Wednesday, 10 May 2023

SHIRIKA LA FOKUS KUENDELEA KUFADHILI SHUGHULI ZA SHIRIKA LA KIVULINI

Shirika la Maendeleo ya Wanawake (Forum for Women and Development- FOKUS) la nchini Norway limeahidi kuendelea kufadhili shughuli zinazotekelezwa na shirika la kutetea haki za watoto na wanawake KIVULINI lililopo mkoani Mwanza.

Mshauri wa Programu ya kuwawezesha wanawake kutoka shirika la FOKUS, Joar Svanemyr aliyasema hayo Mei 09, 2023 wakati akishuhudia namna shirika la KIVULINI limekuwa likishirikisha makundi mbalimbali kutoa elimu ya kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia hususani kwa watoto na wanawake katika Wilaya ya Magu.

Svanemyr alisema mbinu zinazotumika na shirika la KIVULINI kuwakusanya wananchi kwenye makongamano mbalimbali ya kuelimisha jamii ikiwemo kuwatumia wanaharakati ngazi ya jamii, bodaboda, wasanii wa ngoma za asili pamoja na mashabiki wa timu za soka za Simba SC na Yanga SC zimekuwa kivutio kikubwa kwake kwani zimesaidia kuleta mabadiliko wilayani Magu.

Akizindua matawi ya timu za Simba SC na Yanga SC katika Kijiji cha Nyang’hanga Kata ya Sukuma wilayani Magu na kukabidhi vyeti kutoka shirika la KIVULINI, Svanemyr alivutiwa na hamasa ya mashabiki wa timu hizo na jumbe walizoziandika kwenye matawi hayo na kuahidi kwamba shirika la FOKUS litaongeza ufhadhili zaidi ili elimu ya kutokomeza ukatili wa kijinsia ifike katika Kata zilizobaki wilayani Magu kwani kwa sasa ni Kata nne kati ya 25 ndizo zimefikiwa.

Naye Mkurugenzi Mtendaji shirika la KIVULINI, Yassin Ally alisema shirika hilo limekuwa likishirikiana na Serikali pamoja na makundi mbalimbali katika jamii kutoa elimu ya kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuhamasisha maendeleo ambapo hadi sasa zaidi ya mashabiki 400 wa Simba na Yanga wanasaidia kufikisha elimu hiyo nyumba kwa nyumba.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Magu, Lilian Michael alisema vitendo vya ukatili vikitokomezwa katika jamii itasaidia m wenye afya bora, elimu bora na makazi bora ambapo kwa pamoja inasaidia jamii pia kuwa na uchumi imara hivyo malengo ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo kutosomesha watoto wa kike, vipigo na ndoa za utotoni lazima vitokomezwe.

Nao baadhi ya wanaharakati na mashabiki wa timu za Simba na Yanga wilayani Magu wakiwemo Grace John, Samwel Kaswahili, Veronica Mahingu na Amos Sayi walisema hapo awali kulikuwa na matukio ya vitendo vya ukatili wa kijinsia lakini baada ya kuanza kupita kaya kwa kaya kuelimisha jamii, matukio hayo yamepungua na sasa wanafamilia wanashirikiana katika shughuli za maendeleo katika Kata nne za Sukuma, Jinjimili, Kabila na Nyang’hanga ambazo shirika la KIVULINI linatekeleza mradi wa kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG 
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally (kushoto) akitafsiri hotuba ya Mshauri wa Programu ya Wanawake kutoka Shirika la FOKUS la nchini Norway, Joar Svanemyr (kulia) aliyefika Magu mkoani Mwanza kushuhudia mbinu mbalimbali zinazotumika kutoa elimu ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii.
Mshauri wa Programu ya Wanawake kutoka Shirika la FOKUS la nchini Norway, Joar Svanemyr (kulia) akikabidhi cheti kwa mashabiki wa timu ya Simba SC tawi la Nyang'hanga wilayani Magu kilichotolewa na Shirika la KIVULINI ili kutambua mchango wao wa kuelimisha jamii kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Mshauri wa Programu ya Wanawake kutoka Shirika la FOKUS la nchini Norway, Joar Svanemyr (wa pili kulia) akikabidhi cheti kwa mashabiki wa timu ya Yanga SC tawi la Nyang'hanga wilayani Magu kilichotolewa na Shirika la KIVULINI ili kutambua mchango wao wa kuelimisha jamii kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Picha ya pamoja na mashabiki wa timu ya Yanga SC tawi la Nyang'hanga wilayani Magu baada ya Mshauri wa Programu ya Wanawake kutoka Shirika la FOKUS la nchini Norway, Joar Svanemyr kuzindua rasmi tawi hilo.
Picha ya pamoja na mashabiki wa timu ya Simba SC tawi la Nyang'hanga wilayani Magu baada ya Mshauri wa Programu ya Wanawake kutoka Shirika la FOKUS la nchini Norway, Joar Svanemyr kuzindua rasmi tawi hilo.
Mshauri wa Programu ya Wanawake kutoka Shirika la FOKUS la nchini Norway, Joar Svanemyr akifurahia burudani na wakati wa Magu.
Mshauri wa Programu ya Wanawake kutoka Shirika la FOKUS la nchini Norway, Joar Svanemyr na wanaharakati ngazi ya jamii wilayani Magu wanaosaidia kutoa elimu ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii.
Mshauri wa Programu ya Wanawake kutoka Shirika la FOKUS la nchini Norway- Joar Svanemyr (katika), Mkugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI- Yassin Ally (kushoto) na Diwani Kata ya Sukuma ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Magu- Faustine Makingi (kulia).
Mashabiki wa Yanga SC tawi la Nyang'hanga Magu wakifurahia burudani.
Kikundi cha wanawake kikitoa burudani yenye ujumbe wa kuhamasisha jamii kuacha vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Mashabiki wa Simba SC tawi la Nyang'hanga Magu wakieleza namna walivyosaidia jamii kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia. 
Mashabiki wa timu ya Yanga SC tawi la Nyang'hanga Magu wakieleza namna wanavyohamasiwha jamii kuacha vitendo vya ukatili wa kijinsia na kujikita kwenye shughuli za maendeleo.
Wanaharakati ngazi ya jamii wakieleza namna wanavyoelimisha wananchi kuacha vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Magu, Lilian Michael akihamasisha jamii kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia hatua itakayosaidia kufikia lengo la Millenium kwa jamii kuwa na afya bora, elimu, makazi bora na uchumi imara.
Tazama Video hapa chini

Share:

ASHANGAZWA NA UFAULU WA MWANAYE BAADA KUKUTANA NA BAKONGWA

Sikuamini nilipoambiwa kuwa mwanangu amefaulu mtihani wake wa kidato cha nne mpaka nilipojihakikishia mwenyewe kwa kuangalia matokeo na kumuulizia mwalimu mkuu wake shuleni pale alipokuwa anasoma. Ninamfahamu mwanangu vizuri sio mtu wa darasani amekuwa anajihusisha sana na vibarua mbalimbali kusudi asaidie familia yake kipindi ambacho wanafunzi wenzake wakiwa darasani.


Hili lilikuja baada ya ajari iliyotokea na baba yake akafariki papo hapo kwenye gari la abiria la kuelekea dar es salaam ‘NBS’ilimbidi aanze kutunza familia yetu, yeye kama baba.Ikafika kipindi ikawa ngumu kwake kuhudhuria masomo ikawa anahudhuria mara mbili kwa wiki.

Nilianza kuona mwenendo wa masomo yake sio mzuri kwenye matokeo yake ya muhula wa mwisho wa kuingia kidato cha nne, Alishika nafasi ya pili kutoka mwisho kila nilipo jaribu kusema naye hakuonesha changamoto yoyote katika masomo yake alizijuwa shida za nyumbani kwetu na akazipa kipaumbele kikubwa.

Ninafahamu kuwa nguzo ya maisha mazuri kwanza ni shule nilifanya kila la kufanya mwanangu asome ili aje kutukomboa sisi familia yake, nikapalangana kila kona nikawa na madeni kila mahali kwenye vikundi vyetu vya akina mama nikamtafutia tuisheni lakini wala hakuw amhudhuriaji mzuri kwa sababu za vibarua vyake na kila alipo hudhuria hakuwa makini, nilimpima kwenye mtihani wake wa katikati ya mwaka wa kidato cha nne na kugunduwa hakuwa amepiga hatuwa yoyote ile alishika nafasi ya mwisho kabisa wakati huu.

Hakuna mzazi anaye furahi kumuona mwanaye anaharibu maisha yake ili atunzwe yeye, au mwanaye anaharibikiwa ikiwa mzazi bado yuko hai, kwa nikaamuwa kufanya maombi ya siku tatu na kufunga ili mwanangu abadilike lakini bado hata mtihani wake wa pre-nation hakufanya vizuri alipata daraja la nne jirani na mwisho kabisa tena.

Niliamua kumshirikisha wifi yhangu, shangazi yake kwa kuwa ndiye alikuwa ndugu wa pekee kwenye ukoo wa marehemu baba yake aliyeko jirani na sisi, akaniambia kuwa hata yeye mwanaye alimaliza elimu ya chuo kikuu kwa msaada wa daktari BAKONGWA akanatia nguvu akanipa nambari za whatsapp za daktari +243990627777.

Nilipomtafuta daktari alitupa dawa ya kumuongezea mwanangu kumbukumbu na kumfanya ashike vitu kwa haraka zaidi, alikaa kwenye mtihani wake akiwa ametumia dawa ile kwa siku mbili tu, sikuamini lakini matokeo yalipotoka nilishangaa mimi na walimu wake wote kwa ufaulu wa daraja la pili alilopata ulio mruhusu aendelee na masomo ya ngazi ya juu zaidi, ,asante sana daktari kwa msaada ulionipatia kwa mwanangu.
Share:

FCS YAJA NA MRADI WA 'URAIA WETU' KUCHAGIZA MCHAKATO KATIBA MPYA



Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Bw. Francis Kiwanga (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa “Uraia Wetu” kwaajili ya kukuza uwezo wa AZAKi na kuongeza hamasa na wigo wa ushiriki wa wananchi katika machakato wa katiba mpya. Hafla hiyo imefanyika leo Mei 9, 2023 Jijini Dar es Salaam.

Meneja programu wa Tanganyika Law Society (TLS) Mackphason Mshana akizungumza katika hafla hiyo kuelezea ushiriki wao katika mchakato wa katiba mpya kupitia mradi huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Bw. Francis Kiwanga (kushoto) akimshuhudia Mkurugenzi wa Tanzania Association of NGOs Adamson Nsimba (kulia) akisaini mkataba wa utekelezaji wa Mradi huo, katika hafla fupi iliyofanyika leo Mei 9, 2023 Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Bw. Francis Kiwanga (kushoto) katika makabiadhiano ya Mkataba wa utekelezaji wa Mradi huo na Meneja programu wa Tanganyika Law Society (TLS) Mackphason Mshana akizungumza katika hafla hiyo kuelezea ushiriki wao katika mchakato wa katiba mpya kupitia mradi huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Bw. Francis Kiwanga (kushoto) akitia saini Mkataba wa utekelezaji wa Mradi huo na Taasisi ya Jukwaa la Katiba Tanzania. (kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Bob Wangwe.

Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Bw. Francis Kiwanga (kushoto) katika makabiadhiano ya Mkataba wa utekelezaji wa Mradi huo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Jukwaa la Katiba Tanzania Bob Wangwe (kulia).

Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Bw. Francis Kiwanga (kushoto) akimkabiddhi Mkurugenzi wa Tanzania Association of NGOs Adamson Nsimba (kulia) mkataba wa utekelezaji wa Mradi wa “Uraia Wetu” mara baada ya kutia saini mkataba huo Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Bw. Francis Kiwanga (wa pili kushoto) akikabidhi hundi kwa Taasisi zilizosaini mkataba wa utekelezaji wa mradi huo Jijini Dar es Salaam.

(PICHA NA: FCS) DAR ES SALAAM

Foundation For Civil Society (FCS) imezindua mradi ujulikanao “Uraia Wetu” utakaotekelezwa kwa miaka mitatu kwaajili ya kukuza uwezo wa AZAKi na kuongeza hamasa na wigo wa ushiriki wa wananchi katika machakato wa katiba mpya pamoja na michakato ya utawala wa kidemokrasia, ikiwa ni pamoja na mapitio ya katiba na maridhiano ya kitaifa.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mradi huo leo Mei 9, 2023 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Bw. Francis Kiwanga, amesema mradi wa "Uraia Wetu" utachangia kuboresha na kuwezesha mfumo wa sera na mazingira ya ushirikishwaji wa wananchi ili kukuza utawala wa kidemokrasia nchini Tanzania.

"Wananchi wana jukumu kubwa na ni kiungo muhimu cha demokrasia yetu. Mradi wa ‘Uraia Wetu’ unalenga kukuza uhuru wa kujieleza, kupata habari, uhuru wa kukusanyika, na kubaini fursa na nafasi iliyopo kwa wananchi kushiriki kikamilifu kwenye masuala ya kiraia.

"Tunafahamu kwamba Serikali imepiga firimbi ya kuashiria mwanzo wa mchakato wa maandalizi ya katiba mpya na hivyo sisi kama Foundation For Civil Society tukishirikiana na wadau wenzetu wa maendeleo tumeamua kuja na mpango kabambe wa miaka mitatu wenye lengo la kumfanya kila mwananchi aweze kushiriki katika mchakato wa katiba mpya.

"Tunafahamu katiba yetu ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ibara ya 8 imeweka mamlaka kwa wananchi hivyo hata katika zoezi hili tunalofanya la utengenezaji wa katiba ni lazima tuwaweke wananchi katikati ya mchakato wote wa kupata kabita mpya" amesema Bw. Kiwanga.

Aidha ameeleza kuwa wakati wa mchakato wa marekebisho ya katiba uliopita walijifunza na kuona kwamba wananchi wana nia ya kushiriki katika uundaji wa katiba, na kwamba wanataka kuongezeka kwa uwazi, uwajibikaji, maadili ya kitaifa na juhudi za kweli za kupambana na rushwa.

“Wananchi wana nia ya dhati ya kushiriki katika uundaji wa katiba, wanataka kuongezeka kwa uwazi, uwajibikaji, maadili kitaifa na juhudi za kweli za kupambana na rushwa. Hata hivyo, wakati nafasi ya kiraia ni ndogo, makundi yaliyotengwa kama vile wanawake, vijana, watoto, na watu wenye ulemavu hukabiliana na changamoto, kwani wanakosa majukwaa ya kueleza mawazo yao,” ameeleza Bw Kiwanga ameongeza.

Ameongeza kuwa FCS inaamini kuwa Asasi za Kiraia ngazi za chini zinapowezeshwa na kupata nafasi mwafaka ya kutekeleza majukumu yake ipasavyo, wananchi watafahamu haki zao na kufaidika nazo. Jukumu la asasi za kiraia katika kuendeleza ajenda za wananchi bado ni kubwa na muhimu sana.

“FCS inalenga kuhakikisha watu wanawezeshwa na kuwajibika, na wanapata haki zao za msingi za kiuchumi na kijamii ili kufanya maisha yao kuwa bora. Mradi unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) pia utaimarisha uwezo wa AZAKi ili kukuza ushirikishwaji mzuri kati yao na serikali na wadau wakuu wa maendeleo. Kwa kuongezeka kwa uwezo, AZAKi zitaweza kutekeleza majukumu yao ipasavyo, na kushirikiana na serikali kushawishi mabadiliko,” Bw Kiwanga ameongeza.

Kwa upande wake Meneja Mipango wa FCS anayehusika na Utawala na Ujumuishwaji wa Jamii, Bi Edna Chilimo, amesema mradi huo unalenga kukuza ushiriki wa asasi za kiraia kwenye michakato ya sera za wadau mbalimbali na kuimarisha uwezo wa AZAKi ili kukuza uwajibikaji wa umma. Mradi unaendana na malengo ya FCS na Umoja wa Ulaya ya kukuza na kulinda haki za binadamu kupitia mazungumzo, utetezi na kujenga uwezo wa ktaalamu.

“Juhudi hizi zinalenga kukuza uhuru wa vyombo vya habari, upatikanaji wa taarifa bora, amani na utatuzi wa migogoro, ushiriki wa wananchi, hasa kwa wanawake na vijana, upatikanaji wa haki kwa makundi ya watu waliotengwa na mipango ya kupambana na rushwa” amesema Bi. Chilimo.

Umoja wa Ulaya (EU) utafadhaili Mradi wa “Uraia Wetu” kwa miaka mitatu kuanzia 2023 hadi 2025 ambapo FCS kama sehemu ya utekelezaji wa mradi huo, imetoa ruzuku ya Tsh 4,916,402,000 kwa AZAKi kumi na mbili (12) za Tanzania Bara na Zanzibar. AZAKI hizo zitaweza kufanya shughuli zitakazochangia katika utekelezaji wa malengo ya mradi huo.

FCS ni Shirika huru la Kitanzania la Maendeleo lisilo la faida ambalo hutoa ruzuku na huduma za kujenga uwezo kwa AZAKi nchini. Tangu kuanzishwa kwake miaka 20 iliyopita, FCS imechangia pakubwa katika kuimarisha uwezo wa asasi za kiraia nchini Tanzania. FCS imeziwezesha AZAKi kuwa chachu ya maendeleo na wananchi kuwa mstari wa mbele katika kuimarisha utawala wa kidemokrasia nchini Tanzania.
Share:

BAISKELI ZA UMEME, PIKIPIKI ZITAZUIA UCHAFUZI WA MAZINGIRA NA PUNGUZA GHARAMA ZA USAFIRI


Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) Shaukatali Hussein kushoto akifuatilia vijana hao wakiendelea na utengenezaji wa pikipiki zinazotumia umeme

Vijana wakiendelea na utengenezaji wa pikipiki za umeme kama wanavyoonekana katika Shule ya Ufundi Tanga School

Vijana wakiendelea na matengenezo ya pikipiki zinazotumia umeme

Matengenezo ya Pikipi za kutumia Umeme yakiendeleaMkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) Shaukatali Hussein akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maendeleo ya mafunzo hayo

Na Mwandishi Wetu,Tanga


VIJANA wanaopata mafunzo ya kutengeneza na kuunda Pikipiki na Baiskeli zinazotumia umeme Jijini Tanga wamesema kwamba zitasaidia kuzuia uchafu wa mazingira katika maeneo mbalimbali nchini. Pia, ma dereva haswa bodaboda wataweza kujiongezea kipato kwa kupunguza gharama ya mafuta na usafiri


Mafunzo hayo yanaendeshwa na Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization(TOIO) na Robotech Labs chini ya ufadhili wa Shirika la Botnar Fondation ambao wamedhamiria kutoa ujuzi kwa vijana ili kuweza kuutumia na kuweza kujikwamua kiuchumi


Akizungumza wakati mafunzo hayo yakiendelea ,Mwanafunzi wa kidato cha Pili wa shule ya Sekondari Tanga Ufundi Saidi Kasim alisema mafunzo hayo yanawapa mwanga mzuri wa mbeleni kutokana na kwamba ujuzi wanaoupata utawasaidia kuweza kujiajiri


Alisema kutokana na kwamba mbinu mbalimbali ambazo wamekuwa wakifundishwa siku hadi siku ikiwemo jinsi ya kutenegenza pikipiki za umeme na baiskeli kutokana kwa mkufunzi wao na hivyo kuwa njia nzuri ya kuweza kukabiliana na soko la ajira hapa nchini.


Aidha alisema kutokana na kwamba hivi sasa zipo changamoto mbalimbali zinazotokana na uchafuzi wa mazingira na hivyo wakati Serikali ikichukua jitihada za kukabiliana nayo mradi huo utakuwa ni wa manufaa kutokana na kujibu tatizo hilo.


“Mafunzo haya na pikipiki za umeme na baiskeli tunayojifunza hapa ni jinsi zinavyotengenezwa na namna ya kuweka fremu zanje na kuweka waya hakika mradi huu utatusaidia sana “Alisema


“Lakini pia utatusaidia kujiajiri pindi tunapomaliza shule na kwenda nje tunaweza kuanzisha mradi wa kubadilisha pikipiki za kawaida na zikawa zinatumia umeme kutokana na kwamba sio jambo gumu”Alisema


Haya hivyo alitoa wito kwa vijana wengine Jijini Tanga kuchangamkia mafunzo hayo kutokana na umuhimu wake wa kuweza kuwaandaa kujiajiri baadae na hivyo kujikwamua kiuchumi wao na jamii zao


Naye kwa upande wake Peter Sanga ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili alisema mafunzo ambayo wamefundishwa kwenye mradi huo yamewawezesha kufahamu namna ya kuzibadilisha pikipiki za umeme na baiskeli kutoka zilivyokuwa awali zikitumia mafuta.


Hata hivyo alisema pia wamefundishwa namna ya kutengeneza pikipiki na baiskeli hizo kutumia umeme na hilo ni jambo muhimu kutokana na kwamba kipindi hiki uchafuzi wa mazingira umekuwa mkubwa sana.


“Kwa sababu ukifuatilia vyombo vingi vya usafiri vimekuwa vikitumia mafuta na yamekuwa ni chanzo cha kuchafua mazingira hivyo vyombo hivyo ni muhimu kwa lengo la kutunza mazingira”Alisema


Aliongeza kwamba mradi huo una umuhimu mkubwa katika kutunza mazingira kwa sababu vitakapokuwepo hata vyombo vinavyotumia mafuta vitapungua na hivyo kuwa moja ya kutunza mazingira.


Awali akizungumza Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) Shaukatali Hussein alisema kwamba wameanza fursa ya mafunzo hayo kuanzia May 5 -10 kuhusu pikipiki na baiskeli za umeme lengo wanataka vijana kutoka kata mbalimbali wachangamkie fursa ya kusoma jinsi ya kuviunga,kuvirekebisha na kutenegenza baiskeli na pikipiki za umeme.


Alisema somo hilo lina vipindi viwili awamu ya kwanza ni kuanzia asubuhi saa nne mpaka saa sita na pili kuanzia saa nane mpaka saa kumi mpaka sasa wamepata vijana zaidi ya 30 huku akitoa shukrani za dhati kwa Jiji la Tanga na Taasisi ya Fondation Botnar ambao wamewezesha kutoa mafunzo hayo kwa vijana mbalimbali.
Share:

Tuesday, 9 May 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO MEI 10,2023

















Share:

MBUNGE MTATURU ATIKISA BUNGE AGUSA WAKULIMA



MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameishauri serikali kuanzisha kanda maalum ya kilimo ili kuwezesha zao kulimwa kwenye mkoa husika unaostahmili zao hilo.

Akichangia bajeti ya wizara ya kilimo Mei 9,2023,Mtaturu amesema ikifanyika hilo usalama wa chakula utakuwepo na mwisho wa siku pato la Taifa litaongezeka kupitia sekta ya kilimo.

“Nikuombe sana nchi hii tumekuwa sasa kutoka Mtwara mpaka Kigoma watu wanataka wote walime zao moja linaitwa korosho haiwezekani mwenyekiti,hatuwezi kuwa na kilimo cha korosho nchi nzima hata mazingira au hali ya hewa hairuhusu maana yake hata concetration ya namna ya kusaidia kilimo haitakuwepo,

“Mtu atoke kule Tandahimba anataka kwenda mpaka kule Mwanza alime alizeti haiwezekani ,tufike mahali tuwe na kanda maalum kwamba hii kanda ni ya alizeti kama ni Singida tu constrate pale Singida na mikoa ambayo inaweza kutoa maeneo,”amesisitiza.

Amempongeza Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Mkoa wa Singida Parseko Koni kwa ambaye alizuia mahindi kulimwa mkoani humo na badala yake akaelekeza watu walime mtama na matokeo yake ikazalishwa kwa wingi.

ENEO LA UMWAGILIAJI.

Akichangia eneo hilo Mtaturu ameishauri serikali kuzingatia kilimo cha umwagiliaji ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

“Nina amini kabisa mabadiliko ya tabia nchi yameathiri kilimo cha Tanzania na sio Tanzania pekee bali maeneo mengi ya Afrika, lakini kama tutaendelea na hali ya kusubiria huruma ya Mungu kwa ajili ya kuleta mvua peke yake hatutaweza kusogeza kilimo hiki na kila mwaka tutakuja na sababu kwamba mwaka jana hatukufikia lengo kwa sababu mvua haikunyesha za kutosha,”amesema.

Ametoa ombi kwa serikali kutenga bajeti ya kutosha kwenye eneo la skimu za umwagiliaji ,lakini tunaomba skimu hizi nani anaenda kuzitunza kule chini,tunaona skimu nyingi hazitoi matokeo na kuna baadhi ya maeneo hata watu hawajui maana ya skimu yenyewe,nikuombe Waziri tutafute Mechanism nzuri ya kusimamia hili,

Amesema kuna maeneo mengi ya mito ,kuna maji ambayo yanapita kila mahali lakini wasipozuia maji na kuyatumia vizuri maana yake kilimo hakitaweza kubadilika.

SKIMU YA UMWAGILIAJI YA MANG’ONYI.

“Tunajua kwenye wizara yako umeiangalia skimu ya Mang’onyi lakini nikuombe waziri wakati unahitimisha hoja uzingatie hili,watu wa Mang’onyi wanataka kusikia wizara inasemaje,mwaka huu wa fedha tujenge ile skimu na kuiboresha kwa kuwa sasa hivi kuna soko la mbogamboga katika mgodi wa Ashanta ambao upo pale Mang’onyi,”amesema.

Mtaturu amesema wakitaka mabadiliko kwenye sekta ya kilimo nchini yanahitajika mambo matatu ambayo ni utaalam kwa maana ya teknolojia au elimu,uwekezaji kwa maana ya fedha na pembejeo ambazo zinafaa katika maeneo ya nchi.

“Ukienda kwenye utaalam ni afisa ugani wangapi ambao wana uwezo wa kumsaidia mkulima pale kijijini,wengi wanazidiwa uwezo na wakulima hivyo kuna haja ya kuwasaidia kubadilisha mtazamo wa kazi wanazozifanya,”ameongeza.

Ameiomba serikali iongeze fedha za kutosha kwenye eneo la kilimo ili watu Milioni 40 wanaojishughulisha na kilimo waweze kubadilisha kilimo na uchumi wan chi.

“Eneo la mbolea,viuatilifu na mbegu ni eneo ambalo tukifnaya vizuri na kuongeza utafiti na mbegu za kutosha zinazofaa zitamfanya mkulima awe na matokeo makubwa kwenye eneo lake,”.

SHUKRANI KWA SERIKALI.

“Kwanza nimpongeze Rais Samia Suluhu Hassan kwa dhamira yake ya kukibadilisha kilimo cha Tanzania kwa kuamini kabisa tukiboresha kilimo maana yake unaboresha uchumi wao watanzania wengi ambao wanafanya kazi hii,

“Nimshukuru zaidi waziri Bashe kwa namna ambavyo sisi watu wa Ikungi tulivyokuwa na changamoto ya upungufu wa chakula lakini wakatuletea chakula cha bei nafuu kutoka NFRA ,chakula kilitusaidia na leo tunaenda kufanya mavuno,”ameeleza.

KILIMO KILIVYOSHABIHIANA NA ILANI YA CCM.

Mtaturu amesema kupitia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),yam waka 2020/2025,imeahidi kusimamia vizuri eneo la matumizi endelevu ya maji ya ardhi na ardhi ya kilimo na kuongeza miundombinu ya umwagiliaji jambo ambalo kupitia bajeti iliyosomwa tunaona linaendelea kutekelezeka.

“Makadirio yaliyowekwa mpaka 2025,tunapaswa tufikie asilimia 28 ya Pato la Taifa,lakini ukiangalia kwenye wasilisho tumefikia asilimia 26.1 maana yake tunaenda vizuri,miaka miwili na nusu ijayo huwenda tutafikia asilimia 28 kama ilivyoahidiwa katika Ilani,”amebainisha.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger