share:

SERIKALI YAPANGA KUNUNUA MITAMBO 15 YA UCHORONGAJI MIAMBA



Oktoba 2023 mitambo mitano itatolewa mkoani Dodoma

• Sekta inachangia 56 % ya fedha za kigeni

Serikali kupitia Wizara ya Madini imepanga kununua mitambo 15 ya uchorongaji wa miamba kwa ajili ya utafiti wa kina wa Madini.

Hayo yamebainishwa leo Septemba 25 , 2023 na Waziri wa Madini Mhe. Mavunde wakati akiongea katika kipindi cha Jambo Tanzania (TBC1) kutokea  viwanja vya maonesho vya  EPZ bomba mbili mkoani Geita. 

Akielezea kuhusu mkakati wa  VISION 2030 Madini ni Maisha na Utajiri Mhe. Mavunde  amesema kuwa Serikali imejipanga kufanya utafiti wa Madini nchi nzima kwa lengo la kupata taarifa zitakazo weza kufungamanisha sekta ya Madini na Sekta nyingine za kiuchumi.

Akifafanua hali ya utafiti wa Madini  amesema mpaka sasa utafiti wa kina umefanyika kwa asilimia 16 tu ambazo taarifa zake ndio zinatumika lengo  la Serikali ni kuongeza taarifa kupitia tafiti nyingine ziitakazofanywa na GST.

Mpaka sasa Sekta ya Madini inachangia asilimia 56 ya Fedha za kigeni ambazo zinachangia asilimia 9.1 ya pato la Taifa(GDP) , hii ni kwa utafiti wa 16% uliofanyika , hivyo kufikia 2030 tutakuwa  tumefanya utafiti nchi nzima.

Sambamba na hapo Mhe. Mavunde ameeleza kuwa Wizara ya Madini kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira  zitaendeleza juhudi za kutunza mazingira kama Sheria zinavyoelekeza.

Pia Mhe. Waziri Mavunde ameshiriki zoezi la upandaji miti katika viwanja vya maonesho vya EPZ.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU SEPTEMBA 25,2023






























































Share:

Sunday, 24 September 2023

KIKAO KAZI NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI KWA UTARATIBU WA OFISI YA MSAJILI WA HAZINA


Share:

NSSF INAVYOWEKA ALAMA YA MAFANIKIO MAONESHO YA MADINI

*Mkurugenzi Mkuu amueleza Naibu Waziri Mkuu jinsi wanavyowafikia wachimbaji wadogo

*Mkoa wa Geita pekee walikusanya bilioni 56 kwa mwaka fedha ulioishia Juni 2023


Na MWANDISHI WETU, GEITA

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba, amemueleza Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko kuwa NSSF inashiriki Maonesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini kwa sababu ndio Mfuko pekee wenye jukumu la kuandikisha wanachama kutoka sekta binafsi na sekta isiyo rasmi wakiwemo wachimbaji wadogo wa madini ili waweze kujiunga na kujiwekea akiba kwa ajili ya maisha yao ya sasa na baadaye.

Mshomba amesema hayo tarehe 23 Septemba, 2023 alipokuwa akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Mkuu alipotembelea banda la NSSF katika maonesho hayo yenye kauli mbiu isemayo ‘Matumizi ya Teknolojia Sahihi katika Kuinua Wachimbaji Wadogo Kiuchumi na Kuhifadhi Mazingira’ yanayoendelea katika viwanja vya EPZA, Bombambili Mkoani Geita.

Amesema tokea maonesho hayo yalipoanza mwaka 2018, NSSF imekuwa na mafanikio makubwa kwani ushiriki wake umechangia ukuaji wa Mfuko ambapo kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 2023, walikusanya michango ya takribani shilingi bilioni 56.

“Wakati Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani, hapa Mkoani Geita pekee NSSF ilikuwa inakusanya michango ya shilingi bilioni 29 ambayo ni mara mbili katika kipindi hiki cha miaka miwili na nusu ya uongozi wa Mheshimiwa Rais, kwa hiyo kwetu sisi ni mafanikio makubwa sana na tunaamini tutaendelea kufanya vizuri zaidi,” ameeleza Mshomba.

Aidha, amesema mafanikio ya NSSF kwa ujumla ni mazuri ambapo katika mwaka wa fedha ulioishia Juni 2023, thamani ya michango iliyokusanywa ilikuwa ni ya shilingi trilioni 1.66 na katika mwaka wa fedha ulioishia Juni 2022, thamani ya michango iliyokusanywa ilikuwa ni shilingi trilioni 1.48.

Mshomba amesema hilo ni ongezeko kubwa na kwamba thamani ya NSSF imeendelea kukua kwa kasi ambapo kwa mujibu wa hesabu zilizokaguliwa mwezi Juni 2022, thamani ya Mfuko ilikuwa trilioni 6.08 na kuwa mpaka kufikia mwezi Juni 2023 thamani ya Mfuko imefikia trilioni 7.6 kwa hesabu ambazo zinaendelea kukaguliwa.

“Huo ni ukuaji mkubwa mno hasa ukizingatia kabla ya hapo na baada ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuingia madarakani thamani ya Mfuko ilikuwa ni trilioni 4.8 hivyo mafanikio hayo ni kazi kubwa anayofanya Mheshimiwa Rais ya kuvutia wawekezaji,” amesema Mshomba.

Amesisitiza kuwa, maonesho hayo ya madini tokea yalipoanza yamekuwa chachu ya ongezeko hilo la wanachama na michango, ambapo ameushukuru uongozi wa Mkoa wa Geita chini ya Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Martine Shigela kwa ushirikiano mkubwa wanaowapatia.

Kuhusu matumizi ya TEHAMA, Mshomba amesema NSSF imeweka kipaumbele kikubwa katika matumizi ya TEHAMA ili kurahisisha huduma za wanachama wao jambo ambalo linaendana na kauli mbiu ya maonesho ya madini.

Mshomba amesema NSSF inaendelea kusajili wanachama wapya kutoka sekta binafsi na sekta isiyo rasmi hususan wachimbaji wadogo ambao ndio lengo la Mfuko kushiriki katika maonesho hayo ya madini.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger