Sunday, 22 January 2023

MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA YAZINDULIWA SHINYANGA


Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati akizindua Wiki ya Sheria Mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Januari 22,2023


Na Marco Maduhu, SHINYANGA

WANANCHI wa Mkoa wa Shinyanga, wametakiwa kutumia fursa madhimisho ya wiki ya sheria, kujitokeza kwa wingi kupata elimu ya sheria na msaada wa kisheria bure, ili kufahamu namna ya kupata haki zao kwa mujibu wa sheria.


Maadhimisho hayo ya Sheria hapa nchini yameanza leo Januari 22 na yatahitimishwa Februari 1 mwaka huu, ambapo katika Mkoa wa Shinyanga kutakuwa na utoaji wa elimu ya sheria na kupatiwa msaada wa kisheria bure, na usikilizwaji  kero mbalimbali na kutafutiwa ufumbuzi, ambayo itakuwa ikitolewa katika viwanja vya Zimamoto vilivyopo Nguzonane Manispaa ya Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, ametoa wito huo wakati akifungua maadhimisho ya wiki ya sheria mkoani Shinyanga kwa niaba ya Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Yahaya Nawanda ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo, amewataka wananchi wa Mkoa wa Shinyanga watumie fursa kwenye maadhimisho hayo ya wiki ya Sheria kupata elimu na msaada wa kisheria bure pamoja na kupata ufumbuzi wa matatizo yao.

Katika hatua nyingine Mkude amewataka wananchi wanapokuwa na matatizo ya migogoro, wasikimbile tu mahakamani, bali waitatue kwa njia ya usuluhishi na kuleta amani, pamoja na kutopoteza muda kwa kufanya shughuli za uzalishaji kwa kuhudhuria mahakamani kila mara.

Alitoa wito pia kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga, wajitokeze kwa wingi kwenye mabanda katika wiki hiyo ya Sheria, ili wapate elimu mbalimbali za msaada wa kisheria, na kupata haki zao kwa mujibu wa Sheria.

Aidha, aliwataka watumishi wa mahakama kufanya kazi zao kwa weledi, kuzingatia maadili ya utumishi wa umma, sheria, kanuni na miongozo ya Serikali kwa watumishi wa umma, ili kutoa haki sawa kwa wananchi katika utatuzi wa migogoro yao.

“Natoa Rai kwa wananchi kila wanapokuwa na migogoro wasikimbile Mahakamani, bali waitatue kwa njia ya usuluhishi na kuleta amani, na ile ambayo itashindikana ndipo waipeleke mahakamani,” alisema Mkude.

“Natoa Rai kwa wananchi kila wanapokuwa na migogoro wasikimbile Mahakamani, bali waitatue kwa njia ya usuluhishi na kuleta amani, na ile ambayo itashindikana ndipo waipeleke mahakamani,” amesema Mkude.

Aidha, amewataka watumishi wa mahakama kufanya kazi zao kwa weledi, kuzingatia maadili ya utumishi wa umma, sheria, kanuni na miongozo ya Serikali kwa watumishi wa umma, ili kutoa haki sawa kwa wananchi katika utatuzi wa migogoro yao.

Naye Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Athumani Matuma, alikazia suala la utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi, na kueleza kuwa ni njia ambayo itapunguza pia mrundikano wa kesi mahakamani, sababu kuna kesi nyingine siyo za kupelekwa mahakamani bali zinahitaji usuluhishi.

Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya wiki ya Sheria inasema, umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kukuza uchumi endelevu wajibu wa mahakama na wadau.


Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya sheria mkoani Shinyanga.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Athumani Matuma akizungumza kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya sheria mkoani Shinyanga.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Athumani Matuma, (kushoto) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Sheria mkoani Shinyanga.

Uzinduzi maadhimisho ya wiki ya Sheria mkoani Shinyanga yakiendelea.

Uzinduzi maadhimisho ya wiki ya Sheria mkoani Shinyanga yakiendelea.

Uzinduzi maadhimisho ya wiki ya Sheria mkoani Shinyanga yakiendelea.

Uzinduzi maadhimisho ya wiki ya Sheria mkoani Shinyanga yakiendelea.

Uzinduzi maadhimisho ya wiki ya Sheria mkoani Shinyanga yakiendelea.

Uzinduzi maadhimisho ya wiki ya Sheria mkoani Shinyanga yakiendelea.

Uzinduzi maadhimisho ya wiki ya Sheria mkoani Shinyanga yakiendelea.

Uzinduzi maadhimisho ya wiki ya Sheria mkoani Shinyanga yakiendelea.

Uzinduzi maadhimisho ya wiki ya Sheria mkoani Shinyanga yakiendelea.

Uzinduzi maadhimisho ya wiki ya Sheria mkoani Shinyanga yakiendelea.

Picha za pamoja zikipigwa kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya sheria mkoani Shinyanga.

Picha za pamoja zikipigwa kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya sheria mkoani Shinyanga.
Picha za pamoja zikipigwa kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya sheria mkoani Shinyanga.
Maandamano yakiendelea kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya sheria mkoani Shinyanga.

Maandamano yakiendelea kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya sheria mkoani Shinyanga.

Maandamano yakiendelea kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya sheria mkoani Shinyanga.

Maandamano yakiendelea kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya sheria mkoani Shinyanga.

Maandamano yakiendelea kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya sheria mkoani Shinyanga.

Share:

UHAMIAJI WATUMIA WIKI YA SHERIA SHINYANGA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI....ANGUMBWIKE AHAMASISHA MATUMIZI YA MTANDAO

Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga, Mrakibu wa Uhamiaji Lydia Angumbwike (kulia) akielezea huduma zinazotolewa na Jeshi la Uhamiaji wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Sheria Mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Januari 22,2023 katika Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga. Wa tatu kushoto ni Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude, wa pili kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Athumani Matuma wakiwa katika banda la Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga.


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga limeshiriki Maadhimisho ya Wiki ya Sheria Mkoa wa Shinyanga kwa kutoa elimu juu ya huduma wanazotoa ikiwemo Utoaji Pasipoti, Vibali vya Ukaazi, Vibali vya kuingia nchini (Visa),kudhibiti uhamiaji haramu, kuendesha kesi za uhamiaji haramu pamoja na kupokea maombi ya uraia.

Maadhimisho ya Wiki ya Sheria Mkoani Shinyanga yamezinduliwa rasmi leo Jumapili Januari 22, 2023 katika Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Maadhimisho ya Wiki ya Sheria mwaka 2023 iliyoanza leo nchini na kutarajiwa kuhitimishwa Februari 1,2023 yanayoongozwa na kauli inayosema, “Umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kukuza uchumi endelevu wajibu wa mahakama na wadau”.

Akizungumza wakati wa Maadhimisho hayo, Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga, Mrakibu wa Uhamiaji Lydia Angumbwike amesema wanatumia fursa ya maadhimisho ya Wiki ya Sheria kutoa elimu kwa jamii kuhusu huduma zinazotolewa Uhamiaji ambazo ni pamoja na kukagua Fomu za maombi ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) sambamba na huduma ya uendeshaji wa kesi zinazohusu wahamiaji haramu na kupokea maombi ya uraia wa Tanzania.


Angumbwike amezitaja huduma zingine wanazotoa kuwa ni Utoaji wa Hati ya Kusafiria (Pasipoti), huduma ya vibali vya ukaazi, vibali vya kuingia nchini (Visa) na huduma ya kudhibiti wahamiaji haramu.

Angumbwike amesema pia Uhamiaji inatoa Huduma kwa njia ya Mtandao (Tanzania E-Immigration Online Portalhivyo kuwahamasisha wananchi kutumia fursa ya Mtandao kupata huduma zinazotolewa Uhamiaji.


"Mfumo wa Passport kwa njia ya mtandao ni huduma mpya inayomuwezesha muombaji kujaza Fomu ya Maombi ya Pasipoti kwa njia ya Kielektroniki akiwa mahali popote. Baada ya kujaza fomu hiyo, atatakiwa kuichapisha (Print) na kuiwasilisha pamoja na vielelezo vingine katika Ofisi ya Uhamiaji iliyo karibu naye kwa ajili ya kushughulikiwa maombi yake ya Pasipoti",amesema Angumbwike.
Akizungumza wakati akifungua maadhimisho hayo, Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude amewataka wananchi wa Mkoa wa Shinyanga watumie fursa ya maadhimisho hayo ya wiki ya Sheria kupata elimu na msaada wa kisheria bure na kupata ufumbuzi wa matatizo yao.
Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga, Mrakibu wa Uhamiaji Lydia Angumbwike (kulia) akielezea huduma zinazotolewa na Jeshi la Uhamiaji wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Sheria Mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Januari 22,2023 katika Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga. Wa tatu kushoto ni Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude, wa pili kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Athumani Matuma wakiwa katika banda la Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga.
Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga, Mrakibu wa Uhamiaji Lydia Angumbwike (kulia) akielezea huduma zinazotolewa na Jeshi la Uhamiaji wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Sheria Mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Januari 22,2023 katika Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga. 
Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga, Mrakibu wa Uhamiaji Lydia Angumbwike (kulia) akielezea huduma zinazotolewa na Jeshi la Uhamiaji wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Sheria Mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Januari 22,2023 katika Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga. 
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati akizindua Wiki ya Sheria Mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Januari 22,2023
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati akizindua Wiki ya Sheria Mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Januari 22,2023
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Athumani Matuma akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Sheria Mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Januari 22,2023
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Athumani Matuma akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Sheria Mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Januari 22,2023
Maafisa mbalimbali wakipiga picha ya kumbukumbu wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Sheria Mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Januari 22,2023.

Picha zote na Kadama  Malunde - Malunde 1 blog


Share:

ZAIDI YA HATI MILKI ZA ARDHI MILIONI MOJA KUTOLEWA KUPITIA MRADI WA LTIP


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza katika semina ya siku moja ya Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 21 Januari 2023.

Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Jesca Msambatavangu akichangia hoja kwenye semina ya siku moja ya Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii na wale wanaotoka halmashauri ambazo Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) unaanza iliyofanyika mkoani Dodoma tarehe 21 Januari 2023.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi Malisili na Utalii Ally Juma Makoa akisisitiza jambo wakati wa semina ya siku moja ya Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 21 Januari 2023.

Mbunge wa Jimbo la Mafinga Cosato Chumi akichangia hoja katika semina ya siku moja ya Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii na wale wanaotoka halmashauri zinazopitiwa na mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 21 Januari 2023.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete akizungumza semina ya siku moja ya Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii na wale wanaotoka halmashauri zinazopitiwa na mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 21 Januari 2023.

Wabunge wakiwa kwenye semina ya siku moja kuhusiana na utekelezaji wa mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 21 Januari 2023.

Mratibu wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) Joseph Shewiyo akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa LTIP kwa wabunge tarehe 21 Januari 2023 jijini Dodoma (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

**************************

Na Munir Shemweta, WANMM

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) inatarajia kutoa Hati Milki za Ardhi milioni moja katika maeneo ya mijini pamoja na Hati Miliki za Kimila laki tano kwenye maeneo ya vijijini.

Aidha, kwa yale maeneo ambayo upangaji wake utaleta ugumu kutokana na ujenzi holela maeneo hayo utambuzi wake utachukuliwa kama ulivyo na Mradi wa LTIP utatoa Leseni za Makazi milioni moja.

Hayo yamebainishwa tarehe 21 Januari 2023 na Mratibu wa mradi wa LTIP Joseph Shewiyo wakati wa semina ya siku moja na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii kujadili utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi iliyofanyika jijini Dodoma.

Alisema, kazi ya utoaji hati miliki kwenye maeneo ya mijini itafanyika kwa kutumia watumishi wa serikali kwa asilimia 20 huku asilimia 80 iliyobaki ikifanywa na makampuni yaliyosajiliwa kufanya kazi ya kupanga na kupima.

‘’Kazi ya mfano (Pilot) imeanza jiji la Dodoma ambapo kata tatu za Mbabala (Bihawana), Nghong’ona (Mapinduzi) na kata ya Mpunguzi (Mkwawa) zimechaguliwa. Aidha, halmashauri nane za Dodoma Jiji, Chalinze, Mafinga, Rungwe, Nzega, Tarime, Korogwe na Kigoma Ujiji ndizo zitakazoanza kwa mwaka wa kwanza wa utekelezaji wa mradi’ alisema Shewiyo

Akielezea upande wa Hati Milki za Kimila, Mratibu huyo wa LTIP alisema, kazi hiyo itafanywa na watumishi wa serikali na taasisi zisizo za kiserikali na kubainisha kuwa kazi itakayofanyika ni pamoja na kuweka mipango ya matumizi bora ya ardhi ya vijiji 250 na utoaji hati milki laki tano za kimila.

Aliwaeleza Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii iliyojumisha pia Wabunge wanaotoka halmashauri ambazo mradi huo utaanza kwa mwaka wa kwanza kuwa, mradi wa LTIP utekelezaji wake utakuwa na shughuli mbalimbali na kuzitaja kuwa ni pamoja na utoaji Hati, maandalizi ya ramani za msingi, uboreshaji mfumo wa ILMIS, Alama za msingi na mifumo ya uthamini sambamba na ujenzi wa ofisi za ardhi za mikoa 25.

‘’Kazi nyingine zitakazofanyika kupitia mradi wa LTIP ni ukarabati wa ofisi za ardhi kwenye halmashauri 41, uboreshaji ofisi za Mabaraza ya Ardhi katika halmashauri 41, ukarabati wa masijala za ardhi za vijiji 250, kuwajengea uwezo watumishi pamoja na uratibu wa masuala ya kijamii na mazingira’’. Alisema Shewiyo.

Kwa upande wao, Wabunge wametaka utekelezaji Mradi huo wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi nchini uende sambamba na utoaji elimu kwa wananchi hasa wanawake pamoja na watendaji wa serikali kuanzia ngazi ya mitaa ili kuleta ufanisi zaidi katika mradi.

Cosato Chumi, Mbunge wa Mafinga Mjini mkoani Iringa ameshauri utekelezaji mradi huo uangalie pia maeneo ya viwanda na kubainisha kuwa sekta hiyo ni muhimu na imeendelea kukua kwa kasi kwenye maeneo mbalimbali.

Mradi wa uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi ni mradi ulio chini ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na utekelezaji wake umeanza Mei, 2022 na unatarajia kukamilika May 2027 (Miaka 5).

Lengo la mradi wa LTIP ni kuboresha ufanisi katika utawala wa ardhi na kuongeza usalama wa milki kwenye maeneo ya mradi. Lengo hilo linaenda sambamba na kuongeza idadi ya miamala itokanayo na nyaraka za umiliki, kupunguza muda unaotumika kupata nyaraka za milki, kuongeza uelewa wa usalama wa milki kwa kuzingatia jinsia, kuongeza idadi ya watanzania wanaomiliki nyaraka za umiliki pamoja na kuongeza ufanisi utakaofanya wamiliki kuridhika na mchakato wa uandaaji nyaraka za umiliki.
Share:

KATAMBI:SERIKALI KUENDELEA KUWAJENGEA VIJANA MAZINGIRA WEZESHI NCHINI

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi akizungumza na uongozi na wanafunzi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini wakati wa hafla ya kuwakaribisha wanafunzi wapya wa mwaka wa masomo 2022/2023, jijini Dodoma.

Sehemu ya wanafunzi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini wakisikiliza maelezo ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kuwakaribisha wanafunzi wapya wa mwaka wa masomo 2022/2023.


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi akimkabidhi cheti cha pongezi Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Hosen Mayaya ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake katika malezi ya wanafunzi wa chuo hicho.


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Patrobasi Katambi akiwa ameshika kombe pamoja na Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Hosen Mayaya (kulia) mara baada ya kukabidhiwa na vijana wa chuo hicho walioshiriki mashindano ya SHIMIVUTA.


Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Hosen Mayaya akieleza jambo wakati wa hafla hiyo.


Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (MISO), Bi. Sayuni Mmari akizungumza wakati wa hafla ya kuwakaribisha wanafunzi wapya wa mwaka wa masomo 2022/2023, Dodoma.

.....................................

Na: OWM – KVAU -DODOMA

Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kutoa kipaumbele na kuweka mikakati mbalimbali ya kuwajenga vijana mazingira wezeshi yatakayo wawezesha kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa na kuwasaidia kujikwamua kiuchumi.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi wakati wa hafla ya kuwakaribisha wanafunzi wapya wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kwa mwaka wa masomo 2022/2023 katika ukumbi wa Mwl. Nyerere uliopo chuoni hapo jijini Dodoma.

Mheshimiwa Katambi amesema, dhamira ya Serikali ni kuwapatia vijana elimu bora na thabiti inayoendana na mazingira yao na kuhakikisha elimu hiyo inawasaidia katika kuhudumia taifa na kuwapatia maarifa yatakayo wawezesha kujiongoza.

“Vijana ndio nguvu kazi ya taifa na Serikali ina matarajio makubwa na kundi hilo kwa kuwa ndio watakaoleta mapinduzi ya ukuaji wa uchumi wa nchi,” amesema

“Endeleeni kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya katika Taifa letu ya kuhakikisha masuala ya vijana yanapewa kipaumbele,”

Ameongeza kuwa, Serikali imeendelea kuweka mikakati endelevu yenye malengo ya kuwezesha vijana ikiwemo kuwapatia mikopo yenye riba nafuu ambayo hutolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, vilevile mikopo inayotolewa na halmashauri mbalimbali zilizopo nchini kupitia mapato ya ndani (4% kwa vijana, 4% wanawake na 2% Watu wenye Ulemavu) ambayo imewezesha vijana kuanzisha na kuendeleza miradi mbalimbali inayowaingizia kipato.

Ameeleza kuwa jitihada nyingine zilizofanyika ni pamoja na kuwezesha vijana kupitia Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi ambayo kupitia mafunzo tarajari (Internship) yanayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Kitengo cha Huduma za Ajira (TaESA) imewezesha wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu kushiriki mafunzo ya uzoefu wa kazi na baadhi ya vijana wameajiriwa na makampuni mbalimbali. Pia, amesema kitengo hicho kimeweza kuwaunganisha vijana na fursa za ajira nje ya nchi ikiwemo wakati wa kombe la dunia.

Vile vile, ameeleza namna vijana nchini walivyoweza kunufaika na fursa mbalimbali za ajira kupitia miradi ya kimakakati inayoendelea kutekelezwa nchini.

Aidha, Naibu Waziri Katambi amewataka vijana hao kutambua wajibu walionao na kuwa na tabia njema ili waweze kufanikiwa sambamba na kutimiza malengo yao.

Naye, Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Hosen Mayaya, ameshukuru Serikali kwa kuendelea kuwezesha sekta ya elimu nchini ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika kukomboa taifa.

Kwa upande wake, Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (MISO), Bi. Sayuni Mmari ameeleza kuwa wanafunzi wa chuo hicho wataendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali.
Share:

Saturday, 21 January 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JANUARI 22,2023

Share:

KUNA ONGEZEKO LA ZAIDI YA TANI 70,000 ZA SUKARI NCHINI - DKT. ASHIL


Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na biashara Dkt. Hashil Abdalah akizungumza katika kikao na wadau wa uzalishaji wa sukari chini kilicholenga kufahamu hali ya uzalishaji wa sukari nchini kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi za TIC Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Kilombero Sugar Company Guy Williums akizungumia hali ya uzalishaji wa Sukali katika kiwanda hicho alipokuwa akiwasilisha salamu zake kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdalla katika kikao hicho Jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa chama cha wazalishaji wa sukari Tanzania, Seif. A. Seif (wa pili kushoto) akizungumzia hali ya upatikanaji wa Sukari nchini apokuwa akitoa taarifa ya uzalishaji wa Bidhaa hiyo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdalla katika kikao hicho Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Msaidizi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gungu Mibavu akipongeza jitihada zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita katika kuhamisha uzalishaji wa Sukari hapa nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Dkt. Ashil Abdalla (katikati aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe waliohudhulia mkutano.

(PICHA NA HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, DSM

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amesema kuwa uzalishaji wa sukari nchini umeongezeka hadi kufikia zaidi ya tani 70,000 na kufanya kuwa na zaidi ya tani 160,000 kwenye maghala katika kipindi cha 2022 /2023 na kupunguza kwa kiasi kikibwa uhaba wa sukari nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji katika kikao na wadau wa uzalishaji wa sukari chini kilicholenga kufahamu hali ya uzalishaji wa sukari nchini, Dkt. Abdalah amesema Serikali inaendelea kuhakikisha uwepo wa uwekezaji mkubwa katika sekta hiyo Ili kuleta tija kwa Taifa zima.

“Mwaka huu tumeingiza uzalishaji wa sukari wa kiwanda kipya cha bagamoyo ambao umepelekea uzalishaji wa sukari kwa ujumla wake kuongezeka kuliko hata ule wa mwaka jana, hii inapelekea mazungumzo haya kuendelea mara kwa mara” Ameongeza.

Ameeleza kuwa mafanikio hayo ya kuongezeka kwa uzalishaji wa sukari ni kutokana na jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani katika kuhamasisha uzalishaji na uwekezaji kwenye Sekta hiyo.

“Rais Samia mara kadhaa amekuwa akiweka wazi kuwa Tanzania inawahitaji wawekezaji katika Sekta mbalimbali na yeye mwenyewe kusimamia kwa vitendo kuhakikisha wawekezaji wanaongezeka” ameeleza Dkt. Abdallah.

Aidha amewahakikishia wakulima wa zao la miwa kuwa sasa changamoto zao za kupata masoko zimepata ufumbuzi kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa sukari.


Kwa upande Mwenyekiti wa Chama cha Wazalishaji wa Sukari Tanzania, Seif. A. Seif, amesema kuwa ongezeko kubwa la sukari linaonesha nchi ina sukari ya kutosha hivyo imekuwa faraja kubwa kwa Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwani alikuwa na azma ya kutaka nchi ijitosheleze kwa uzalishaji wa sukari.


Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gungu Mibavu, amesema kutokana na ongezeko la uzalishaji wa sukari nchini, inaonesha kwamba jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika kuhamasisha uzalishaji na uwekezaji kwenye tasnia hiyo unazaa matunda.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger