Kiwanda cha kutengeneza Magodoro chateketea Moto
Mwenyekiti wa kikundi cha vijana cha kutengeneza Magodoro Ally John akionyesha namna Kiwanda chao kilivyoteketea na Moto.
Mwenyekiti wa kikundi cha vijana cha kutengeneza Magodoro Ally John akionyesha namna Kiwanda chao kilivyoteketea na Moto.
*****
KIWANDA cha kutengeneza Magodoro cha vijana wajasiriamali ambacho kipo Mtaa wa Viwandani Manispaa ya Shinyanga kimeteketea na moto.
Vijana hao wajasiriamali ni wanufaika wa mikopo fedha za mapato ya ndani ya halmashauri asilimia 10, ambazo hutolewa kwa wanawake na vijana asilimia nne na watu wenye ulemavu asilimia mbili.
Mwenyekiti wa kikundi hicho cha vijana cha kutengeneza Magodoro Ally John, akizungumza jana Kiwandani hapo, amesema Kiwanda chao kimeungua moto Februari 5 mwaka huu majira ya saa 8 usiku na kuteketeza kila kitu.
“Thamani ya mali zote ambazo zimeteketea kwenye Kiwanda chetu cha kutengeneza Magodoro ni Sh. Milioni 93 na tulikuwa na Oda ya Magodoro 282 ambayo ilikuwa kesho yake tuyapeleke Mwanza na Tabora na tulikuwa na Pikipiki mpya ndani ya kiwanda, vitu vyote vimeteketea hakuna ambacho kimeokolewa,”amesema John.
Aidha, amesema kikundi chao kinawezeshwa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa kupewa mikopo, kwamba walianza kupewa mwaka 2017 kiasi cha fedha Sh. Milioni 15 wakarejesha fedha zote, na mwaka wa fedha (2020/2021) wakapewa tena Sh.milioni 40 na walikuwa wamerejesha Sh.milioni 10 na sasa Kiwanda kimewaka Moto.
Amesema kikundi chao kina vijana 10 na sasa hawana ajira na hawajui hatimaye yao, sababu bado wanadeni la kurejesha mkopo wa halmashauri kiasi cha fedha Sh.milioni 30 na Kiwanda ndiyo kimeteketea moto, na kuiomba halmashauri ione namna ya kuwanyanyua tena.
Naye Ofisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga John Tesha, amesema.....