Tuesday, 6 June 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO JUNI 7,2023



























Share:

MIGODI YA BARRICK NORTH MARA NA BULYANHULU YAADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI KWA KUHAMASISHA JAMII KUPANDA MITI NA KUTUNZA MAZINGIRA


Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Barrick North Mara uliopo wilayani Tarime mkoani Mara wakishiriki zoezi la kupanda miti katika maeneo ya mgodi wakati wa maadhimisho ya siku ya Mazingira duniani jana.

                                                       ****
Migodi ya Barrick North Mara na Bulyanhulu iliyopo katika wilaya za Tarime na Msalala katika mikoa ya Shinyanga na Mara imeadhimisha Siku ya Mazingira Duniani 2023 kwa wafanyakazi wake kushiriki kupanda miti ya matunda na kivuli, kuhamasisha jamii kupanda miti na kufanya usafi kwenye vitongoji jirani.

Katika maadhimisho hayo, mgodi wa Barrick North Mara umetoa msaada wa miche ya miti ya matunda na kivuli ipatayo 200 na kushirikiana na jamii kuipanda katika Shule ya Sekondari ya Matongo wilayani Tarime.

Akizungumza wakati wa upandaji wa miti hiyo, Meneja Mazingira wa mgodi huo, Frank Ngoloma amesema wameelekeza shughuli hiyo katika shule hiyo mpya ili kuiboreshea uoto wa asili na mazingira kwa ujumla.

“Tumeamua kushirikiana na jamii kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani kwa kupanda miti, tumeanzia ndani ya mgodi ambapo wafanyakazi wa kila idara wameshirikiana na viongozi wao kupanda miti, na hii inaonesha commitment (uwajibikaji) ya mgodi katika kulinda mazingira”,Ngoloma.

Afisa Mtendaji wa Kata (WEO) ya Matongo, Lackson Isibhu, ameupongeza mgodi wa Barrick North Mara kwa kuthamini maadhimisho hayo na kuona umuhimu wa kushirikiana na jamii kupanda miti ili kulinda mazingira.

“Tunaushukuru mgodi wa Barrick North Mara kwa kutambua sikukuu za kitaifa na kimataifa. Kati ya taasisi au mashirika yaliyopo katika wilaya yetu ni Barrick North Mara pekee ndio wanafanya tukio kama hili la siku ya mazingira na wanakuja kusaidiana na jamii kuboresha mazingira,” amesema Lackson.

Kwa upande wake Kaimu Maneja Mahusiano ya Jamii na Mazingira wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Respicius Onesmo, alisema wameamua kuungana na Halmashauri ya Msalala kuhakikisha wanatoa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa jamii na mgodi utafadhili zoezi la kufanya usafi katika maeneo ya vijiji na vitongoji vinavyozunguka mgodi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala, Charles Fusi, aliipongeza Barrick Bulyanhulu, kwa kuunga mkono jitihada za Serikali za kuhamasisha utunzaji wa mazingira na alitoa wito kwa wananchi kuzingatia utunzaji wa mazingira na kuepuka kuzalisha taka za plastiki ambazo mbali na kuharibu mazingira unasababisha madhara mbalimbali ya Kiafya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala,Charles Fusi, akiongea wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika eneo la Kakola ambapo Mgodi wa Barrick Bulyanhulu umeshirikiana na Halmashauri hiyo kuhamasisha utunzaji wa mazingira.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Barrick Bulyahulu uliopo wilayani Msalala mkoani Shinyanga wakifanya usafi katika maeneo ya kitongoji cha Kakola wakati wa maadhimisho ya siku ya Mazingira duniani jana.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Barrick Bulyahulu uliopo wilayani Msalala mkoani Shinyanga wakifanya usafi katika maeneo ya kitongoji cha Kakola wakati wa maadhimisho ya siku ya Mazingira duniani jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala,Charles Fusi, akikabidhi zawadi ya vifaa vya usafi vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa vikundi mbalimbali vya kufanya usafi wilayani humo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani jana.
Picha ya Pamoja ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala,Charles Fusi, na baadhi ya wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu nyuma ya vifaa vya kuhifadhi taka vilivyotolewa na mgodi huo kwa ajili ya kutunzia taka katika maeneo mbalimbali kabla ya kupelekwa kwenye madampo.
Mmoja wa wafanyakazi wa mgodi wa Barrick North Mara uliopo wilayani Tarime mkoani Mara akishiriki zoezi la kupanda miti katika eneo la shule ya sekondari ya Matongo wilayani humo wakati wa maadhimisho ya siku ya Mazingira duniani jana.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Barrick North Mara uliopo wilayani Tarime mkoani Mara wakiwa na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Matongo wilayani humo baada ya kushiriki zoezi la kupanda miti katika maeneo ya shule hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya Mazingira duniani jana.
Share:

ASILIMIA 70 YA MAPATO YA VITUO VYOTE NCHINI INATEGEMEA NHIF - DKT. MOLLEL

 
Naibu Waziri wa Afya nchini Dkt.Godwin Mollel akizungumza leo June 6,2023 Bungeni Dodoma.

NA WAF - BUNGENI DODOMA 

NAIBU Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amebainisha kuwa, asilimia 70 ya Mapato ya vituo vya huduma za Afya vya Serikali pamoja na binafsi vinategemea Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya  (NHIF) ili kuendesha vituo hivyo.


Dkt. Mollel ametoa maelekezo hayo leo Juni 6, 2023 wakati akijibu swali la Mbunge wa Nkasi Kaskazini Mhe. Aida Joseph Khenani katika Bunge la kumi na mbili Mkutano wa kumi na moja kikao cha 41, Jijini Dodoma. 

Amesema, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umekuwa ni nguzo muhimu katika uboreshaji wa huduma za Afya Nchini ambapo taasisi binafsi za Afya pamoja na vituo vya huduma za Afya vya Serikali vimeonekana kutoweza kujiendesha bila uwepo wa Mfuko huo kutokana na Watanzania wenye uwezo wa kulipa fedha taslimu kuwa wachache. 

Ameendelea kusema kuwa, Serikali imefanya maboresho kwa kuongeza idadi ya dawa, vitendanishi na vifaa tiba ambapo kwa ngazi ya zahanati imeongeza kutoka aina 254 hadi 451 na kwa ngazi ya vituo vya Afya toka aina 414 hadi 828.

Sambamba na hilo, Dkt. Mollel amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya inaendelea kutoa hamasa kwa  viongozi wote ikiwemo Wabunge kuunga mkono Bima ya Afya kwa wote pindi mswada huo utapoletwa Bungeni ili wananchi wanufaike na huduma za afya katika ngazi zote kuanzia zahanati mpaka hospitali ya Taifa bila kikwazo chochote. 

Ameendelea kusema, katika kipindi ambacho Wizara inaendelea kufanya maboresho kwenye Bima ya Afya kwa wote, Wizara inaendelea kushirikiana na OR TAMISEMI na Wadau wa CHF kuboresha Bima ya Afya ya CHF ili kukidhi mahitaji ya kupata huduma bora kwa wananchi hasa wenye kipato kwa chini. 

Aidha, Dkt. Mollel amemwelekeza Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ndani ya siku tatu hospitali ya Wilaya ya Biharamuro ipate huduma za NHIF ili wananchi wa Wilaya hiyo waanze kunufaika na huduma hiyo. 

Pamoja na hayo Dkt. Mollel amesema, Dkt. Mollel amesema, Serikali inaendelea kuboresha utoaji huduma katika maeneo yote ya utoaji huduma ikiwemo upatikanaji wa dawa, vifaa na vifaa tiba pamoja na kuendelea kutoa ajira kwa Wataalamu mbalimbali wa afya

Share:

TBS YAPONGEZWA KUENDESHA MAFUNZO YA SUMUKUVU WILAYANI KONGWA

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri wilaya ya Kongwa Dk. Omari Nkulo akifungua mafunzo ya udhibiti wa sumukuvu kwenye mahindi na karanga pamoja na bidhaa zake katika kata ya Mtanana wilayani Kongwa mapema jana.

*********************

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri wilaya ya Kongwa Dk. Omari Nkulo amewataka washiriki wa mafunzo ya udhibiti wa sumukuvu kwenye mahindi na karanga pamoja na bidhaa zake katika kata ya Mtanana wilayani Kongwa kuzingatia mafunzo hayo ili kuweza kulinda afya za walaji na uchumi kwa ujumla.

“Nawasihi sana kuzingatia mafunzo haya kwani tukielewa na kutekeleza itatusaidia kulinda afya za walaji na hata kufaidika kiuchumi kwani mahindi yetu na nafaka zingine zitakua salama kuuza katika soko la ndani na nje ya nchi “alisema Dk.Nkulo

Vilevile Dk.Nkulo alishukuru Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa mafunzo hayo na kutoa wito kwa washiriki kuwa mabalozi wa sumukuvu kwa wengine.

Dk.Nkulo ametoa wito huo kwa washiriki wa mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Shirika la viwango Tanzania (TBS)kupitia mradi wa kudhibiti sumukuvu Tanzania (TANIPAC).

Mafunzo hayo yanayoendelea wilayani Kongwa yameshafanyika wilayani Kiteto na yanategemewa kufanyika katika wilaya ya Gairo na Kilosa.
Share:

𝗨𝗝𝗔𝗭𝗔𝗝𝗜 𝗡𝗔 𝗨𝗧𝗘𝗡𝗚𝗘𝗡𝗘𝗭𝗔𝗝𝗜 𝗪𝗔 𝗗𝗢𝗗𝗢𝗦𝗢 𝗦𝗔𝗦𝗔 𝗡𝗜 𝗞𝗜𝗗𝗜𝗝𝗜𝗧𝗔𝗟𝗜


Na Mussa Enock,DODOMA.

Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) imefanikiwa kutengeneza mfumo shirikishi wa kidijitali wenye usalama na gharama nafuu unaomuwezesha mwananchi au taasisi kutengeneza na kujaza dodoso, kupata tathmini pamoja na takwimu za dodoso kwa njia ya mtandao. 

Hayo yalibainishwa na Meneja wa Kituo cha Utafiti na Ubunifu na Uendelezaji wa Serikali Mtandao (eGovRIDC) cha e-GA, Mhandisi Dkt. Jaha Mvulla alipofanya mazungumzo na mwandishi wetu ofisini kwake Jijini Dodoma.

“Mamlaka tuliamua kutengeneza mfumo huu ili kuwepo na mfumo shirikishi na salama wa kuhifadhi takwimu zinazotokana na madodoso, kuzuia urudufu wa utengenezaji wa madodoso, pamoja na kupunguza gharama kutoka kwenye mifumo ya dodoso inayotumia leseni” alisema Dkt. Jaha.

Alifafanua kuwa, mfumo huo umegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo ni dodoso LITE na dodoso PRO ambapo, katika utengenezaji wa maswali na upatikanaji wa takwimu katika dodoso LITE umefanywa kuwa urahisi zaidi ili kumrahisishia mtumiaji katika kujaza au kutengeneza dodoso.

Walengwa wakuu wa mfumo huu ni Taasisi za Umma na wananchi wenye uhitaji wa kutengeneza madodoso ili waweze kupata takwimu au majibu sahihi ya dodoso husika, alisema Jaha.

“Mfumo huu una uwezo wa kuhifadhi data pia ni salama kwakuwa umejengwa na wataalamu wazalendo wa ndani na unawaruhusu watumishi kufanya uchambuzi, kuhifadhi na kupata takwimu za madodoso ya taasisi yanayotengenezwa, pia taasisi au mtu binafsi anaweza kutengeneza dodoso muda wowote na mahali popote kwa jia ya mtandao” alisema Jaha.

Aidha, mtumishi anaweza kutengeneza dodoso la taasisi na kugawa namba ya dodoso na nywila kwa wahusika tu ili waweze kujaza na pia, mfumo unaruhusu na kuziwezesha taasisi kutengeneza maswali katika fomati mbalimbali na kutumia njia ya program ya simu au Kivinjari katika kujaza dodoso.

Kwa sasa Mfumo huu unapatikana bila gharama yoyote kupitia https://ift.tt/gc6MYB5, ili taasisi iweze kuunganishwa na kutumia mfumo huu, taasisi husika inapaswa kuwasiliana na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) kupitia Dawati la Msaada https://ift.tt/dHmws9f.

Share:

SERIKALI YA ANZA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAJI NDANI YA JIMBO LA KWELA





Serikali imeanza utekelezaji wa Miradi ya Maji ya Mkunda group,Kaoze group pamoja na Ilemba ambayo inatarajiwa kukamilika katika Mwaka wa fedha 2023/2024.


Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Maji Meryprisca Mahundi Juni 6/2023 wakati akijibu Maswali ya Mbunge wa jimbo la kwela Deus Sangu aliyetaka kujua "Je, lini Serikali itapeleka fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji katika maeneo ya Mkunda Kaengesa, Kaoze Group na Ilemba"


Mahundi amesema wizara imeshajipanga kwa Mwaka ujao wa fedha kwenda kutekeleza ili kuwaondolea adha wanayoipata wananchi


"Laela na Mpui Miradi wa Mau unaendelea kufanya kazi kwa maana ya taratibu zinaendelea kukamilishwa, na tayari kwa pale Laela utaratibu umekamilika na mwezi huu juni mwishoni tutaanza kutekeleza", amesema Naibu Waziri Mahundi.
Share:

MCHUNGAJI MATATANI KWA KUMBAKA MUUMINI WA KANISA LAKE


Mchungaji mmoja kutoka katika Kaunti ya Embu nchini Kenya amefikishwa mahakamani Jumatatu Juni 5,2023 kwa tuhuma za kumbaka muumini wa kanisa lake.

Pasta Benson Mwaniki Njuki wa Kanisa la Full Gospel Karurina, ameshtakiwa kwa kumbaka binti mwenye umri wa miaka 22, mnamo Juni 1,2023  katika Kijiji cha Karurina, Embu Magharibi.

Njuki alishtakiwa kwa kuingiza kiwiliwili chake ndani ya mwanamke huyo na pia kumshika sehemu za siri bila idhini yake.

 Kulingana na stakabadhi za mahakama, inasemekana kuwa mwanamke huyo alikuwa katika kikao cha maombi katika kanisa la Njuki, akiwa amepiga magoti, wakati mchungaji huyo alimbaka.

Mahakama ilielezwa kwamba wakati wote huo, mchungaji huyo alikuwa amevaa mavazi yake rasmi ya kanisa.

 Jaribio lake la kupiga mayowe lilisitishwa baada ya mshtakiwa kumshinda nguvu na kumfunga mdomo. 

Mwanamke huyo alimsimulia mama yake tukio hilo na alipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Embu Level V ambapo ilithibitishwa Njuki alimuingiza kiwiliwili chake na fomu ya P3 na fomu ya Huduma ya baada ya Kumbaka (PRC) zilijazwa. 

Tukio hilo liliripotiwa katika Kituo cha Polisi cha Itabua, ambapo mchungaji huyo alikamatwa. 

Njuki alikana mashtaka hayo alipojitokeza mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi wa Embu, Robert Gitau.

 Aliachiliwa kwa dhamana ya KSh.100,000 na mdhamini mwenye kiasi sawa au dhamana ya pesa taslimu ya KSh.50,000. 

Kesi hiyo itatajwa tena mnamo Juni 11,2023.

Chanzo - Tuko News
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JUNI 6,2023



































Share:

Monday, 5 June 2023

NEMC YAIPONGEZA HOSPITALI YA MUHIMBILI KUENDELEA NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA


KATIKA kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limekabidhi vifaa vya kutenganishia taka katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo Juni 5,2023 mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo, Meneja wa Uzingatiaji wa Sheria na Ufuatiliaji (NEMC), Bw. Hamadi Taimur ameipongeza hospitali hiyo kwa kuendelea kutunza mazingira na kuzitaka taasisi nyingine zikiwemo hospitali kuiga mfano huo.

“Ukiangalia hapa Muhimbili mazingira yake ni ya kijani hakuna taka zinazozagaa na hii imewezekana kutokana na hospitali kuwa na timu inayosimamia usafi wa mazingira ya hospitali, kwakweli hili ni jambo la kuigwa na tunawaasa wengine waje wajifunze hapa” amefafanua Bw. Taimur.

Bw. Taimur ameongeza kuwa NEMC inaamini kuwa vifaa vilivyotolewa leo vitasaidia kuendelea kuboresha shughuli za usafi na utunzaji wa mazingira wa maeneo mbalimbali ya hospitali kwa kuwa hospitali inazalisha taka za aina mbalimbali ikiwemo taka hatarishi.

Akipokea msaada huo msaada huo Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi na Matengenezo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Bi. Domiana John kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji MNH ameishukuru NEMC kwa msaada huo na kuongeza kuwa vifaa hivyo vitasaidia kuendelea kuimarisha shughuli za usafi hospitalini hapa.

Bi. Domiana amesema kipaumbele cha hospitali ni usafi na usalama wa wadau mbalimbali wanaoingia na kutoka ndio maana imeendelea kuweka mazingira katika hali ya usafi na kuepuka kuzagaa hovyo kwa taka kwa lengo la kuepuka magonjwa mbalimbali.


Share:

AIBUKA MSHINDI WA TSH 2,183,703/= KWA 250/=



 Maisha ni mipango bila ya kuweka malengo ni sawa na kusafiri baharini bila kuwa na dira, hutojua unaelekea wapi. Meridianbet wanakupa tochi ya kumulika maisha yako kama ambavyo mfalme mpya wa beti na kitochi alivyoangaza maisha yake kwa dau la Tsh 250/= kisha kujishindia mamilioni ya pesa.

 

Huyu ni mwamba sana aliyeibuka Milionea kwa siku moja tu, ambayo aliamua kubashiri na Meridianbet kupitia beti na kitochi *149*10# kisha aliweka dau la Tsh 250 na kuanza kusikilizia maokoto (pesa) kudondoka.

 

Ili kujiweka kwenye nafasi kubwa ya ushindi Mfalme mpya wa kubashiri soka aliamua kuweka machaguo yenye odds kubwa, huku kila timu akiipa chaguo lake ambalo aliona linaweza kuzalisha Tsh 250/= na kuwa mamilioni.

 

Mabibi na Mabwana hatimaye Meridianbet wamemtambulisha kwenye familia ya mabingwa, mshindi mpya wa Tsh Milioni 2,183,703/= na wewe una nafasi ya kuwa mfalme ukibashiri soka na kucheza kasino ya mtandaoni.

 

Machaguo Gani Aliweka?

 

Mfalme huyu alitengeneza tiketi yenye timu 11 za uhakika, huku akichagua machaguo ya aina tatu kama vile sare kipindi cha kwanza, ushindi kwa timu ya ugenini, ushindi kwa timu ya nyumbani na sare kipindi cha pili.

 

Kati ya timu 11 timu saba alizipa chaguo la sare kwenye kipindi cha kwanza, huku nne zilizobaki akitoa ushindi kwa timu ya ugenini na nyumbani.

 

NB: Ligi zimeisha lakini usiwaze wajanja wanatengeneza hela kupitia kasino ya mtandaoni, jiunge meridianbet kama bado na upate mizunguko ya bure kucheza kasino ya mtandaoni, jiunge sasa.

 

Share:

AJALI YA COASTER, LORI YAUA NA KUJERUHI MIKUMI

Watu watano wanahofiwa kufariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari dogo aina ya Coaster iliyokuwa ikitokea mkoani Mbeya ikigongana na lori katika eneo la Iyovi Tarafa ya Mikumi mkoani Morogoro.

Chanzo - Mwananchi
Share:

WAFANYAKAZI BARRICK BULYANHULU WAPONGEZWA KWA KUFANIKISHA USHINDI WA JUMLA TUZO ZA AFYA NA USALAMA (OHS) 2023


Meneja Mkuu wa Barrick Bulyanhulu,Cheick Sangare akiongea katika hafla hiyo.
Meneja wa Usalama katika mgodi wa Bulyanhulu,Duncan Mclaren akiongea katika hafla hiyo.
Mfanyakazi wa Barrick Bulyanhulu, Hassan Kalegeya akipokea cheti kutoka kwa Meneja Mkuu waMgodi,Cheick Sangare (kushoto)
WalterBlanca Nshimah akipokea cheti
Waziri Kazuvi akipokea cheti
Flora Zakaria akipokea cheti
Emmanuel Mwakanyopole akipokea cheti
Charles Hiza akipokea cheti
Azaely Kitange akipokea cheti
Wafanyakazi wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu walioshiriki maonesho ya OSHA na kufanikisha ushindi wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja Usalama wa Mgodi wa mgodi huo Duncan Mclaren wakati wa hafla hiyo.

****

Mgodi wa Barrick Bulyanhulu umewapongeza wafanyakazi wake walioshiriki katika maonyesho ya OSHA 2023 yaliyofanyika mkoani Morogoro, ambapo ulifanikiwa kushinda tuzo kubwa ya mshindi wa juu wa jumla pia ilinyakua tuzo ya uandaaji Ripoti Bora ya Tathmini ya Hatari katika uchimbaji madini na mshindi Bora wa tuzo ya Usalama na afya (OHS) katika sekta ya madini.

Hafla ya kuwapongeza wafanyakazi hao ilifanyika katika mgodi wa Bulyanhulu ambapo walitunukiwa vyeti na Meneja Mkuu wa mgodi huo, Cheick Sangare,ambaye alisema kampuni itaendelea kuhakikisha sera yake ya usalama inatekelezwa kwa vitendo.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger