Friday, 12 May 2023

WAZIRI MCHENGERWA ATEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MKUU, AFIKA ENEO LA TUKIO, ATOA POLE NA MAAGIZO MAZITO KWA WATENDAJI.



Na John Mapepele

Agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa alilolitoa jana bungeni la kutaka Waziri wa Maliasili na Utalii na Watendaji wa Wizara hiyo kufika mara moja kijiji cha Mwanavala wilayani Mbarali wakishirikiana na Uongozi wa Mkoa wa Mbeya kutatua migogoro baina ya Hifadhi ya Ruaha na wananchi hao limekamilika leo Mei12,2023 baada ya kufika.

Akiongea kwenye kikao na wananchi hao leo mei 12, 2023 amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuwachukulia hatua za kinidhamu maafisa wote wa Serikali walioshiriki kwenye migogoro huo.
Hata hivyo amewaomba wananchi kuzingatia sheria ambapo amewataka kutovamia maeneo ya makazi ambapo katika mgogoro huo baadhi ya wananchi walikutwa kilomita kumi ndani ya Hifadhi ndipo walipoanza kutolewa kwa nguvu na wahifadhi.

Mhe. Mchengerwa ametoa mkono wa pole wa shilingi milioni moja kwa wananchi watano kila moja kama kifuta machozi kutokana na ugomvi wa wahifadhi na wananchi hao. Hata hivyo hakuna tukio lolote la kifo.

Amefafanua kuwa tatizo la mipaka katika Hifadhi hiyo linakwenda kumalizika ambapo amesema jumatatu anasaini GN mpya ya mpaka wa eneo hilo.
Hata hivyo imethibitika kuwa madai ya kwamba ng'ombe 250 walishikiliwa siyo ya kweli kwa kuwa wananchi wote katika mkutano wamekubali kuwa hakuna ng'ombe hata moja aliyeshikiliwa na Hifadhi

Aidha amesema mipaka ya Hifadhi hiyo iliwekwa mwaka 1910 wakati Hifadhi hiyo ikijulikana kama Saba Game Reserve na mwaka 1946 ikijulikana kama Hifadhi ya Rungwe na hatimaye mwaka 1964 kama Hifadhi ya Ruaha hadi sasa.

Ameongeza kuwa dhamira ya Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuona kuwa kero zote katika maeneo ya Hifadhi zinatatuliwa kwa amani na upendo.

"Ibara ya 68 ya CCM inasisitiza uhifadhi wa raslimali hivyo sisi sote tunapaswa kushirikiana kwa pamoja tuhifadhi kwa faida ya kizazi cha sasa na baadaye" ameongeza Mhe. Mchengerwa
Katika kikao hicho, bwana Ngalao Laini ameiomba Serikali kuangalia namna bora ya kuwahamisha wananchi na kuwatengea maeneo bora ya makazi pindi inapoamuliwa kuwaondoa katika Hifadhi.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambaye pia aliambatana katika ziara hiyo na Kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa, na wilaya ya Mabarali na viongozi wa CCM wa wilaya hiyo aliwaambia wananchi katika mkutano huo kuwa Serikali itahakikisha kuwa wananchi wote wanatendewa haki ikiwa ni pamoja na kufanya tathimini za makazi na kuwalipa fidia stahiki.

Share:

JUMUIYA YA WAZAZI CCM SHINYANGA MJINI YATOA MSAADA KITUO CHA KULELEA WATOTO CHA BROTHER OF CHARITY

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko (aliyevaa kofia kushoto) na viongozi mbalimbali wakikabidhi chakula katika kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga


Na Kadama Malunde -Malunde 1 blog
Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini imetoa msaada Chakula kwa watoto wenye ulemavu wa viungo na magonjwa ya akili wanaolelewa katika Kituo cha Brothers of Charity kilichopo mtaa wa Majengo kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga.


Akizungumza wakati wa kukabidhi vyakula hivyo leo Ijumaa Mei 12,2023, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko amesema CCM inatambua makundi ya watu wenye uhitaji ndiyo maana imewatembelea watoto hao na kuwapatia msaada.


“Tupo kwenye ziara ya kamati ya utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga Mjini kutembelea kata mbalimbali kwa ajili kukagua uhai wa Jumuiya, kuingiza wanachama wapya na kuhamasisha kuanzisha miradi ya kiuchumi na tumekuja hapa kuwatembelea watoto wetu na kuwapatia hiki kidogo tulichokuja nacho na tunaahidi kuendelea kufika hapa na tunaomba wadau wengine na wananchi wajitokeze kusaidia watoto hawa”,amesema Mrindoko.


“Tunawashukuru walezi wa watoto hawa. Hii kazi mnayofanya kulea na kuwafundisha watoto hawa mambo mbalimbali kwakweli kazi hii mnayofanya ni kazi ya kitume. Tunawashukuru na tunawapongeza sana. Nimeambiwa watoto hawa walikuwa hawajui chochote lakini mmewafundisha jinsi ya kujitambua na sasa wanafanya wao wenyewe. Asanteni sana nasi tunaendelea kukitangaza kituo hiki lakini pia tutaendelea kufika hapa ili tushirikiane kutatua changamoto zinazojitokeza”,amesema.



Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Doris Yotham Kibabi amesema Jumuiya hiyo ina jukumu la malezi ndiyo maana watembelea kituo hicho cha watoto na kuwapatia chakula ikiwemo unga wa sembe, mchele, mafuta ya kupikia, chumvi, juisi na biskuti.


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kituo cha Brother of Charity, Brother George Paul Rice amekishukuru Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutembelea kituo hicho ambacho sasa kina watoto zaidi ya 20 na kuwapatia msaada wa chakula.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko  akizungumza kwenye kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga leo Ijumaa Mei 12,2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko  akizungumza kwenye kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga leo Ijumaa Mei 12,2023.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Doris Yotham Kibabi akizungumza kwenye kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga leo Ijumaa Mei 12,2023.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Doris Yotham Kibabi akizungumza kwenye kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga leo Ijumaa Mei 12,2023.
Mkurugenzi wa Kituo cha Brother of Charity, Brother George Paul Rice wakati Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga Mjini ikitembelea kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga
Mkurugenzi Msaidizi wa Kituo cha Brother of Charity, Brother Francis Bega wakati Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga Mjini ikitembelea kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga
Sehemu ya chakula kilichotolewa na Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga Mjini katika kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko (aliyevaa kofia kushoto) na viongozi mbalimbali wakikabidhi chakula katika kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko (aliyevaa kofia kushoto) na viongozi mbalimbali wakikabidhi chakula katika kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko (aliyevaa kofia kushoto) na viongozi mbalimbali wakikabidhi chakula katika kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga
Zoezi la kukabidhi chakula katika kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga likiendelea
Zoezi la kukabidhi chakula katika kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga likiendelea
Zoezi la kukabidhi chakula katika kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga likiendelea
Zoezi la kukabidhi chakula katika kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga likiendelea
Muonekano bango katika kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

KATAMBI:TUTAENDELEA KUWACHUKULIA HATUA WAAJIRI WASIOWAPA MIKATABA WAFANYAKAZI


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi akijibu swali Bungeni leo Mei 12, 2023, jijini Dodoma.




Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akijadili jambo na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi Bungeni jijini Dodoma leo tarehe 12 Mei, 2023.

Na.Mwandishi Wetu-DODOMA

OFISI ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imeanza kufanya ukaguzi na kuwachukulia hatua waajiri wanaokwepa kuwapa mikataba wafanyakazi kwa kuwatumia kama vibarua ili kunyonya haki zao.

Naibu Waziri wa Ofisi hiyo, Mhe. Patrobas Katambi ameyasema hayo bungeni leo Mei 12, 2023 alipokuwa akijibu maswali ya nyongeza ya Mbunge wa Viti maalum (Chadema), Mhe. Sophia Mwakagenda. Katika swali lake, Mbunge huyo amehoji serikali inatoa kauli gani kwa baadhi ya viwanda kwenye Mkoa wa Pwani maeneo ya Mbagala na Mkuranga vinavyowatumikisha wafanyakazi kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa 11 jioni na kuwaa ujira wa Sh.4,000 kwa siku.

Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri Katambi amesema serikali imebaini wapo waajiri wanakwepa kuwapa mikataba ya kazi wafanyakazi ili kuendelea kuwaita vibarua na kuendelea kufanya kazi kwa muda mrefu ni unyonyaji mkubwa.

“Ofisi ya Waziri Mkuu imeanza kuchukua hatua na tunafanya kaguzi kujua historia ya wafanyakazi wamefanya kazi kwa kipindi gani na aina ya kazi anayoifanya ili kuwaingiza kwenye mifumo ya kuwa na mikataba ya kazi ili haki zao zilindwe kwa mujibu wa sheria,”amesema.

Naibu Waziri huyo amesema katika sheria ya ajira na mahusiano kazini inaeleza moja ya mambo ni kukubaliana yawe kimkataba na yaandikwe na kuwekwa wazi na kitendo cha waajiri kutolipa mishahara au masilahi yao ni kuvunja sheria hiyo.

Katika swali la msingi, Mbunge huyo amehoji lini Serikali itahakikisha watanzania wanaofanya kazi kwenye kampuni za Kichina wanalipwa vizuri kwa mujibu wa sheria.

Akijibu swali hilo, Katambi amesema serikali imeendelea kusimamia utekelezaji wa Sheria za Kazi ili kulinda haki za wafanyakazi kupitia Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara katika Sekta Binafsi imefanya utafiti na kuboresha kima cha chini cha mshahara kwa sekta binafsi na tayari viwango vimetangazwa.

Amelihakikishia bunge kuwa ofisi hiyo itahakikisha waajiri wanatekeleza ipasavyo viwango vya mishahara vilivyotangazwa kwa kufanya kaguzi za mara kwa mara katika maeneo ya kazi na kutoa elimu kwa waajiri na wafanyakazi ili kujenga uelewa wao katika kutekeleza Sheria za kazi.
Share:

ASHINDWA KUVUMILIA AFANYA TAFRIJA BAADA YA KUPONA UGONJWA WA MOYO

Nilipoambiwa kuwa maisha yangu yapo hatarini na siku zangu za kuishi ziko ukingoni ndipo nilipoanza kufanya kila jitihada iliyoko ndani ya uwezo wangu kusudi nijinasue kwenye ugonjwa huo mbaya wa moyo.

Ugonjwa huu ndio ulinikutanisha na bingwa wa mabingwa daktari BAKONGWA mwenye nambari za whatsapp +243990627777. Dalili za ugonjwa wa moyo nilianza kuziona mapema nilipopata dalili za maumivu ya kifua, kifua kubana na muda mwingine kusindwa kabisa kupumua na kuzidiwa hata kuwekewa mirija ya upumuaji.

Nilijithibitishia haya nilipo kwenda kufanyiwa vipimo Hospitali ya taifa Muhimbili na ndio hao waliosema kuwa hakuna tiba labda nipambane sana kubadilisha moyo tena itanibidi nisafiri kwenye nchi za watu huko ili kusudi hili litimie.Kuhofia kufariki mimi nikajichanga na kufanya mawasiliano ya ndugu zangu waliopo huko nchi za ughaibuni.

Nilipowapa majibu na vipimo vya afya yangu walisema kupata mtu ambaye anaweza kujitolea moyo wanibadilishie nizoezi gumu sana, kwani kundi langu la damu lilikuwa ni herufi ‘O’.

Nilipouliza kuhusu gharama wao walisema gharama ambazo kwangu hazikuwa gharama za juu , nikaona nazikidhi lakini wakanikumbusha upasuai huwo hauna uhakika kama mimi nitatoka mzima kwenye chumba cha upasuaji.Hilo nalo likanitia wazimu zaidi ofu ya mimi kufariki kabla sijafanya makubwa ikaongezeka ikawa maradufu sasa.

Ushauri nilioambulia kutoka kwao ni kuwa nipunguze vyakula vya mafuta na nijaribu kufanya mazoezi ya mwili angalau yatanisaidia kurudisha afya yangu kama vile ambavyo ilikuwa mwanzoni japo hii haikumaanisha kwamba nitapona.

Miaka minne sasa nikiwa najinyima na kula vyakula vya shauri na kufanya yale waliyosema --- yaani niliishi kwa shida maisha yasiyo na furaha imani ya mimi kupona haikuwepo tena mbele yangu.

Sasa nikaanza kufikiria kuwa ninafariki hata mtoto sijaacha hili nalo lilinitia uchungu zaidi, jioni moja nikiwa kwenye dimbwi la mawazo sana nisijuwe hili wala lile nilitembelewa na bosi wangu nyumbani akija kufahamu yali ya afya yangu kwakuwa sasa hata kazini sikuwa mhudhuriaji mzuri kwa sababu za igonjwa unaonisumbuwa.

Tuliongea sana nikamueleza hali ngumu na shida ninazozipitia kuhusu ugonjwa wangu nay eye akaniuliza, Umewahi badili mtazamo wa tiba ? haraka harala nikajibu ndiyo m naye akarudia akasema sasa jaribu kumuona daktari bakongwa akaniandikia tovuti za huyo daktari https://bakongwadoctors.com na kuniacha humo ndani tukaagana kwa ishara za mikono sikumsindikiza kwa kuhofia kijua kikali na afya yangu havipatani.

Nilipopata wasaa tu wa kuwa peke yangu niliingia kwenye hizo tovuti zake kisha nika nakiri nambari zake na kumtafuta kujuwa ni namna gani atanipa msaada kwenye shida yangu.Daktari alinisikiliza na kunipa dawa ya kunywa jwa muda wa siku mbili kisha akaniambia nitakapo maliza dawa nikapime hospitalini kujihakikishia mwenyewe.

Nilifanya hivyo na kwa kujiaminisha nilirudi palepale hospitali ya taifa hakika hata madaktari walionipima walishangazwa na majibu ya vipimo hivyo nilikuwa mzima hakukuwa na shida yoyote tena kwangu, ndipo nilipoamini kuwa kwa daktari bakongwa hakuna kubwa yote kwake ni madogo tu , asante sana daktari kwa msaada sasa ninadunda tena upya na nimeandaliwa tafrija siku ya kurejea kazini.


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA MEI 12,2023



 



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger