Saturday, 23 September 2023
Friday, 22 September 2023
WADAU WAVUTIWA NA BANDA LA GST KATIKA MAONESHO YA TEKNOLOJIA YA MADINI MKOANI GEITA
● Wadau wa sekta ya Madini waona umuhimu wa kutumia taarifa za GST
Wadau mbalimbali wameeleza kuvutiwa na kitabu cha Madini Yapatikanayo Tanzania kinachopatikana katika Banda la Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) lililopo kwenye maonesho ya sita ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita.
Hayo yamebainishwa leo tarehe 22 Septemba 2023 na Meneja Masoko wa GST wakati akizungumza kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa GST, amesema kuwa kitabu hicho ni toleo jipya ambalo limetoka mwaka 2023 likiwa na taarifa mbalimbali zinazoonesha madini yanayopatikana nchini Tanzania kuanzia ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata na Kijiji.
Priscuss amefafanua kuwa toleo hili ni tofauti na toleo la zamani, hii ni kutokana na toleo hilo jipya kuwa na taarifa nyingi zaidi za uwepo wa madini(occurrences) na pia linaelezea jiolojia ya mkoa husika pamoja na ramani yake.
Akizungumzia kuhusu uwepo wa kitabu hicho ,Priscus ametumia fursa hiyo kuwaalika wadau wote wakiwemo wachimbaji wadogo wa madini kutumia kitabu hicho sambamba na taarifa nyingine za jiosayansi utafiti wa jiosayansi ili kuongeza tija katika shughuli za utafutaji na uchimbaji madini.
Sambamba na kitabu hicho GST katika maonesho hayo imekuja na machapisho mbalimbali ya jiosayansi yanayoelezea jiolojia na aina mbalimbali za madini yanayopatikana nchini Tanzania.
Aidha , akielezea kuhusu uchunguzi wa madini maabara, ametoa wito kwa wadau kutumia maabara ya madini ya GST kwani ni ya kisasa na majibu yake ni ya uhakika. Pia, amewaalika wadau wenye changamoto za kujua miamba au madini waliyonayo kufika katika banda hilo na kupima bure ili watambue aina ya miamba na madini waliyonayo.
Maonesho ya Teknolojia ya madini kwa mwaka 2023 yanabebwa na kaulimbiu inayosema "Matumizi sahihi ya Teknolojia katika kuinua Wachimbaji wadogo kiuchumi na kuhifadhi Mazingira
TANZANIA KUBORESHA MFUMO WA USIMAMIZI NA UTOAJI WA TAARIFA ZA ANGA
Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Hamza Johari (katikati) akisaini Kandarasi ya Mkataba wa Utekelezaji wa Mradi wa Mfumo wa Usimamizi na Utoaji wa Taarifa za Anga na Kampuni ya Indra Avitech wenye thamani ya Tsh. Bilioni 9. Bw. Simon Masike alisaini kwa upande wa kampuni ya Indra Avitech. Hafla hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya TCAA Septemba 22, 2023.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imesaini kandarasi ya mfumo wa usimamizi wa taarifa za anga na Kampuni ya Indra Avitech kwa ajili ya kuboresha usalama wa safari angani katika anga ya Tanzania kupitia utoaji wa taarifa za anga zenye ubora wa hali ya juu, salama na muhimu kwa wakati sahihi kwa wadau mbalimbali wa usafiri wa anga.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari leo Mamlaka hiyo imesaini mkataba wenye thamani ya Shilingi Bilioni Tisa kwa ajili ya kubuni, kusambaza, kusanikisha, kuunganisha, na kuzindua Mfumo wa Usimamizi wa Taarifa za Anga ambapo Mradi huu utatekelezwa kwa miezi 18.
Amesema sehemu ya mpango thabiti wa Usimamizi wa Taarifa za Anga (AIM) wa kuboresha mfumo wake wa taarifa za anga kwa kutoa usimamizi wa taarifa za anga kwa njia ya kisasa zaidi kwa kutoa na kubadilishana taarifa za anga za dijitali zenye ubora na kushirikiana na pande zote hivyo kuhakikisha usalama, utaratibu, na ufanisi wa urambazaji wa anga wa kitaifa na kimataifa.
“Lengo la utekelezaji wa Mradi wa Mfumo wa Usimamizi wa Taarifa za Anga ni kuboresha mfumo wa AIM katika kuboresha usahihi wa data, upatikanaji, na ufanisi kwa kuzingatia mahitaji ya Upandishaji wa Mfumo wa Anga wa Usafiri (ASBU), na kufuata viwango vya kitaifa na kimataifa” ,Alisema Johari
Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Hamza Johari (katikati), Mkurugenzi Huduma za Sheria TCAA, Maria Makala (wa pili kulia), Mwakilishi wa Kampuni ya Indra Avitech , Bw. Simon Masike(wa pili kushoto) wakisani Kandarasi ya Mkataba wa Utekelezaji wa Mradi wa Mfumo wa Usimamizi na Utoaji wa Taarifa za Anga na Kampuni ya Indra Avitech wenye thamani ya Tsh. Bilioni 9 iliyofanyika Makao Makuu ya TCAA Septemba 22, 2023.
Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Hamza Johari (wa pili kushoto) akikabidhiana mkataba na Mwakilishi wa Kampuni ya Indra Avitech, Bw. Simon Masike mara baada ya kusaini Kandarasi ya Mkataba wa Utekelezaji wa Mradi wa Mfumo wa Usimamizi na Utoaji wa Taarifa za Anga na Kampuni ya Indra Avitech wenye thamani ya Tsh. Bilioni 9 iliyofanyika Makao Makuu ya TCAA Septemba 22, 2023. Mkurugenzi Huduma za Sheria TCAA, Maria Makala (wa pili kulia).
Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Hamza Johari (katikati) pamoja na Mwakilishi wa Kampuni ya Indra Avitech, Bw. Simon Masike ( wa pili kushoto) wakionesha mkataba mara baada ya kusaini Kandarasi ya Mkataba wa Utekelezaji wa Mradi wa Mfumo wa Usimamizi na Utoaji wa Taarifa za Anga na Kampuni ya Indra Avitech wenye thamani ya Tsh. Bilioni 9 iliyofanyika Makao Makuu ya TCAA Septemba 22, 2023.Wa pili kulia ni Mkurugenzi Huduma za Sheria TCAA, Maria Makala
Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Hamza Johari (katikati) akizungumza wakati wa kusaini Kandarasi ya Mkataba wa Utekelezaji wa Mradi wa Mfumo wa Usimamizi na Utoaji wa Taarifa za Anga na Kampuni ya Indra Avitech wenye thamani ya Tsh. Bilioni 9 iliyofanyika Makao Makuu ya TCAA Septemba 22, 2023.
Mwakilishi wa Kampuni ya Indra Avitech, Bw. Simon Masike akizungumza wakati Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) waliposaini Kandarasi ya Mkataba wa Utekelezaji wa Mradi wa Mfumo wa Usimamizi na Utoaji wa Taarifa za Anga na Kampuni ya Indra Avitech wenye thamani ya Tsh. Bilioni 9 iliyofanyika Makao Makuu ya TCAA Septemba 22, 2023.
Kaimu Mkurugenzi Wa Huduma Za Uongozaji Ndege TCAA, Hamis Kisesa akizungumza wakati Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) waliposaini Kandarasi ya Mkataba wa Utekelezaji wa Mradi wa Mfumo wa Usimamizi na Utoaji wa Taarifa za Anga na Kampuni ya Indra Avitech wenye thamani ya Tsh. Bilioni 9 iliyofanyika Makao Makuu ya TCAA Septemba 22, 2023.
Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi TCAA,Bw. Daniel Malanga(katikati), Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka Bw. Teophory Mbilinyi (kushoto) na Mkurugenzi Huduma za Sheria TCAA, Maria Makala wakiwa kwenye hafla ya kusaini Kandarasi ya Mkataba wa Utekelezaji wa Mradi wa Mfumo wa Usimamizi na Utoaji wa Taarifa za Anga.
Meneja Uhusiano na Mawasiliano TCAA, Yessaya Mwakifulefule(kushoto), Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) kinachomilikiwa na TCAA, Aristid Kanje (katikati) na Afisa Mtoa Taarifa za Anga Mwandamizi (TCAA) wakiwa kwenye hafla ya kusaini Kandarasi ya Utekelezaji wa Mradi wa Mfumo wa Usimamizi na Utoaji wa Taarifa za Anga.
Baadhi ya wadau mbalimbali wa uSafiri wa anga wakiwa kwenye hafla ya kusaini Kandarasi ya Mkataba wa Utekelezaji wa Mradi wa Mfumo wa Usimamizi na Utoaji wa Taarifa za Anga.
Picha za pamoja
BREAKING NEWS: HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WENGINE WAPYA WALIOONGEZWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO TAREHE 20.9.2023
Kama kawaida MaswaYetu Blog inakuletea taarifa amabazo ni muhimu sana kwa mustakabli mzima wa Taifa letu,
Chini hapo ni majina MAPYA ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha 5 2023 awamu ya pili mwezi huu septemba.
KUYAONA MAJINA HAYO
WANANCHI KATA ZA LUHUNGA NA IHANU WILAYANI MUFINDI KUNUFAIKA NA UJENZI WA BARABARA YA IYEGEYA- LULANDA
Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) inaendelea na ujenzi wa barabara ya Iyegeya- Lulanda yenye urefu wa Km 10.4 kwa kiwango cha lami kwa kutumia Teknolojia mbadala ya ECO Roads ikiwa ni utekelezaji wa malengo ya Serikali ya kupunguza gharama za ujenzi na matengenezo ya barabara na kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati ili kuwezesha wananchi kusafiri kwa urahisi na kusafirisha mazao yao kwa urahisi.
Akizungumza wakati wa ziara maalum ya ukaguzi wa mradi huo, Meneja wa TARURA Mkoa wa Iringa Mhandisi Makori Kisare ameeleza kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo uliofikia asilimia 50 ya utekelezaji na kubainisha kuwa matarajio makubwa ni kukamilika kwa mradi huo ndani ya muda uliopangwa.
"Kasi ya utekelezaji wa mradi huu ni kubwa na matarajio ni kwamba mradi huu utakamilika kwa wakati na kuwanufaisha wananchi ili waweze kusafiri na kusafirisha mazao yao kwa urahisi kutoka eneo la Sawala hadi Lulanda", alisema Mhandisi Makori.
Barabara hiyo ya Iyegeya kwenda Lulanda tayari Mkandarasi anaendelea na hatua mbalimbali za utekelezaji na ujenzi wake unatarajia kukamilika ifikapo Agosti 2024.
Barabara ya Iyegeya- Lulanda inajengwa ikiwa ni mwendelezo wa barabara ya Sawala-Mkonge-Iyegeya kilomita 30 ambazo tayari zilishajengwa kupitia mradi wa Agri-Connect.
NAIBU WAZIRI NDERIANANGA AFANYA MAZUNGUMZO
Naibu Waziri Nderiananga akutana na kufanya mazungumzo na RC Morogoro
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima alipomtembelea ofisini kwake kwa lengo la kujadili utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo na Uvuvi ya AFDP inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima alipomtembelea ofisini kwake kwa lengo la kujadili utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo na Uvuvi (AFDP)inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima alipomtembelea ofisini kwake kwa lengo la kujadili utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo na Uvuvi (AFDP)inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.