Monday, 1 May 2023

JAMAA AZUA GUMZO MTANDAONI ALIVYOPIGA PICHA KICHWA CHINI AKIFUNGA NDOA NA MKEWE



NA ANDREW CHALE


MWALIMU wa Dance na mcheza dance mjini Arusha ambaye picha zake zimekuwa gumzo mitandao kuanzia Aprili 29, 2023, Kilumbo Steven amefunguka juu ya uwezo wake wa aina mbalimbali ya 'break dance' akiwa amepiga picha akiwa kichwa chini na miguu juu akiwa na Mke wake wa ndoa pembeni.


Akizungumza kwa njia ya simu na Mwandishi Andrew Chale,  Break Dancer huyo kupitia mpango wake wa B Boy Kilumbo anasema kuwa amepata simu nyingi ikiwemo pia kuona wadau wakiposti picha zake hizo mitandaoni.


"Nimefanya densi ndani ya harusi yangu.

Lakini pia picha nyingi tulipiga sema hizo mbili za kusimama kwa kichwa chini ndo imesambaa zaidi mitandaoni,  ila tumepiga picha nyingi " amesema Kilumbo.


Aidha,  amefafanukuwa B Boy Kilumbo ni kwamba B imesimama kwenye Break,  Boy imesimama kama yeye mwenyewe  na Kilumbo ni jina lake.


"Watu wengi wameona picha zile lakini wamekuwa na maoni tofauti, Mie ni kijana ambaye nina malengo makubwa kupitia kipaji changu.


Nataka kuendeleza uwezo wangu huu na hata kuwarithisha wengine."Amesema Kilumbo. 


Ambapo lengo kubwa ni kuanzisha Shule maalum ya Break Dance kwa vijana wote wa kiume na kike ilikuongeza vijana wengine zaidi.


"Hapa Tanzania najulikana kwa vijana wengi na nimekuwa nikiwafunza kwenye Break Dance.


Lakini pia nimekuwa nikishiriki mashindano tofauti, ikiwemo shindano la Hip-hop Hasili na mwaka juzi nilikuwa mshindi wa kwanza.


Pia nimekuwa nikifanya mashindano kwa njia ya mtandao 'Online' Marekani na pia nchi zingine hivyo kwa sasa malengo ni kuona nafika mbali na pia kuacha alama.


Kilumbo anasema kuwa, yeye ni Mngoni aliyeamua kufanya maisha yake Arusha ambapo pia mbali na kufanya Break Dance, lakini pia anajihusisha na masuala ya Utalii akifanya program ya 'Ngondi ya mtembezi' akitembeza Watalii maeneo mbalimbali.



Mwisho.

Share:

MTOTO ALIYEDAIWA KUFARIKI NA KUZIKWA AKUTWA AKIWA HAI


Wakazi wa Kijiji cha Salong’we kilichopo wilayani Magu mkoani Mwanza wamekumbwa na taharuki baada ya mtoto aitwaye Mabilika Wilson aliyefariki na kuzikwa tarehe 17 mwezi huu kupatikana akiwa hai katika Kijiji cha Mwangika wilayani Kwimba mkoani humo.

Wilson Bulabo ni baba mzazi wa mtoto huyo amesema ni kweli mtoto wake huyo aliumwa kwa siku mbili na kufariki hatimaye wakamzika lakini alipoenda kumuangalia huyo mtoto aliyeonekana Kijiji cha Mwangika alimgundua kuwa ndiye mtoto wake aliyezikwa wiki chache zilizopita.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa amefika katika Kijiji hicho na kushuhudia kaburi likifukuliwa kwa ajili ya taratibu za uchunguzi wa tukio hilo ambapo amewataka wakazi wa Kijiji hicho na vijiji vya Jirani, kuwa watulivu kipindi ambacho uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.

Via EATV
Share:

JAMAA MWENYE WATOTO ZAIDI YA 550 APIGWA MARUFUKU KUSAMBAZA MBEGU ZAKE ZA KIUME


Jonathan Jacob Meijer (41) raia wa Uholanzi amepigwa marufuku kusambaza mbegu zake za kiume baada ya kugundulika kuwa ana watoto zaidi ya 550 duniani kupitia utoaji wa msaada wa mbegu za kiume za uzazi.

Mwanaume huyo mwaka 2017 alizuiwa kutoa mbegu za uzazi kwenye kliniki ya masuala ya uzazi nchini Uholanzi baada ya kufahamika kuwa alikuwa amezalisha watoto zaidi ya 100

Inaelezwa kuwa badala ya kuacha kuendelea na utoaji wa msaada huo, Jonathan aliendelea kutoa mbegu zake nje ya nchi yake na kwa njia ya mtandao.

Mahakama ya Uholanzi mjini The Hague imemwambia atoe orodha ya kliniki zote alizowatumia na kuziagiza ziharibu mbegu zake.
Share:

WARUDISHA MALI WAKIWA NA MATUMBO KAMA WENYE MIMBA

Ninaitwa Nathaniel kazi yangu ni uuzaji na usambazaji wa magari kutoka China kuleta Tanzania.Kazi yenyewe siyo kongwe sana kwangu ni kazi niliyoifanya kwa muda wa miaka mitatu sasa kabla sijaacha kujishughulisha na utowaji wa copper kwenye vyuma chakavu.

Kazi yenyewe niliipata baada ya kumfahamu daktari BAKONGWA bingwa wa kutatua shida za wengi mwenye nambari zake za whatsapp +243990627777 na tovuti zake https://bakongwadoctors.com .

Mwaka wa tatu toka nianze kujihusisha na kazi hii ya kuuza magari nilikuwa mwenye kusafirisafiri sana mara kwa mara na hivyo kupaacha nyumbani penyewe bila ya muangalizi, sikuwa mwenye haraka ya kuoa nilitaka kujikamilisha kwanza kwenye kila kona ya maisha yangu.

Sasa nilikuwa nimepanga mara baada ya safari yangu ya mwisho nimhusishe daktari juu ya suala langu la mimi kuoa ili anifanyie wepesi katika jambo hili ambalo vijana wengi huwa linatusumbua.

Uangalizi niliokuwa nao hapo nyumbani ni wa cctv tu ambazo zilifungwa na watu wa kampuni la delmac, kwa hivyo sikuwa na wasiwasi tena, sijui ni kipi walikifanya kwenye ulinzi wangu lakini nilipigiwa simu na delmac nikaambiwa kuwa majambazi wameingia nyumbani kwangu na kuiba kila kitu kwa bahati mbaya walifanikiwa kuzizima cctv na hivyo hazikuwanasa wala hawakujulikana.

Niliogopa sana kwa taarifa hizo tena nilikasirishwa sana nilipokumbuka ni jinsi gani na nguvu kiasi gani nimezitumia kupata mali hizo, nilipokumbuka mtu wa kunisaidia daktari bakongwa , nilimpigia na kumueleza kila lililotokea ,yeye hakuwa na wasiwasi aliniambia kuwa nitakapokuwa nimerudi nyumbani Tanzania mali zangu nazo zitarudi.

Kwakuwa ninamuamini sana sikuwa mtu wa pupa nilifunga mzigo wangu wa magari na kurudi Tanzania , mara tu baada ya kufika nyumbani siku ya pili yake nilishangazwa kuona vijana wanne wamekuja wamevimba matumbo wakiomba msamaha na kurudisha mali walizochukua.

Nilimpigia daktari na kumfahamisha lililotokea yeye akasema nifanye vile mimi ninataka kwa kuwa ni mali zangu nikaamua vijana wale warudishe gharama za kuharibu mfumo wangu wa cctv, mali zangu na kisha kuwasamehe , ninashukuru sana kwa daktari kwa kweli haujawahi kuniangusha katika jambo lolote.


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU MEI MOSI ,2023




 



Share:

YANGA YATINGA NUSU FAINALI CAF


MABINGWA Watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara timu ya Yanga imewatoa kimasomaso watanzania baada ya kutinga hatua ya Nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kutoka sare ya kutofungana na Rivers United kutoka nchini Nigeria mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Yanga imepata nafasi hiyo baada ya ushindi wa mabao 2-0 mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Nigeria.

Yanga ni kama inataka kufuata nyao za timu ya Simba ambayo Mwaka 1993 ilifanikiwa kutinga fainali za Kombe la CAF ikimenyana na Stella Abdijan Kutoka Ivory Coast ambapo hata hivyo haikufanikiwa kuchukua ubingwa

Simba SC ambayo ilikuwa inashikiriki Kombe la Klabu Bingwa Africa ilishindwa kutinga nusu Fainali ya klabu bingwa Afrika kwa kuondoshwa na Wydad Casablanca kwa mikwaju ya Penalti 4-3
Tanzania Sasa imeingiza timu moja nusu Fainali Katika michuano ya Kombe la Shirikisho ambalo zinacheza timu ambazo hazikufuzu Katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Hivi Sasa rasmi Yanga SC itakutana na Marumo Gallants kutoka Afrika Kusini waliwatoa Pyramids ya Misri kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya leo kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Mchezo wa kwanza wa nusu Fainali unatarajia kuchezwa Mei 14 au 15 mwaka huu uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kabla ya wiki moja marudiano kuchezwa nchini Afrika Kusini.

Timu nyingine ambayo zimefuzu Katika michuano ya Kombe la Shirikisho ni ASEC Mimosas ya Ivory Coastal baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya US Monastir sasa inamsubiri Mshindi kati ya FAR Rabat ya Morocco au USM Alger ya Algeria ambao watacheza majira ya saa nne usiku.
Share:

Sunday, 30 April 2023

AUAWA KWA KUCHINJWA BAADA YA KUPEWA TALAKA NA MUMEWE TINDE



Picha haihusiani na habari hapa chini

Na Mwandishi wetu - Tinde

Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Mwanandakuna anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 58-60 mkazi wa kitongoji cha Ngaka kijiji cha Nyambui kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye kali shingoni na tumboni na watu wasiofahamika akiwa nyumbani kwake.


Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa mapema jana jioni  Aprili 29, 2023 kuna vijana walifika eneo jirani na alipopanga mama huyo wakawa wanavuta sigara lakini wakazi wa eneo hilo hawakuchukulia maanani kwa sababu mtaa ule una mwingiliano wa watu wengi.


“Kuna watu wawili walikuwa jirani chumba cha mama huyu, wakakaa kwa muda mrefu wakivuta sigara  na kuchat na simu huyo mama alikuwa anapika chakula cha usiku, wakati mama anatoka kumwaga maji ya kuoshea nyanya/uchafu majira ya saa mbili kasoro usiku ndipo watu hao wakamkaba na kumchoma kwa visu shingoni na tumboni”,wameeleza wananchi kutoka Tinde.


“Huyo mama alikuwa anaishi katika kitongoji hiki hiki na baada ya mgogoro wa ndoa aliondoka kwa mmewe akapanga chumba chake katika kitongoji hiki. Ametoka kwa mme wake miezi kadhaa iliyopita.Tukio hili limetokea wakati kesi ya kugawana mali baina yake na mme wake ipo mahakamani kwani baada ya kuachana na mmewe ambaye yupo Arusha ilifikia hatua ya kugawana mali wiki hii”, taarifa kutoka Tinde zinaeleza.


Inaelezwa kuwa Kesi ya ndoa baina ya mwanamke huyo na mmewe ilikuwa imefikia tamati Alhamis wiki hii Aprili 27,2023 ambapo alipewa talaka kwenye mahakama ya Mwanzo Tinde.


Akizungumza na Mwandishi wetu,i Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ngaka bw. Mabula Kuzenza amesema watu waliohusika na mauaji hayo bado hawajafahamika.

“Jana Jumamosi Aprili 29,2023 majira ya saa mbili usiku nilipigiwa simu na majirani wa marehemu kwamba kuna tukio kuwa Mwanandakuna ameuawa kwa kuchomwa na visu shingoni na tumboni, baada ya hapo nikapiga simu polisi kwa hatua zaidi”,amesema Kuzenza.


“Waliomchoma hawajahamika na chanzo cha mauaji bado hakijafahamika, inaelezwa kuwa kuna watu wasiofahamika walionekana eneo hilo lakini kutokana na kwamba eneo hili limechangamka kuna mwingiliano wa watu hakuna aliyedhani kuna tukio lingetokea… Inasadikika huenda hao ndiyo wamefanya mauaji haya.

Tukio la mauaji limetokea kimya kimya baada ya mama huyo kutoka nje kwenda kumwaga uchafu na ndani ya mtu mfupi majirani wakaona mtu kaanguka chini na kubaini kuwa ameuawa, hata haijulikani imetokeaje tokeaje”,ameeleza Mwenyekiti wa Kitongoji.


Akizungumza na Mwandishi wetu, Diwani wa kata ya Tinde Japhar Kanolo amesema mama huyo ameuawa akiwa nyumbani kwake alipopanga kitongoji cha Ngaka kijiji cha Nyambui kata ya Tinde kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni na tumboni.


“Nilipewa taarifa kuhusu tukio hili la kikatili majira ya saa mbili usiku ambapo wananchi waliokuwa eneo hilo wanasema mapema jana jioni watu waliona vijana wawili wakichat na simu karibu na nyumbani alipopanga mama huyo. Mama huyo alifarakana na mme wake na juzi ndiyo alipata talaka yake mahakamani 40 ya mali walizopata”,ameeleza Kanolo.


Diwani wa viti maalumu tarafa ya Itwangi Mhe. Hellena Daudi Ng’wana mbuli amelaani tukio hilo huku akiomba vyombo vya sheria kuwachukulia hatua kali watu watakaobainika kufanya mauaji hayo ya kikatili.


“Ukatili huu aliofanyiwa mama huyu ni mbaya, wanakosea sana kuua wanawake. Naomba wananchi waache ukatili na vyombo vya vichukue hatua kali kwa watakaobainika kuhusika na tukio hili”,ameeleza Diwani huyo.

Juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ili azungumzie tukio hilo zinaendelea.


Share:

KIWANJA CHA NDEGE CHA SUMBAWANGA KUBORESHWA

Mkoa wa Rukwa waingia katika historia mpya mara baada ya Serikali kupitia Wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) kuingia mkataba na Kampuni ya M/s Beijing Construction Engineering Group Co. Ltd ya nchini China kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga kwa gharama ya Shilingi Bilioni 55.908 kwa muda wa miezi 18.

Uboreshaji huo ni utekelezaji wa mkakati wa Serikali wa kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii Mkoani humo na ukanda wa Magharibi mwa nchi ya Tanzania ili kuongeza ufanisi katika sekta ya usafiri na usafirishaji.

Zoezi la utiaji saini wa mkataba huo uliofanyika katika Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga, mkoani humo umefanyika kati ya Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Rogatus Matavila pamoja na Mwanasheria wa TANROADS, Wakili Gurisha Mwanga na kushuhudiwa na wananchi, viongozi mbalimbali wa Serikali na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa.

Akizungumza baada ya Zoezi hilo, Prof. Mbarawa ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea kuboresha miundombinu pamoja na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) kwa kutoa fedha za utekelezaji wa mradi huo.

Waziri Prof. Mbarawa ameeleza kuwa uboreshaji wa kiwanja hicho utakapokamilika utaruhusu kiwanja hicho kufanya kazi saa 24 yaani usiku na mchana na kitakuwa na uwezo wa kupokea ndege aina ya Boeing Q 400 pamoja na ATR 72.

Amesema utekelezaji wa mradi huo umeletwa mahsusi ili kuchochea shughuli za kiuchumi kama vile kilimo, utalii, uwekezaji, uvuvi, usafirishaji wa mizigo na abiria na shughuli za kijamii kwa ujumla.

"Mapema mwakani wana Sumbawanga mtegemee ndege ya kwanza kutua hapa", amesisitiza Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa amefafanua kuwa uboreshaji wa kiwanja hicho pia utahusisha ujenzi wa jengo jipya la abiria, ununuzi na usimikaji wa taa za kuongozea ndege (AGL) na mitambo ya Usalama (DVOR/DME), barabara ya kuingia na kutoka kiwanjani, maegesho ya magari na uzio wa usalama.

Aidha, amesema kiwanja hicho kwa sasa kina barabara ya kuruka na kutua ndege ya kiwango cha changarawe yenye urefu wa kilometa 1,516 na upana wa meta 30 ambapo kupitia mradi huu barabara hiyo itaboreshwa kufikia urefu wa kilometa 1,750 na upana wa meta 30 kwa kiwango cha lami.

Waziri Prof. Mbarawa, ametoa rai kwa Uongozi wa Mkoa wa Rukwa kuusimamia mradi na vifaa vitakavyotumika katika ujenzi huo pamoja na kuwasisitiza wananchi wetu wanaozunguka eneo la mradi kuepukana na uhalifu wa namna yoyote katika mradi badala yake waulinde mradi huu ili wafaidike na fursa mbalimbali zitakazojitokeza wakati utekelezaji wa mradi ukiwa unaendelea.

"Mkiulinda mradi huu utasaidia kulinda thamani halisi ya mradi lakini pia kukamilika kwa wakati na ubora unaokubalika", amesisitiza Prof. Mbarawa.

Amewaagiza Wataalam wa Wizara, TANROADS, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Anga (TCAA) na Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) na wadau wote kufanya kazi kwa weledi na kusimamia utekelezaji wa mradi huu ili kuhakikisha kuwa mradi unakamilika kwa wakati.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Queen Sendinga, ameishukuru Serikali kwa baraka ya miradi inayoendelea mkoani kwake ambapo ukiondoa kiwanja cha ndege hicho pia ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ya Ntendo - Kizungu (km 25) na barabara ya Matai - Tatanda (km 25) inaendelea vyema.

Mkuu wa Mkoa huyo pia ameahidi kuusimamia uboreshaji wa kiwanja hicho ili uweze kukamilika kwa wakati kwani mkoa huo hauna viporo vya miradi kucheleweshwa.

Awali akitoa taarifa ya mradi huo, Mtendaji Mkuu wa TANROADS, ameeleza kuwa uboreshaji wa kiwanja hicho utahusisha ujenzi wa jengo jipya la abiria lenye uwezo wa kuhudumia abiria 150,000 kwa mwaka ambapo Jengo hilo litakuwa na sehemu ya kuongozea ndege.

Matavila ameeleza kwamba upembuzi yakinifu wa kiwanja hicho ulifanywa na kampuni ya Sir Fredrick Snow & Partners Ltd ya Uingereza ikishirikiana na Kampuni ya Belva Consult ya Tanzania kati ya mwaka 2007 mpaka mwaka 2009.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Eng. Rogatus Mativila akisaini mkataba wa ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbwanga na Mwakilishi kutoka kampuni ya M/s Beijing Construction Engineering Group ya nchini China kwa gharama ya Bilioni 55.908 kwa muda wa miezi 18, mkoani Rukwa.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Eng. Rogatus Mativila pamoja na Mwakilishi kutoka kampuni ya M/s Beijing Construction Engineering Group ya nchini China wakionesha mkataba wa ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbwanga mara baada ya kusainiwa, mkoani Rukwa. Uboreshaji huo utatekelezwa kwa muda wa miezi 18 na utagharimu Bilioni 55.908.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, akizungumza na wananchi wa mkoa wa Rukwa mara baada ya kusiani mkataba wa ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbwanga utakaogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 55.908, mkoani humo.



Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Eng. Rogatus Mativila, akitoa taarifa ya mradi wa ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbwanga utakaogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 55.908, wakati wa utiaji saini mkataba wa uboreshaji wa kiwanja hicho na mkandarasi kutoka kampuni ya M/s Beijing Construction Engineering Group ya nchini China, mkoani Rukwa.


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Queen Sendinga, katika hafla ya utiaji saini mkataba wa ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbwanga utakaogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 55.908, mkoani humo.



Muonekano wa sehemu ya barabara ya kuruka na kutua ndege kwa kiwango cha changarawe katika Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga ambapo Serikali imesaini mkataba wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja hicho kwa gharama ya shilingi Bilioni 55.908, mkoani Rukwa. Ukarabati wa barabara hiyo utafanyika kutoka kilometa 1,516 hadi kufikia kilometa 1,750 kwa kiwango cha lami.
Share:

WAZIRI DKT MABULA AFAFANUA UPOTOSHAJI VIWANJA VINAVYOMILIKIWA NA KAMPUNI YA SLIPWAY TOWERS LTD

Na Munir Shemweta, WANMM

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ametoa ufafanuzi wa viwanja vinavyomilikiwa kampuni ya Slipway Towers Ltd vilivyopo Msasani Peninsula jijini Dar es Salaam ambapo amemuagiza katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eng. Anthony Sanga kuchunguza kubaini kama kuna wataalam waliohusika katika upotoshaji huo ili waweze kuchukuliwa hatua za haraka za kinidhamu.

Aidha, Dkt Mabula ameelekeza kuwa, kuanzia sasa Manispaa ya Kinondoni inapotaka kupangisha maeneo au eneo ambalo ni kwa matumizi ya umma inatakiwa kijiridhisha kwanza kwa lengo la kujua eneo husika kama mipaka yake haijaingiliana na wapangishaji wengine ili kuepuka migogoro.

Kumbukumbu za Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi zinaonesha kuwa viwanja namba 1497, 1498 na 1856 vinamilikiwa kampuni ya Slipway Towers Limited kwa hati namba 29035 ya muda wa miaka 99 iliyotolewa Januari 1, 1980 kwa ukubwa wa hekta 1.383 kama ilivyo kwenye ramani ya usajili namba 18460 ya mwaka 1980.

Hata hivyo, upimaji wa viwanja ulirejewa na kufanyiwa maboresho yaliyoongeza kiwanja namna 1967 ambapo kampuni ya Slipway Towers Ltd iliomba kiwanja husika kuunganishwa kwenye hati moja na maombi kukubaliwa na kusajiliwa Agosti 13, 1998 ambapo ukubwa uliongezeka kutoka hekta 1.383 hadi 1.8759.

Waziri Mabula alitoa ufafanuzi huo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam tarehe 29 April 2023 kufuatia malalamiko yaliyotolewa na mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Somgoro Mnyonge kuhusu umiliki na uendelezaji wa eneo katika viwanja hivyo.

"Ieleweke wazi kuwa mhe. Dkt Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akivutia wawekezaji wengi nchini katika sekta mbalimbali kwa maslahi mapana ya nchi yetu hivyo serikali haitavumilia vitendo vinavyoenda kinyume na azma ya rais kuvutia wawekezaji na tanzania ni sehemu salama kuwekeza" alisema Dkt Mabula.

Amemuelekeza Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala kusimamia taratibu zote katika kipindi cha mpito wakati mgogoro katika eneo hilo ukishughulikiwa sambamba na kusimamia pale inapotokea changamoto yoyote kwa kuangalia namna bora ya kufanya mawasiliano kabla ya kutolewa matamko yenye kuleta upinzani.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, uhakiki uliofanywa na wataalam wa wizara yake umebaini kuwa, siyo kweli kwamba mwekezaji kampuni ya Slipway Towers Limited imeingia baharini kwa mita 850 bali zilizotajwa ni mita za mraba ambazo Manispaa ya Kinondoni imempangisha kampuni ya Dorishers ndani ya kiwanja cha hati milki namba 29035 kinachomilikiwa na kampuni ya Slipway Towers Limited.

"Tangu mwaka 1998 hadi sasa wizara haijapata maombi ya Slipway kufanya mabadiliko yoyote kwenye ramani au hati miki na hakuna jambo lolote wizarani linalohusiana na upimaji au umilikishaji unaohusina na kampuni ya Slipway towers ltd, kilichosemwa na meya wa manispaa ya kinondoni kuwa kuna mchakato unaoendelea ndani ya wizara hakipo na hakuna mchakato wala maombi". Alisema Waziri Mabula.

Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, mpango wa uendelezaji upya eneo la Masaki yaani Masaki-Oyesterbay Development Plan ya 2011-2031 ulijadiliwa na kupitishwa na Baraza la Mawaziti hivyo marekebisho yoyote ya mpango wa eneo hilo lazima yapitishwe na Baraza la Mawaziri.

"Kwa hiyo wizara kama wizara hakuna inachoweza kufanya mabadiliko hayo kwa sababu tayari yapo katika mpango wa uendellezaji ulioasisiwa na Baraza la Mawaziri na marekebisho yoyote lazima yapitishwe na baraza hilo". Alifafanua Dkt Mabula.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula akifafanua jambo wakati wa kikao chake na waandishi wa habari kufafanua upotoshaji wa viwanja vinavyomilikiwa na kampuni ya Slipway Towers Ltd tarehe 29 April 2023.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Slaam wakati wa kutoa ufafanua wa upotoshaji wa viwanja vinavyomilikiwa na kampuni ya Slipway Towers Ltd tarehe 29 April 2023.

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Eng. Anthony Sanga (Kulia) pamoja na Mpima wa Wizara ya Ardhi Romanus Sanga wakati wa kikao cha Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam tarehe 29 April 2023. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)
Share:

CHUO CHA MZUMBE KUZITAFUTIA MASOKO BUNIFU ZINAZOIBULIWA NA WANAFUNZI WAKE



Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof.William Mwegoha wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda la chuo hicho katika kilele cha Maadhimisho ya maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.


Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof.William Mwegoha,akizungumza na watumishi wa chuo hicho katika banda la chuo hicho katika kilele cha Maadhimisho ya maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.


Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof.William Mwegoha akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa chuo hicho wakati wa kilele cha Maadhimisho ya maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

CHUO Kikuu cha Mzumbe kimesema kitaendelea kuibua,kuendeleza na kuzitafutia masoko bunifu mbalimbali zinazoibuliwa na wanafunzi wa chuo hicho huku kikidai tayari ina kitengo maalum kwa kusimamia bunifu hizo.

Hayo yameelezwa na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof.William Mwegoha wakati akizungumza katika banda la chuo hicho katika maonesho ya wiki ya ubunifu yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Prof Mwegoha amesema wanayafurahia maonesho hayo kwani yanahamasisha bunifu mbalimbali pamoja na masuala ya Sayansi na Teknolojia.

Amesema Mzumbe wanachokifanya ni kuhakikisha wanapromoti bunifu mbalimbali za wanafunzi wao ambapo amedai kwa sasa wana Kitivo cha Sayansi na Teknolojia.

Amesema katika mambo wanayofanya katika kitivo hicho ni pamoja na wanafunzi kuja na bunifu mbalimbali ambazo zinaenda kutatua changamoto za wananchi.

Amesema bunifu ambazo wamekuja nazo ni kwa ajili ya kupambana na changamoto za afya,mazingira,usafirishaji na uchukuzi.

“Sasa hivi tuna kitengo maalum kabisa kwa ajili ya kusimamia bunifu,baada ya hapa hawa vijana ili zile waweze kuzitangaza zifike mahali ambako wataweza kutengeneza biashara ambazo zitawainua kiuchumi.

“Hii inaendana na sera ya kitaifa ya kuhakikisha kwamba vijana wanajiajiri vijana wanaokuja hapa wanakuja na mawazo yao na tunawapa ushuri na baadae kuzigeuza kuwa biashara ikiwa ni pamoja na kuwatafutia wafanadhili ambao watazikuza,”amesema Prof Mwegoha

Amesema kupitia kituo hicho cha ubunifu wameanza kwenye kituo atamizi ambacho kinawataalamu kwa ajili ya kukuza idea zao.

Amesema chuo kinakiwezesha kitengo hicho ili kuendeleza miradi na waendelee kuwepo na kuwafikisha katika ndoto zao.

“Tutaendelea kuzisapoti mpaka pale ambapo wanaweza kuziendeleza na kuwa fursa.Hata wakiamua kwenda kufanya hizo kazi wana mahali pa kuanzia,”amesema Prof Mwegoha

Amesema katika bunifu walizokuja nazo ni pamoja na jiko ambalo linatumia mkaa wa taka kwa ajili ya kulinda mazingira.

“Katika bunifu ambazo tumekuja nazo ni jiko ambalo linatumia mkaa wa taka kwa ajili ya nishati na hii ni moja ya bunifu ambazo zipo nyingi ili serikali ikipiga marufuku mkaa tuweze kusapoti, majiko yanatumia taka lakini yanatoa nishati kubwa,”amesema Prof Mwegoha
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger