Wednesday, 22 February 2023

SHIRIKA LA POSTA LA PANDA MITI KUTUNZA MAZINGIRA KWENYE CHANZO CHA MAJI MTO MHUMBU

 

Meneja wa Shirika la Posta Tanzania mkoani Shinyanga Julius Mponda (kushoto) akiwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ACP Janeth Magomi wakipanda miti kwenye chanzo cha maji mto mumbu ili kutunza mazingira.

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

SHIRIKA la Posta Tanzania mkoani Shinyanga limepanda miti kwenye chanzo cha maji mto Mhumbu uliopo jirani na nyumba za Jeshi la Polisi maeneo ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kukilinda chanzo hicho na kutunza mazingira.

Zoezi hilo la upandaji miti limefanyika leo Februari 22, 2023, ambapo watumishi wa Shirika hilo la Posta walishirikiana na Askari Polisi kupanda miti kwenye chanzo hicho cha maji mto Mhumbu, na kupandwa jumla ya miti 150 ya matunda na kivuli.

Meneja wa Shirika la Posta Tanzania mkoani Shinyanga Julius Mponda, amesema wamepanda miti kwenye chanzo hicho cha maji ikiwa ni kutekeleza maagizo ya Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango alipokuwa mkoani Shinyanga aliagiza Taasisi za Serikali zishiriki kupanda miti kwenye vyanzo vya maji.

“Shirika la Posta Tanzania mkoani Shinyanga tupo hapa kupanda miti kwenye chanzo hiki cha maji mto mumbu, ili kutunza mazingira na pia kutekeleza agizo la Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango la Taasisi za Serikali kutunza mazingira nya vyanzo vya maji, na tumepanda miti 150 ya matunda na kivuli,”amesema Mponda.

Aidha, amesema miti ambayo wameipanda itasaidia kulinda chanzo hicho cha maji pamoja na kutunza mazingira kwa kuzuai mmomonyoko wa udongo kwa sababu mto huo upo jirani na makazi ya watu zikiwamo na nyumba za Jeshi la Polisi.

Katika hatua nyingine ametoa shukrani kwa Jeshi la Polisi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na Manispaa kwa ushirikiano ambao wameutoa kwao na kufanikisha zoezi hilo la kupanda miti kwenye chanzo hicho cha maji mto Mhumbu.

Naye Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ACP Janeth Magomi, ambaye aliwaunga mkono Shirika hilo la Posta kupanda miti akiwa na Askari wake, amesema miti hiyo wataitunza ikue, huku akitoa wito kwa wananchi wa Shinyanga, wapande miti kwa wingi kwa sababu miti ni uhai na inatunza mazingira.

Amesema miti mingi ikipandwa kila mahali itaifanya Shinyanga kuwa ya kijana pamoja na kumaliza tatizo la ukame.

Meneja wa Shirika la Posta Tanzania mkoani Shinyanga Julius Mponda akizungumza kwenye zoezi hilo la upandaji miti.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akizungumza kwenye zoezi hilo la upandaji miti.

Meneja wa Shirika la Posta Tanzania mkoani Shinyanga Julius Mponda akipanda mti.

Meneja wa Shirika la Posta Tanzania mkoani Shinyanga Julius Mponda akipanda mti.

Meneja wa Shirika la Posta Tanzania mkoani Shinyanga Julius Mponda akipanda mti.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akipanda mti.

Afisa Maliasili na Mazingira Manispaa ya Shinyanga Ezra Manjerenga akipanda Mti.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.
Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Awali Picha ya pamoja ikipigwa kwenye zoezi hilo la upandaji miti kabla ya kupandwa kwenye chanzo cha maji mto mumbu.

Awali Picha ya pamoja ikipigwa kwenye zoezi hilo la upandaji miti kabla ya kupandwa kwenye chanzo cha maji mto mumbu.

Awali Picha ya pamoja ikipigwa kwenye zoezi hilo la upandaji miti kabla ya kupandwa kwenye chanzo cha maji mto mumbu.

Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania mkoani Shinyanga wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kupanda miti kwenye chanzo cha maji mto mumbu.

Picha ya pamoja ikipigwa.
Share:

MAADHIMISHO YA NUSU KARNE YA HIFADHI YA TAIFA YA MLIMA KILIMANJARO KUFANYIKA MACHI 16....UKAME BADO NI CHANGAMOTO



Kamishna msaidizi wa hifadhi ambaye pia ni Mkuu wa hifadhi ya KINAPA ,Angela Nyaki akiongea na waandishi wa habari juu ya maadhimisho ya kwanza ya miaka 50 tangia kuanzishwa kwa hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro


Na Woinde Shizza , ARUSHA


Mabadiliko ya tabia nchi yaliyosababishwa na ukame wa muda mrefu katika mikoa ya ukanda wa pwani mwa Tanzania pamoja na shughuli za kibinadamu yanatajwa kuwa ni miongoni mwa sababu ya kuyeyuka kwa theluji ya mlima Kilimanjaro.


Wataalam wa uhifadhi wanaeleza kuwa Hali hiyo imekuwa ikisababishwa na upepo kuvuma kuelekea mlima huo mrefu kupita yote barani Afrika.


Hayo yameelezwa na kamishna msaidizi wa hifadhi ambaye pia ni Mkuu wa hifadhi ya KINAPA ,Angela Nyaki wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya maadhimisho ya kwanza ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro yatakayofanyika, Machi 16 Mwaka huu katika makao makuu ya mlima huo yaliyopo, Marangu Mkoani Kilimanjaro .


Alisema kuwa upepo wa unapotoka katika mikoa ya ukanda wa pwani unapokuja katika mlima Kilimanjaro unakuja ukiwa mkavu pamoja na joto ambapo ndio unasababisha barafu kuendelea kuungua kwa hiyo sio jukumu la hifadhi ya mlima huo bali ni jukumu la Tanzania nzima kuhakikisha tunajihamisha hadi katika katika mikoa hiyo ambapo wanakata mikaa 
kwa wingi ambapo madhara yake yanaonekana kabisa katika katika mlima huo haswa kule kileleni.


"Tumejaribu kufuatilia sana kupitia ikolojia tukagundua kuwa kukiwa na upepo mkali sana baharini basi na mlimani kunakuwa na upepo mkali pia " ,alisema Angela.


Alibainisha kuwa maadhimisho hayo yataanza Machi 1,hadi kilele machi 16 mwaka huu,na mambo mbalimbali yatafanyika ikiwemo usafi wa Mlima utakaofanyika kwa siku kumi kuanzia machi 1,ambapo wadau wa utalii wapatao 500 watashiriki.


Alisema shughuli zingine zitakazofanyika katika sherehe za maadhimisho hayo ni pamoja na ugawaji na upandaji wa miti, zoezi litakalozinduliwa na mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu ,Pia watawatembelea waongoza utalii wa miaka ya 70 ili kuzungumza nao na kupata uzoefu wao na ushauri wao


Alisema tangu kuanzishwa kwa shughuli za utalii katika mlima Kilimanjaro, mafanikio kadhaa yamepatikana ikiwemo ongezeko la watalii na kufikia elfu 50 kwa mwaka, kuongezeka kwa njia za kupandisha mlima huo kutoka njia moja hadi kufikia njia sita .

Naibu Kamishna wa Uhifadhi na maendeleo ya biashara,Herman Batiho akiongea na waandishi wa habari


Kwa upande wake Naibu Kamishna wa Uhifadhi na maendeleo ya biashara,Herman Batiho alisema maadhimisho hayo ya kwanza ya aina yake yalioandaliwa na Shirika la hifadhi za taifa (TANAPA)yanalenga pia kuutambulisha umma na dunia kwa ujumla kuwa mlima huo upo na unapatikana katika nchi ya Tanzania pekee.


Alisema kilele cha maadhimisho hayo kitafanyika Marangu, mkoani Kilimanjaro, huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango .


Alisema maadhimisho ya jubilee ya miaka 50 ya mlima Kilimanjaro ni utaratibu wa kawaida wa Tanapa kufanya katika hifadhi zake pindi sinapo timiza miaka 25 au 50 na hii ni baada ya kufanya maadhimisho kama hayo ya miaka 60 ya Hifadhi ya taifa ya Serengeti


"Kilele cha maadhimisho ya Mlima kilimanjaro kitafanyika Marangu Mkoani Kilimanjaro yalipo makao makuu ya Mlima huo huku makamu wa rais dkt Philip Mpango akitarajiwa kuwa mgeni rasmi " alibainisha


Alisema mlima huo wenye urefu wa kilometa 5,895 ulianzishwa rasmi kama hifadhi ya Taifa Kilimanjaro , Machi 16, Mwaka 1973 kwa ajili ya shughuli za utalii.
Share:

Tuesday, 21 February 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO FEBRUARI 22,2023









Share:

WANANCHI DUGUSHILU WATEMA NYONGO MBELE YA DC MKUDE.... "HAKUNA MIUNDOMBINU, TUMEDANGANYWA SANA"

Wakazi wa kijiji cha Dugushilu kata ya Igaga wilayani Kishapu wakiwa kwenye mkutano wa hadhara

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude akizungumza na wananchi wwa kijiji cha Dugushilu kata ya Igaga wilayani Kishapu

Na Sumai Salum - Kishapu

Wananchi wa kijiji cha Dugushilu kata ya Igaga wilayani Kishapu wamemuomba mkuu wa wilaya hiyo , Joseph  Mkude kuwasaidia  kutatua kero zao kwa haraka kwani zimesababisha kuchelewa kwa maendeleo kijijini hapo.


Wametoa ombi hilo Jana Februari 20, 2023 kwenye mkutano wa hadhara wa kuzungumza masuala ya maendeleo ya kijiji na Kata ambapo wamesema kuwa kumekuwa na ahadi zisizotekelezeka kwa viongozi mbalimbali waliopita hapo kuhusu utatuzi wa changamoto ya miundombinu ya barabara,zahanati ya kijiji,umeme pamoja na maji.

Mkazi wa kijiji hicho, Agnes Ng'ombeyapili amesema kuwa ujio wa mkuu wa wilaya  unawapa imani kuwa atafuatilia utatuzi wa changamoto ya ukosefu wa maji na umeme kiasi ambapo ukosefu wa maji kuhatarisha uhai wao na afya ya ndoa.


 "Mkuu wetu wa wilaya tunamashukuru umefika hapa ujue wagombea wakija wamekuwa wakitoa ahadi bila kutekeleza tunaambiwa tutaletewa umeme tunapiga vigeregere,tunawatandikia hadi vitenge vyetu chini wanavikanyaga lakini hamna kitu na kuhusu swala la ukosefu wa maji tunaamka saa 10 usiku na fisi ni wengi lakini kwa kuwa hatuna visima vya kudumu hatuna namna zaidi ya kukabiliana nao kwa kujificha ili tupate maji", amesema Agnes.


Aidha wakati akichangia hoja ya miundombinu ya barabara Bw. Julius Joseph amesema kuwa Dugushilu wamefanywa  kijiji cha kuchukulia Kura kwa sababu kwa muda mrefu wanaambiwa kuletewa barabara hadi leo hakuna barabara ya kuelekea makao makuu ya wilaya(Mhunze) hakuna barabara la uhakika  kuelekea Ukenyenge na hata Uchunga.


"Kuna jengo la zahanati tuliambiwa tujenge na serikali itamalizia mpaka sasa hakuna kilichofanyika zaidi limegeuzwa kuwa jumba la taka sasa kama na wewe umekuja kuzungumza tu na usifanye utekelezaji sawa hatuna jinsi lakini bado tunaimani na wewe utatekeleza", ameongeza Joseph.


Naye Ndunguli Salula  mbali na kumpomgeza Mkude  kuwa  DC wa kwanza kufika kwenye mkutano wa hadhara kijijini hapo, amesema kuwa wamechoshwa na propoganda za wanasiasa kuwaahidi kuwaletea maendeleo na baadae wakiwauliza sababu ya kucheleweshwa wanasema serikali itafanya baadae hivyo ni bora wanasema ukweli mapema ili wawe huru.

 

Hata hivyo Diwani wa Kata hiyo ya Igaga Mhe. James Kamiga alimaarufu BONYA'S amesema, amekuwa akisumbua ofisi za Tarura,Tanesco,Mipango na ofsi ya Maji na wameahidi utekelezaji kufanyiwa haraka ambapo tayari wamepokea Shilingi milion 50 kutoka ofisi ya mipango ili kumalizia  jengo la zahanati na mahali ambapo hapajakamilika wananchi watajitahidi kukamilisha kwa sababu ni huduma muhimu kwao hivyo wakati wa utekelezaji miradi hiyo ya kimikakati mwananchi yoyote asizuie shughuli za utekelezaji.


Kwa upande wake Mkuu wa wilaya Kishapu, Joseph Mkude amewahakikishia wananchi wa Dugushilu  kuwa serikali ya awamu ya sita inawahakikishia kuwasogezea huduma kwa kushirikina na wananchi hivyo wawe na utayari kutoa maeneo kwa ajili ya ujenzi wa shule ili kupunguza changamoto ya watoto kutembea umbali mrefu na watambue kuwa hakutakuwa na fidia iwapo nguzo za umeme,Bomba za maji na huduma zingine za jamii zikipita kwenye maeneo yao.

 

Sambamba na hayo Mkude amechangia kiasi ya shilingi laki nne 400,000 kwa ajili ya ukamilishaji boma la zahanati ya kijiji pamoja na ujenzi wa shule ya msingi kijijini hapo.



Share:

Video : NTEMI OMABALA - EVA

Share:

MUUGUZI AKAMATWA TUHUMA ZA KUBAKA WAGONJWA WAJAWAZITO


Polisi nchini Uganda wamemkamata muuguzi kwa tuhuma za kubaka na jaribio la kuwabaka wagonjwa wawili wajawazito katika Hospitali ya Entebbe Grade B.

Muuguzi huyo aliye mafunzo alikamatwa Jumamosi, Februari 18, jioni na kwa sasa anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Entebbe Central.

Naibu Msemaji wa Polisi wa Jiji la Kampala, Luke Owoyesigire alisema mshukiwa, Kutesa Denis, alikuwa akiwatambua waathiriwa wake kutoka wodi ya Wanawake.

Kisha aliwawekea dawa ya kuwapoteza fahamu inayoshukiwa kuwa chloroform kabla ya kuwanyanyasa kingono.

"Dawa inayoshukiwa kuwa ya chloroform ilipatikana kutoka kwa makazi yake katika hospitali hiyo, na barua ikapatikana ambapo aliomba kuombewa dhidi ya mawazo machafu aliyokuwa nayo," Owoyesigyire alisema kwenye taarifa, akiwataka waathiriwa wengine kujitokeza, akisema kwamba inawezekana mtuhumiwa aliwanyanyasa wanawake wengine.

Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Peterson Kyebambe alisema kuwa tukio hilo sasa limewachochea kuongeza tahadhari na na kuimarisha usalama kwa kufunga kamera zaidi za CCTV.

Via: Tuko News
Share:

UNAWEZA KUONGEZA MAUZO MARA MBILI KATIKA BIASHARA YAKO KWA KUFANYA HILI!




Naitwa Saidi, sasa ni miaka 10 nafanya biashara lakini haijawahi kuwa rahisi hata mara moja kwani changamoto ambazo nimekuwa nikikumbana nazo ni nyingi sana hadi kuna wakati ulifikia nikaanza kukataa tamaa.

Nimekuwa nikifanya biashara ambayo nashukuru kipato ambacho nimekuwa nikipata kinaniwezesha kumudu gharama za maisha ya kila siku.

Biashara yangu ya kuuza vyakula vya mifugo inaniwezesha kuitunza familia vizuri, kusomesha watoto wangu, kuwasaidia wazazi wangu na kufanya mambo mengine ya kimaendeleo kama kujenga na kununua mashamba kwa ajili ya uwekezaji wa hapo baadaye.

Hata hivyo ghafla wateja walinikimbia licha ya kuwa na bidhaa nzuri na zaidi nilikuwa tayari najulikana na watu wengi lakini wote wakawa hawanunui tena kwangu bali kwa wafanyabiashara wenzangu wa jirani.

Jambo hilo lilinifanya nianze kufikiriki kuna mchezo umefanyika dhidi ya biashara yangu maana nilikuwa sijaiwekea kinga licha ya kusikia watu wakisema biashara lazima iwekewe kinga.

Mara moja nilianza kumtafuta mtaalamu ambaye anaweza kutoa kinga ya kuaminika dhidi biashara yangu, nilitafuta kwa muda bila mafanikio hadi pale nilifanikiwa kumpata Dr. Kiwanga,

Nilimpigia Dr. Kiwanga na kumuelezea kuwa biashara yangu imevamiwa na inahitaji ulinzi wa mara moja kwani wateja wangu wamekimbia wote.

Nashukuru Dr. Kiwanga alinielewa na kunifanyia tiba na kuniambia ndani ya siku tatu nitapata majibu ya jambo hilo.

Ukweli ndani ya siku tatu wateja walianza kuja kwenye biashara yangu kama ilivyokuwa hapo awali, cha kushangaza zaidi ni kwamba niliiuza kuliko ilivyokuwa mwanzo.

Na sasa biashara yangu inaenda vizuri hadi majirani zangu wanatamani kujua ni kipi hasa nimefanya, hawa ndio waliovamia biashara yangu kwa uganga wao lakini safari hii nimefanikiwa kuwakomesha vilivyo.

Mauzo yangu yameongezeka mara tatu ya ilivyokuwa mwanzo, sikuwahi kutarajia jambo kama hili.

Ukiachana na hayo, Dr. Kiwanga ana uwezo wa kukuwezesha kuwa mtu wa bahati maishani, kushinda bahati nasibu kukukinga na maadui zako na mengineo. Kwa maelezo zaidi wasiliana nao kupitia barua pepe kiwangadoctors@gmail.com ama kwenye wavuti www.kiwangadoctors.com na namba ya simu +254 769404965.



Share:

Monday, 20 February 2023

PJFCS, POLISI, OFISI YA RC WATOA MSAADA WA VIFAA TIBA, VYAKULA LISHE KUNUSURU AFYA ZA WATOTO WENYE UTAPIAMLO


Kikundi cha mazoezi (PJFCS), Polisi na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wakiwa katika Hospitali ya Rufaa leo wakitoa masaada wa vifaa tiba, vyakula lishe kwa ajili ya kunusuru Afya za watoto wenye Utapiamlo, kupata miti na kuchangia damu.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

KIKUNDI cha mazoezi cha Polisi Jamii Fitness Center (PJFCS) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, wametoa msaada wa vifaa tiba na vyakula lishe kwa ajili ya kunusuru afya za watoto wenye Utapiamlo.

Msaada huo wa vifaa tiba na vyakula lishe kwa ajili ya kunusuru afya za watoto wenye utapiamlo, vimetolewa leo Februari 20, 2023 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, ikiwa ni malengo waliojiwekea ya kuanzisha Mbio za Shinyanga Madini Marathon ili kunusuru afya za watoto wenye Utapiamlo.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Shinyanga Madini Marathon Roland Mwalyambi, amesema Kauli mbiu ya mbio hizo za Shinyanga Madini Marathon ili kuwa ni 'Kimbia kwa afya saidia watoto wenye Utapiamlo', kwamba fedha ambazo watazipata zitakwenda kununua vifaa tiba na lishe kwa ajili ya kuokoa afya za watoto wenye utapiamlo.

“Mbio za Shinyanga Madini Marathon zilifanyika mwaka 2022 na fedha ambazo tulizipata tumenunua vifaa tiba na vyakula lishe kwa ajili ya kuokoa afya za watoto wenye Utapiamlo na leo tumevikabidhi hapa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga,"amesema Mwalyambi.

Naye Mlezi wa kikundi hicho cha mazoezi cha Polisi Jamii, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ACP Janeth Magomi, amesema uokoaji wa afya kwa watoto wenye utapiamlo ni faida kwa taifa, kwa sababu litapata vijana wenye akili na kuwa viongozi wazuri wa baadae.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dk. Kambi Buteta, ameshukuru kupewa vifaa tiba na vyakula lishe ambayo alisema vitakuwa msaada mkubwa kunusuru afya za watoto wenye Utapiamlo.

Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto Dk. Yustina Tizeba, alisema tatizo la watoto wenye utapiamlo mkoani humo ni kubwa, lakini linaweza kuzuilika endapo wajawazito wakazingatia suala la lishe bora kipindi cha ujauzito wao.

Aidha, kikundi hicho cha mazoezi Polisi jamii wakiongozwa na mlezi wao Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ACP Janeth Magomi, wakiwa katika Hospitali hiyo pia walipanda Miti 100, pamoja na kuchangia damu salama.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa tiba na vyakula lishe kwa ajili ya kunusuru afya za watoto wenye Utapiamlo.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dk. Kambi Buteta akizungumza kwenye makabidhiano ya vifaa tiba na vyakula lishe kwa ajili ya watoto wenye Utapiamlo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Shinyanga Madini Marathon Roland Mwalyambi, akizungumzia utekelezaji wa ahadi yao ya kutoa msaada wa vifaa tiba na vyakula lishe kwa ajili ya kuokoa afya za watoto wenye Utapiamlo.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi (kushoto) ambaye ni Mlezi wa kikundi cha mazoezi cha PJFCS, akikabidhi vifaa tiba na vyakula lishe kwa ajili ya kuokoa afya za watoto wenye Utapiamlo, (kulia) ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga Dk. Kambi Buteta.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi (kushoto) ambaye ni Mlezi wa kikundi cha mazoezi cha PJFCS, akikabidhi vifaa tiba na vyakula lishe kwa ajili ya kuokoa afya za watoto wenye Utapiamlo, (kulia) ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga Dk. Kambi Buteta.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi (kushoto) ambaye ni Mlezi wa kikundi cha mazoezi cha PJFCS, akikabidhi vifaa tiba na vyakula lishe kwa ajili ya kuokoa afya za watoto wenye Utapiamlo, (kulia) ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga Dk. Kambi Buteta.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi (katikati) akiongoza zoezi la uchangiaji damu.
Uchangiaji damu ukiendelea.
Uchangiaji damu ukiendelea.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi (kulia) akizundua bustani ya matunda.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akiongoza zoezi la upandaji miti ya matunda katika eneo la Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga.
Zoezi la upandaji miti ya matunda likiendelea.
Zoezi la upandaji miti ya matunda likiendelea.
Zoezi la upandaji miti ya matunda likiendelea.
Zoezi la upandaji miti ya matunda likiendelea.
Zoezi la upandaji miti ya matunda likiendelea.
Zoezi la upandaji miti ya matunda likiendelea.
Zoezi la upandaji miti ya matunda likiendelea.
Picha ya pamoja ikipigwa.
Picha ya pamoja ikipigwa.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger