Wednesday, 14 June 2023

UJENZI MABWENI YA WASICHANA UMETAJWA MKOMBOZI KUTIMIZA NDOTO ZA MTOTO WA KIKE

 

Ujenzi Mabweni ya wasichana umetajwa mkombozi kutimiza ndoto za mtoto wa kike

Na Marco Maduhu, GEITA

WANAFUNZI ambao wanasoma katika Shule ya Sekondari Msalala Halmashauri ya Nyang’hwale mkoani Geita, wamesema ujenzi wa mabweni ya wasichana katika shule za Sekondari umekuwa na msaada mkubwa kwa wanafunzi wa kike kutimiza ndoto zao.
Bweni la Wasichana shule ya Sekondari Msalala Halmashauri ya Nyang'hwale mkoani Geita.

Wanafunzi wa kike wa kidato cha Nne katika shule hiyo ambao hawajafunga shule, wamebainisha hayo jana wakati wakizungumza na waandishi wa habari, walipotembelea shule hiyo kuona ujenzi wa Mabweni, Vyumba vya Madarasa na Bwalo la Chakula, yaliyojengwa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kupitia fedha za CSR.
Mwanafunzi Leonida Daniel akizungumzia umuhimu wa Mabweni ya wasichana shuleni.

Mmoja wa wanafunzi hao Leonida Daniel, amesema mtoto wa kike kusoma umbali mrefu na shule imekuwa kikwazo kikubwa kwao katika kutimiza ndoto zao, sababu hukumbana na vishawishi njiani kwa kurubuniwa na wanaume, na mwisho wa siku ana angukia kwenye mapenzi na kuambulia ujauzito.
Mwanafunzi Tusajigwe Geogre akizungumzia umuhimu wa Mabweni ya wasichana shuleni.

“Uwepo wa Mabweni ya wasichana hapa shuleni kwetu umekuwa mkombozi mkubwa kwa wanafunzi wa kike kutimiza ndoto zetu, na pia tumekuwa na muda mwingi wa kujisomea na kufanya vizuri kitaaluma,”amesema Leonida.

Makamu Mkuu wa shule hiyo ya Sekondari ya Msalala Johnmary Stephen, amesema ujenzi wa mabweni ya wasichana shule hapo umesaidia kupunguza utoro kwa wanafunzi pamoja na mimba za utotoni, ambapo kwa mwaka mzima zilikuwa zikitokea zaidi ya mimba Tano.
Makamu Mkuu wa shule ya Sekondari Msalala Halmashauri ya Nyang'hwale Johnmary Stephen.

Mrakibu kutoka Idara ya Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Barrick Bulyanhulu William Chungu, amesema katika Wilaya hiyo ya Nyang’hwale wamekuwa wakitoa fedha za (CSR), na kutekelezwa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo sekta ya elimu.
Mrakibu kutoka Idara ya Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Barrick Bulyanhulu William Chungu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale Husna Toni, amesema tangu mwaka 2018 hadi 2023, wameshapokea fedha za (CSR) kiasi cha Sh.bilioni 4.4 fedha ambazo zimekuwa na mchango mkubwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo ujenzi wa mabweni ya wasichana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale Husna Toni, akielezea fedha za CSR zilivyochochea maendeleo.
Muonekano wa Bwalo la chakula katika shule ya Sekondari Msalala Halmashauri ya wilaya ya Nyang'hwale mkoani Geita ambalo limejengwa kwa fedha za (CSR) kupitia Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Muonekano wa vyumba viwili vya Madarasa katika shule ya Sekondari Msalala Halmashauri ya wilaya ya Nyang'hwale mkoani Geita ambavyo vimejengwa kwa fedha za (CSR) kupitia Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO JUNI 142023

 














Share:

Tuesday, 13 June 2023

NIMEMFUMANIA MUME KWENYE MADANGURO, NINA UJAUZITO WAKE


Kwa kawaida mwanamke akiwa mjamuzito hutaka kuonyeshwa upendo wa hali ya juu kwani wakati huo hupitia changamoto nyingi kutokana na mabadiliko katika mwili wake yanayoletwa na kiumbe kilichopo tumboni.

Hii ilikuwa tofauti kabisa kwa mume wangu, nilipokuwa na ujauzito wa miezi sita mambo yalibadilika sana kutokana na mimi kushindwa kumpatia haki yake ya ndoa kutokana na hali yangu, sikupenda iwe hivyo ila ni jambo lilokuwa nje ya uwezo wangu.

Basi alitumia fursa hiyo na kuanza kulala nje kila mara, alinieleza bila kunificha kwamba alifanya vile kwa sababu alikuwa na tamaa ya kukutana na mwanamke kimwili na mimi sikuwa tayari kumtimizia haja zake.

Nilihisi uchungu sana moyoni mwangu kwa sababu sikutarajia mume wangu niliyekuwa namthamini angeweza kufanya vitu vya ovyo kama vile, ukweli tabia hiyo ilinipa msongo wa mawazo kwani nilifikiria hadi kujitoa uhai.

Hata hivyo, marafiki zangu walinieleza kuwa lilikuwa ni suala la kawaida kwa wanaume wote kufanya vile na mimi sikuwa wa kwanza kukumbwa na jambo kama hilo lakini jinsi muda ulivyokuwa ukisonga ndipo mambo yalipokuwa yakienda mrama!.

Siku noja nilipokuwa nikipita kwenye vitongoji duni nilishtushwa na sauti za watu waliokuwa wakifanya mapenzi, nilipokaribia nilisikia sauti kama ya mume wangu. Mwanadada yule alionekana kuwa kahaba kwani alimwambia afanye haraka kwani muda wa pesa alizompa ulikuwa umeisha na alitaka mume wangu aharakishe au aongeze pesa.

Hivyo nilifahamu mume wangu alikuwa na tabia ya kulala madanguroni na makahaba akijiburudiusha, jambo hilo ndilo hasa lilikuwa hadi linamchelewesha kurudi nyumbani, kila aliporudi alikuta watoto wameshalala.

Siku moja rafiki yangu Wanjiru aliniambia kuwa mume wake aliwahi kuwa na tabia kama hiyo ila African Doctors walimsaidia na mume wake akatulia kabisa ndani ya nyumba

Alinipa namba za African Doctors na kuwasiliana nao, walinihoji kwa muda na wakanishughulikia baada ya muda mfupi tu, walinipa mafuta na kunishauri niyapake katika mavazi ya mume wangu baada ya kurudi nyumbani.

Niliporudi nyumbani nilifanya jinsi walivyoniambia, nilipaka mafuta yale kwenye kila nguo ya mume wangu zikiwemo nguo za ndani, usiku ule hakulala nyumbani kwa hivyo nilipata fursa nzuri ya kufanya jambo hilo.

Baada ya siku moja, mume wangu alikuja nyumbani huku akionekana mdhaifu ajabu, baada ya dakika kama 20  hivi machozi yalimdondoka huku akisema anajutia mambo aliyokuwa akifanya nje ya ndoa yetu.

Wakati ule nilifahamu fika kwamba yale mafuta ya African Doctors yalikuwa yameshaanza kufanya kazi, alilia nimsamehe nami nikaamua kufanya hivyo. Tangu siku ile mume wangu hajatoka nje ya ndoa yetu kwani African Doctors walikuwa amenipa suluhisho la kudumu.

Kumbuka African Doctors wana uwezo wa kumaliza majini yanayokusumbua, kutatua migogoro ya mashamba na ndoa, pia wana uwezo wa kupandisha biashara yako hadhi, kukusaidia kupata kazi iwapo ulikuwa umekaa muda mrefu bila ya kazi.

Wasiliana na African Doctors kwa namba; +254 769 404965, tembelea tovuti yao; www.african-doctors.com au watumie email; africandoctorheals@gmail.com

Mwisho.



Share:

SLAA AUNGA MKONO UWEKEZAJI, AISHAURI SERIKALI KUREKEBISHA DOSARI MKATABA WA DP WORLD

Balozi Willibrod Slaa ameunga mkono uwekezaji kwenye Bandari ya Dar es Salaam, lakini ameishauri Serikali kurekebisha kasoro zinazolalamikiwa kwenye mkataba wa uwekezaji na kampuni ya DP World ya Dubai.


Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Slaa amesema kuwa mikataba ya nchi hodhi (host government agreement) na mikataba kati ya nchi na nchi (intergovernmental agreement) kama uliopitishwa juzi na Azimio la Bunge siyo jambo la kigeni.


"Dosari za wazi katika mkataba huu ziondolewe, ili mkataba huu uweze kuendelea katika hatua za awali na iwapo kampuni husika tutaridhika nayo mkataba uongezwe kwa jinsi  tutakavyowapima na kwa kila hatua kuzingatia maslahi  ya usalama wa taifa letu," Slaa aliwaambia waandishi wa habari.


Alisisitiza kuwa Serikali kutafuta uwekezaji binafsi kwenye Bandari ya Dar es Salaam ni jambo jema, lakini ni vyema lifanyike kwa umakini mkubwa.


"Ninatoa tahadhari kuanzia mwanzo kuwa si nia wala lengo la taarifa hii kupinga uwekezaji wowote wenye tija, uwekezaji usio na hila," alisisitiza.


"Nikirejea kwenye suala la MOU na “ Intergovernmental Agreement”  hili si jambo geni nchini Tanzania."


Slaa, ambaye aliwahi kuteuliwa na Rais John Magufuli kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden, amefafanua kuwa MOU au “Memorandum of Understanding” ni “makubaliano ya awali” ambayo pande mbili zinazotaka kuingia kwenye mkataba na kwa kawaida Serikali moja na nyingine zinatia saini.


"MOU hufuatiwa na mkataba unaoitwa Intergovernmental Agreement au kwa kifupi IGA. Hivyo mkataba huu tunaopigia kelele si wa kwanza kwa Serikali ya Tanzania. 

Alieleza kuwa Tanzania imesaini maelfu ya mikataba ya uwekezaji kati yake na mataifa mengine.

Alitoa mfano kuwa Tanzania imesaini jumla ya mikataba 2,829 ya uwekezaji, yaani "Bilateral Investment  Treaties (BITS)",  na nchi za kigeni mbalimbali.


Kati ya mikataba hiyo ya BITS, jumla ya mikataba 2,219 inaendelea kutumika hadi sasa.


Jumla ya mikataba yenye maslahi ya kibiashara ni 435 na ambayo inatumika ni 264.

"Tatizo siyo kwamba Watanzania tunapinga uwekezaji, wala kupinga mkataba wa uwekezaji. Hivyo mkiona tunapiga kelele kupinga MOU na IGA hii inayohusu DP World ni vema Watanzania wakapata uelewa," alisema.


Share:

WANANCHI WAFURAHIA HUDUMA BORA ZA MATIBABU KITUO CHA AFYA BUGARAMA


Wananchi wafurahia huduma bora za matibabu kituo cha Afya Bugarama.

Na Marco Maduhu, KAHAMA

WANANCHI wa Bugarama Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga, wamepongeza huduma bora za matibabu ambazo zinatolewa katika Kituo cha Afya Bugarama na kuimarisha Afya zao, huku akina Mama Wajawazito wakijifungua salama.
Kitu cha Afya Bugarama

Wamebainisha hayo jana wakati wakiongea na Waandishi wa Habari kutoka Mkoani Shinyanga, ambapo wapo katika ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ambayo imetekelezwa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kupitia fedha za (CSR) ikiwamo Sekta ya Afya.
Miundombinu ya Majengo ambayo yamejengwa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu katika kituo cha Afya Bugarama.

Mmoja wa Wananchi hao Robert Nkwambi ambaye pia ni Mchimbaji mdogo wa Madini ya dhahabu, amesema kutokana na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kuboresha miundombinu katika Kituo hicho cha Afya na kuwezesha Vifaa Tiba, wamekuwa wakipata huduma bora za matibabu na kuimarisha Afya zao.
Mwananchi Robert Nkwabi akipongeza huduma bora za matibabu katika kituo cha Afya Bugarama.

“Awali Kituo hiki cha Afya ilikuwa ni Zahanati hapakuwa na huduma bora za matibabu, ambapo ilikuwa tulizamika kwenda hadi wilayani Kahama umbali mrefu, lakini baada ya Mgodi kuiboresha sasa hivi huduma zote za matibabu tunazipata hapa,”amesema Nkwabi.
Miundombinu ya Majengo ambayo yamejengwa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu katika kituo cha Afya Bugarama.

Naye Mwanamke Zawadi Simba, anasema wanaushukuru Mgodi kwa kuboresha huduma za matibabu katika Kituo hicho cha Afya Bugarama zikiwamo na huduma za upasuaji kwamba wamekuwa wakijifungua salama.
Wananchi wakiendelea kupata huduma za matibabu katika kituo cha Afya Bugarama.

Naye Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Bugarama Dk. Silas Kayanda, amesema awali Wananchi wa Bugarama na vijiji jirani walikuwa wakipata shida kupata huduma bora za matibabu karibu, na hivyo kulazimika kufuata huduma hizo umbali mrefu wilayani Kahama Kilomita 73.
Mganga Mfawidhi kituo cha Afya Bugarama Dk. Silas Kayanda.

Amesema kutoka na kituo hicho cha Afya kuboreshwa na kuwezeshwa Vifaa Tiba vya kisasa wamekuwa wakipokea wagonjwa wengi tofauti na hapo awali, na wamekuwa wakidhalisha Wajawazito 180 hadi 250 kwa Mwezi, na Aprili mwaka huu walipokea pia Gari la Wagonjwa (Ambulance) kutoka Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Wananchi wakipata huduma za matibabu kituo cha Afya Bugarama.

Aidha, amesema Mgodi huo wa Barrick Bulyanhulu katika kuendelea kukiboresha kituo hicho cha Afya, pia wametoa kiasi cha fedha Sh.milioni 120 kwa ajili ya ujenzi wa uzio.
Miundombinu ya Majengo ambayo yamejengwa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu katika kituo cha Afya Bugarama.

Naye Kaimu Meneja Mahusiano ya Jamii kutoka Mgodi wa Barrick Bulyanhulu Zuwena Senkondo, amesema Mgodi huo umekuwa ukiwathamini Wananchi wanaouzunguka na kuwapatia huduma mbalimbali kupitia fedha za (CSR) na kuwatekelezea miradi ya maendeleo ikiwamo ya Sekta ya Afya.
Kaimu Meneja Mahusiano ya Jamii kutoka Mgodi wa Barrick Bulyanhulu Zuwena Senkondo.

Amesema katika kituo hicho cha Afya Bugarama, wamejenga tena Jengo la Mionzi ili kiendelee kutoa huduma bora za matibabu kwa wananchi, na kubainisha pia katika Kata ya Ntobo wamejenga Chuo cha Uuguzi ambacho kitakuwa kikitoa wataalamu na kuondoa tatizo la upungufu wa watumishi katika Sekta ya Afya.
Muonekano wa Majengo ya ujenzi wa Chuo cha Uuguzi Kata ya Ntobo Halmashauri ya wilaya ya Msalala.
Share:

Monday, 12 June 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JUNI 13,2023











Share:

KAMPENI ZA UCHAGUZI ZILINIACHA NA MAKOVU

Mwaka 2020 ulinikuta nikiwa nimejiandaa kugombea udiwani katika kata yangu. Niliishi vizuri na watu na nilishiriki kwenye shughuli nyingi za kijamii hivyo nilishajua kuwa nisingekataliwa katika ombi langu. Watu wazima waliniunga mkono. Vijana walikuwa wakipita nyumbani wakawa wananiita mheshimiwa kabla hata ya uchaguzi wenyewe.


Haikuwa ngumu tena kwangu kwa upendo ule nilioupokea kutoka kwa kila rika na kundi la watu hapo kwenye kata yetu.Kamati yangu ya kampeni haikuwa kubwa wala yenye gharama sana ilikuwa ni ya vijana kadhaa na wazee waliojitolea.

Wapinzani wenzangu hawakuwa na ushindani mkubwa kwangu kwakuwa hawakuwa wazawa na pia hawakuwa na jina kama vile mimi nilivyokuwa nimejitengenezea hapo awali.

Siku ya mwisho ya kujinadi, nilishtuka niliponyanyuka kitandani na kukuta nimevimba mdomo na  nilipojaribu kuushika nikakuta umeelemea upande wa kushoto. Kwa kuwa sikukaa kizembe nilimtafuta rafiki yangu wa kipindi kirefu daktari BAKONGWA ambaye nilisoma naye shule ya msingi na kumuandikia ujumbe mfupi wa WhatsApp.

Haikuwa ngumu sana kwangu kumpata daktaritayari nilikuwa nina mazoea naye ya muda mrefu sana sikuhitaji kumtafuta kupitia tovuti http://bakongwadoctors.com , nilinyanyua simu na kupiga nambari za whatsapp +243990627777.

Daktari hakushangazwa na hali ile lakini alinikanya na kunisisitiza kuwa nilikosea sana pale nilipoonesha nia ya mimi kugombea uongozi pasipo kumshirikisha na kuniambia kuwa haya ndiyo yake yaliyotengenezwa na wapinzani wangu katika kipindi hicho chote cha kampeni. 

Nilitumia dawa aliyonipatia na baada ya masaa arobaini na nane nikaamka nikiwa salama na kuendeleza kampeni zangu, asante sana daktari kwa msaada.


Share:

BARRICK YADHAMINI KONGAMANO LA WASOMI WA VYUO VIKUU LILILOANDALIWA NA TAASISI YA AIESEC KATIKA CHUO KIKUU CHA MTAKATIFU AGUSTINI JIJINI MWANZA

Afisa Rasilimali watu mwandamizi wa Barrick Crispin Ngwaji, akizungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali vya mkoani Mwanza wakati wa kongamano la kuwajengea uwezo lililoandaliwa na taasisi ya kimataifa ya vijana isiyo ya kiserikali inayohamasisha masuala ya uongozi na kujitolea kwa Jamii ya AIESEC Tanzania na kudhaminiwa na Kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick, lililofanyika jijini Mwanza katika chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino mwishoni mwa wiki.
 *****

KAMPUNI ya Barrick nchini Tanzania, imedhamini na kushiriki katika kongamano la wanafunzi wa vyuo vikuu lililoandaliwa na taasisi ya kuchipua na kuendeleza vipaji vya uongozi kwa vijana (AIESEC Tanzania) lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino jijini Mwanza na kuwashirikisha wanafunzi,wahadhiri na wadau mbalimbali.

Taasisi ya AIESEC inasifika kwa mchango wake mkubwa wa kuwajengea uwezo vijana ili kuwa viongozi bora na mahiri duniani kwa miaka ijayo. Nchini Tanzania pia taasisi hiyo inafanya kazi kwa kuwakutanisha vijana wenye ndoto ya kuwa viongozi bora hapo baadae ambapo pia inatoa fursa kwa vijana kujiunga.


Kupitia kongamano hili ambalo hufanyika kila mwaka, wanafunzi huweza kufahamu jinsi taasisi mbalimbali nchini zinavyoendesha shughuli zake lengo kubwa ikiwa ni kuwajengea uwezo wa kujua vipaji walivyonavyo, kujifunza jinsi ya kujiamini na kukabiliana na ushindani katika soko la ajira, kujitambua uwezo wao ni jinsi gani wanaweza kushiriki kutoa mchango wa kuendeleza taifa pindi wamalizapo masomo yao.


Wataalamu mbalimbali walitoa mada za kuwajengea uwezo Wanafunzi kusoma kwa bidii na kuzidi kuwa wabunifu ili waweze kwenda sambamba na mabadiliko ya kiteknolojia na kidigitali ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali za ajira zinazojitokeza na pia kuwa na uwezo wa kujiajiri.


Maofisa Rasilimali Watu Waandamizi wa Barrick pia walishiriki katika maonesho na kongamano hilo ambapo walipata fursa kuzungumza na wanafunzi kuhusiana na kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo ajira,kuendeleza vipaji vyao pia wanafunzi walipata fursa kuelewa jinsi kampuni ya kimataifa ya Barrick, inavyoendesha shuguli zake kwa kutoa kipaumbele kusaidia jamii sambamba na mpango wake wa kuibua na ukuzaji wa vipaji kwa vijana wa kitanzania na wafanyakazi wake na mpango wa kampuni wa kufanikisha kutekeleza malengo endelevu ya milenia.


Afisa Mazingira wa jiji la Mwanza Fanuel Kasenene akiongea katika kongamano hilo alitoa wito kwa wanafunzi kutumia fursa za mafunzo kama haya ya kuwajengea uwezo kuhakikisha maarifa wanayipatiwa wanayatekeleza kwa vitendo badala ya kutegemea elimu ya taaluma zao tu na aliipongeza kampuni ya Barrick kwa jitihada inazofanya kuibua na kukuza vipaji vya vijana wenye viwango mbalimbali vya elimu na kuwapatia ajira sambamba na kuwawezesha kujiajiri.
Afisa Rasilimali watu wa Barrick North Mara, Daniel Paul, akizungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali vya mkoani Mwanza wakati wa kongamano la kuwajengea uwezo lililoandaliwa na taasisi ya kimataifa ya vijana isiyo ya kiserikali inayohamasisha masuala ya uongozi na kujitolea kwa Jamii ya AIESEC Tanzania na kudhaminiwa na Kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick, lililofanyika jijini Mwanza katika chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino mwishoni mwa wiki.
Afisa Mazingira wa jiji la Mwanza, Fanuel Kasenene, akiongea katika kongamano hilo

Wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali vya mkoani Mwanza wakifurahia jambo, wakati wa kongamano hilo.
Wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali vya mkoani Mwanza wakifurahia jambo, wakati wa kongamano hilo.
Wanafunzi wa vyuo vikuu vya mkoani Mwanza wakiskani codes ili kuingia kwenye fursa zilizopo katika kampuni ya Barrick nchini, wakati wa kongamano hilo.
Wanafunzi wa vyuo vikuu vya mkoani Mwanza wakiskani codes ili kuingia kwenye fursa zilizopo katika kampuni ya Barrick nchini, wakati wa kongamano hilo.
Picha ya pamoja ya baadhi ya wafanyakazi wa Barrick na viongozi wa AISEC wakati wa kongamano hilo
Picha ya pamoja ya baadhi ya wanafunzi na wadau mbalimbali walioshiriki katika kongamano hilo
Share:

HOLYSMILE WAKABIDHI TUZO WADAU SHUPAVU KISHAPU




Na Sumai Salum Kishapu

Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Holysmile yenye makao yake makuu wilayani Kahama mkoani Shinyanga iliyoanzishwa na kusimamiwa na Bw. Arnold Bweichum imekabidhi tuzo 37 kwa wadau shupavu mbalimbali wilayani Kishapu mkoani humo.


Usiku huo wa tuzo umefanyika Juni 10, 2023 katika ukumbi wa Stage 2 hotel uliopo Mhunze huku mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Bw. Joseph Mkude ambapo amesema kuwa mashindano hayo yanaleta chachu yenye lengo la kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na wilaya kwa ujumla.


"Vijana hawa wamekuwa wabunifu kwa kuanzisha jambo hili nyeti sio tena vijana wanaokaa mitaani na kulalamika kuwa maisha magumu zaidi sana itawasaidia watu wote watakaopata tuzo hizi kuendelea kuwa na bidii katika utendaji kazi kwa ufanisi zaidi huku wakijua kuna watu wanatambua na kuthamini mchango wao na nipende kuwakaribisha tena Kishapu mwakani kwenye msimu wa pili wa utoaji tuzo za mdau shupavu", amesema Mkude.


Aidha Mkude ameongeza kwa kuwakaribisha wadau mbalimbali kuwekeza wilayani Kishapu hususani eneo la Maganzo kwa kuwa ni rafiki kwa uwekezaji wowote sanjari na kuwakaribisha kwenye ofisi yake kwa misaada mbalimbali ikiwemo msaada wa kisheria.


Mkurugenzi wa Holysmile Bw. Arnold Bweichum amesema lengo la utoaji tuzo hizo ni kutambua juhudi za wadau na kuchochea huduma chanya kwa jamii, kufungua fursa za uwekezaji wa kibiashara, kuhamasisha na kuhimiza shughuli za kimaendeleo afya na uchumi, kuwatambulisha watu mbalimbali na bidii wazifanyazo pamoja na kuwatambulisha ndani na nje ya maeneo yao mpaka kufikia hatua ya kimataifa kutokana na bidii zao.


"Niwashukuru sana wana Kishapu kwa kuwa shapu kuchangamkia fursa ya tuzo hizi kwa kuwa huu ni msimu wa kwanza Huku hapo kabla nilianzia Wilaya ya Kahama baadaye nikaja Shinyanga mjini na sasa tumeona tuje na Kishapu lengo letu si kuweka chuki naona ya washindani mbalimbali hapana ni kupanua mipaka ya kazi zetu na tujifunze kufanya vizuri zaidi na zaidi", ameongeza Bweichum.


Baadhi ya wadau walioudhuria kwenye sherehe za tuzo hizo wameipongeza Holysmile kwa ubunifu huo na kufikia Kishapu na imewatia moyo na kuwapa mwamko wa kujituma zaidi kwani juhudi zao zinaonekana.


Jumla ya tuzo 5 za heshima zilizotolewa ni pamoja na tuzo kwa DC, DED, halmashauri, Mwenyekiti Halmashauri ya Kishapu na (Mkamba Co.ltd pamoja na Williamson Diamond Co.Ltd) tuzo zingine ni kwa hospitali ya Jakaya Kikwete Kishapu ,RUWASA,REDESO,Kanawa sekondari,Shinyanga sekondari,Kishapu Girls,Mwadui Lutheran Sekondari,Mlimani shule ya msingi, Mkulima Bora wa mkonge(Nkinda Kulwa),mfugaji Bora, mnunuzi Bora wa nafaka,msindikaji Bora wa chakula(Kishapu Food),Kishapu oil, mfanyabiashara Bora (Nasoro Salum),NMB,Kata ya Maganzo,Stage 2 hotel,Milembe lodge, Stom palace bar.


TAARIFA KUTOKA HOLYSMILE

ASANTEEENI KISHAPU, ASANTEEE WADAU SHUPAVU 💪
__________
Tunatoa shukrani za dhati kwa Uongozi wa serikali na WadauShupavu Wilaya ya Kishapu kwa kutupokea kwa Msimu wa kwanza kwa kutupa Ushirikiano. Nichukue Fursa hii adhimu kuwashukuru kwa kuhudhuria katika Hafla ya Usiku wa Wadau Shupavu 2022/23 Kwa Hakika Mmejua kutuheshimisha Mwenyezi Mungu awaongoze kwenye kila Hatua ya Majukumu yenu kwa Hakika Ninyi Ni Wadau Shupavu, Karibuni kwenye msimu Mpya wa 2023/2024

Mh. Joseph Mkude, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu (Mgeni Rasmi) Taasisi inatoa shukrani za dhati kwako kwa kukubali kuitikia mwaliko wetu na kuwa Mgeni Rasmi katika tamasha hili, hii kwetu ni heshima kubwa sana, na hakika Mungu akubariki sana.

Pili, tunaushukuru sana uongozi wa Halmashauri ya Kishapu, hakika wametupa ushirikiano wa 100%, bila wao tusingefanikisha ufanyikaji wa tamasha hili.

Tatu, tunawashukuru sana wadhamini wote waliotuunga mkono kufanikisha tamasha hili, kuwataja wote haitoshi, lakini itoshe kusema tunawashukuru sana, na Mungu awazidishie pale walipopunguza wakawezesha tamasha hili.

Mwisho, tunawashukuru washiriki wote kwa kukubali kushiriki ushidani wa tuzo zao Pamoja na mashabiki wao wamesimama imara kuanzia hatua ya mwanzo ya mapendekezo, upigaji wa kura hadi leo siku ya tamasha wamekuja ukumbini kushuhudia na kutuunga mkono, ni upendo mkubwa sana, kishapu ahsanteni sana, ninyi ni mabingwa na kazi iendelee.
-------------------------------------------------
Tunaomba Radhi Kama Kuna Baadhi ya Changamoto zimejitokeza Kwa Kuwa huu ndio Mwanzo Kwa Kishapu Next tutaboresha Zaidi. Kwa hapa tulipo fanya Ashukuliwe Mungu🙏
Kipekee napenda kuwashukuru wadhamini wetu.
➡️ OFISI YA MKUU WA WILAYA
➡️ HALMASHAURI WILAYA YA KISHAPU
➡️NKAMBA GROUP
➡️TBL
➡️WADAU SHUPAVU WOTE

kwa kuendelea kutuunga mkono kwa kila hatua mmekuwa wadau wa muhimu sana katika kuhakikisha tunafanikisha hafla hii ya usiku wa mdau shupavu Kishapu Msimu wa kwanza
2022\2023 tunaahidi kuendeleza ushirikiano wetu. Ahsanteni sana 🙏💪
___________
Sisi ni HolySmile ✅✅🎖️
https://ift.tt/CSJDu53
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger