Saturday, 14 January 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JANUARI 15,2023










Share:

AJALI YA LORI, GARI DOGO YAUA WATU WANNE MOROGORO

 


Watu wanne wamefariki dunia kufuatia ajali ya lori na gari dogo aina ya Toyota Spacio katika eneo la Kwambe Dumila wilayani Kilosa mkoani Morogoro na kusababisha barabara kufungwa kwa saa kadhaa.


Akizungumza na Mwananchi Digital kwa simu leo Januari 14 Mkuu wa wilaya ya Kilosa, Majid Mwanga amesema gari hilo ndogo lilikuwa na watu sita akiwemo dereva ambaye ni mtumishi wa Serikali.

SOMA HAPA ZAIDI Chanzo Mwananchi.
Share:

KIATU KINAVYO TAMBULISHA HADHI YA MWANAUME MTANASHATI



Na Dotto Kwilasa.

Kila mwanaume anahitaji kuwa na mwonekano wa kipekee machoni pa watu bila kujali ni wakati gani au mahali gani..na hii ni kwa wanaume wa kisasa,wanaoenda na wakati .

Mwonekano wa mwanaume huanzia pale chini kabisa kwenye miguu upande wa viatu ,haijalishi ukubwa wa bei ya kiatu husika kinachotazamwa zaidi ni ubora na dizaini ya kiatu na mapenzi ya mtumiaji mwenyewe.

Wanawake wengi wamekuwa wakivutiwa na wanaume wenye hadhi fulani ivi ya kisasa kwa kuzingatia mtazamo wa uvaaji wa viatu vizuri,vyenye hadhi na muonekano wa kuvutia.

Ngoja nikuibie Siri,kuna siku nikiwa kwenye harakati zangu za maisha nilikutana na wadada wakizungumza kuhusu muonekano mzima wa mwanaume kuwa mara nyingi wao huvutiwa zaidi na kiatu .

Yani mwanamke anapokutana na mwanaume njiani kitu cha kwanza anachozingatia kabla ya mambo mengine ni kiatu,anaangalia kiatu kina hadhi??…kama mwanaume hajijali hata akiwa na mwanamke wake hawezi kumjali..

Wanawake wanazingatia zaidi upekee wa mwanaume kuanzia viatu kabla ya muonekano mwingine kama mavazi,pafyumu namna anavyonyoa,anavyo zungumza na mwendo wake..

Kwa kifupi tu sio kila kiatu ni kiatu,mwanaume unapaswa kuzingatia katika utaratibu wako wa mitoko hukosi viatu vya matukio tofauti tofauti mfano kwenye sherehe,mitoko ya kawaida, kazini na safarini,namaanisha kiatu unachovaa kiendane na unachoenda kukifanya kwa wakati huo.


Cha kuzingatia zaidi unapaswa kwenda na wakati bila kujali nafsi yako inapenda Nini..kikubwa hapa ni kwenda na wakati na kuwa na mvuto wa kidigitali . 




Share:

WANAFUNZI WANNE PEKEE KATI YA 88 WARIPOTI KIDATO CHA KWANZA


Wanafunzi wanne kati ya 88 waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza katika shule ya Sekondari Izumachel iliyopo wilayani Geita

Ikiwa wiki moja imepita tangu kuanza kwa msimu wa masomo mwaka 2023 Tanzania, wanafunzi wanne kati ya wanafunzi 88 waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Izumachel iliyopo wilayani Geita mkoani hapo ndio walioripoti katika shule hiyo.

Shule hiyo iliyoanza mwaka 2022 ikiwa na wanafunzi 40 wa kidato cha pili hadi sasa walioripoti na kuanza masomo ni wanafunzi 26 na kufanya shule nzima kuwa na wanafunzi 30 kati ya 128 walioachaguliwa kujiunga na shule hiyo.


chanzo Mwananchi
Share:

DC MWENDA KUANZISHA MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU IRAMBA


Na Mwandishi wetu,Iramba-Singida.

Wilaya ya Iramba mkoani Singida  imejipanga kuanza mashindano ya mpira wa miguu ili kuwakutanisha vijana pamoja na kuimarisha afya zao, kutambua vipaji vyao na kuviendeleza.

Mashindano hayo yanaratibiwa na Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida Suleiman Mwenda huku yakiwa yanatarajiwa kuanza mapema mara baada ya msimu wa kilimo kumalizika.

Mwenda amebainisha hayo jana tarehe 13 Januari 2023 wakati akizingumza na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya WazoHuru Media Group Limited  Mathias Canal aliyemtembelea ofisini kwake Mjini Kiomboi,Singida.

Amesema kuwa Ligi ya mpira wa miguu ambayo ina lengo la kuimarisha sekta ya michezo Wilayani hapo na kuwakutanisha vijana itasaidia kutengeneza mahusiano imara na madhubuti katika msingi wa maendeleo kwa mtu mmoja mmoja na Wilaya kwa ujumla wake.

"Nawasihi wananchi na wadhamini mbalimbali kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha dhamira hii katika kuimarisha sekta ya michezo na kufanikisha kuanza na kumalizika kwa mashindano hayo,michezo ni furaha,amani na upendo,"amesisitiza.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya WazoHuru Media Group Limited Mathias Canal amempongeza Mkuu huyo wa Wilaya kwa kujipanga kuanzisha mashindano hayo ambayo yatakuwa chachu ya kuitangaza Wilaya ya Iramba na sekta ya uwekezaji.

Amesema kuwa Wilaya ya Iramba ina maeneo mengi mazuri na ardhi ya kutosha kwa ajili ya uwekezaji katika sekta ya Kilimo, Elimu, Mifugo na Uvuvi ikiwa ni pamoja na sekta ya Viwanda.


Share:

CMSA YATOA NENO UORODHESHWAJI HATIFUNGANI YA BENKI YA KCB



Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA),CPA Nicodemus Mkama

***
MAMLAKA ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) imesema uorodheshwaji wa hatifungani ya Benki ya KCB yaani KCB Fursa Sukuk, ni miongoni mwa sehemu ya maendeleo katika sekta ya fedha hapa nchini na inaweka historia ya kuwa hatifungani ya kwanza inayokidhi misingi ya Shariah kutolewa kwa umma na kuorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam, na ambayo imeidhinishwa na Mamlaka hiyo.


Akizungumza Januari 13,2023 jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuorodheshwa kwa hatifungani inayokidhi misingi ya shariah kwenye soko la hisa la Dar es Salaam ,Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka hiyo Nicodemus Mkama amesema Oktoba 25, 2022 CMSA ilidhinisha Benki ya KCB kuuza hatifungani inayokidhi misingi ya shariah.

"Yaani KCB Fursa Sukuk, yenye thamani ya Sh. bilioni 10 na ongezeko la Sh.bilioni 5.Idhini ilitolewa na CMSA baada ya Benki ya KCB kukidhi matakwa ya Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana Sura ya 79 ya Sheria za Tanzania. Pia na Miongozo ya Masoko ya Mitaji na Dhamana ya Utoaji wa Hatifungani ya mwaka 2019 ambapo pamoja na mambo mengine, KCB ilitakiwa kuwa, Waraka wa Matarajio wa utoaji wa hatifungani ya Fursa Sukuk.

"Kuidhinishwa na Bodi ya Ushauri wa Shariah (Shariah Advisory Board) ya benki ya KCB na kupata ithibati kutoka kwa kampuni yenye utaalam kuhusu uwekezaji unaokidhi Misingi ya Shariah.Benki ya KCB ilikidhi matakwa haya kwa kuwa na Bodi ya Ushauri wa Shariah ambayo ni KCB Sahl Shariah Advsory Board na ithibati ilitolewa na Kituo cha ushauri kuhusu uwekezaji unaokidhi Misingi ya Shariah."

Amesema Mauzo ya hatifungani ya Fursa Sukuk yalifunguliwa Novemba 9, 2022 na kufungwa Desemba 5 , 2022, ambapo kiasi.

Share:

Friday, 13 January 2023

JUMUIYA YA WAZAZI MKOA WA DAR ES SALAAM YAPONGEZWA KUANDAA MAFUNZO YA UONGOZI KWA VIONGOZI WAKE


Na Mwandishi Wetu

NAIBU Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Balozi Rajab Luwhavi ameipongeza Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuandaa mafunzo maalumu ya viongozi wa jumuiya hiyo yaliyoanza kutolewa kwa Kamati ya utekelezaji.

Balozi Luwhavi ametoa pongezi hizo leo Januari 13,2023 jijini Dar es Salaam mbele ya washiriki wa mafunzo hayo yaliyoratibiwa na jumuiya hiyo chini ya Uongozi wa Mwenyekiti wake Khadija Ally baada ya kutembelea Kambi ya mafunzo hayo ya siku tatu yanayofanyika Kigamboni,Jijini Dar es Salaam.

Amesema kwamba amevutiwa na mafunzo hayo na yameonesha mwanzo mpya wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwamua kuwapatia mafunzo hayo viongozi wake.

“Nampongeza Mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam Khadija Ally kwa kuandaa mafunzo haya.Hakujipa muda wa kusherehekea nafasi aliyoipata baada ya kuchaguliwa ameamua kuandaa mafunzo hayo huku akitumia nafasi hiyo kukumbusha mambo ya msingi yanayohusu Chama hicho na jumuiya zake'',amesma Balozi Luwahi.

Amesema moja ya changamoto iliopo ni zana ya kuamini wanaopaswa kuelimishwa ni wale walioko chini kabisa,la hasha huyu Mwenyekiti mmepata mpya kabisa na maalum, ameanza kujifunza yeye na Kamati yake ya utendaji kwanza,na kwamba anampongeza Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, kwa sababu mtazamo wake sio mtazamo wa viongozi wa sasa .

''Mkoa wa Dar es Salaam ni namba moja kwa kila kitu, namba moja kwa ukubwa wake maana ndio unaongoza kwa idadi ya watu Tanzania, lakini ndio namba moja kwa nguvu zake kiuchumi,ndio mlango mkubwa wa kupokea na kutoa wageni kwenye nchi yetu, unapopata uongozi Mkoa wa Dar es Salaam ni tofauti na unapopata uongozi katika mkoa mwingine,Kwanini ni kwasababu ya mazingira ya mkoa wenyewe kwa hiyo nampongeza sana kwa mwanzo aliounesha wa kuandaa mafunzo haya kwa kamati yake ya utekelezaji ''amesema Balozi Luwhavi.

“Nampongeza yeye kwasababu hakujipa muda wa kusherehekea nafasi aliyoipata baada ya kuchaguliwa, amekiwahi hata chama chenyewe, tuendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu aendelee kumpa nguvu na maarifa , afya njema na umri mrefu zaidi ili atutumikie zaidi kwenye chama chetu, lakini niwapongeze ninyi nyote kwa kuchaguliwa.

Kuhusu jumuiya ya wazazi amesema kwa mujibu wa historia ndio jumuiya kubwa yenye lengo la kuwanganisha wazazi wote na kuwa mwanachama wa jumuiya ya wazazi sio lazima uwe mwanachama wa CCM.

“Katiba ya CCM haijawazuia kuwa mwanachama wa CCM kama haujaingia kwenye jumuiya wala haijasema kwa mtu anayependa kuwa mwanachama wa jumuiya ya wazazi peke yake akaridhika akawa mwanachama wa CCM isipokuwa tu ukitaka kugombea uongozi utakaokuingiza kwenye vikao vya Chama hicho basi sharti lake lazima uwe mwanachama wa CCM.

” Ndio maana huko nyuma tulitenganisha suala la itikadi na kuwaunganisha watu,kwasababu jukumu la kwanza la jumuiya ya wazazi ni kuwaunganisha wazazi wote chini ya uongozi mmoja, jukumu lake la pili ndio la kwenda kwenye uanachama.”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam Khadija Ally amewaomba waliopata nafasi ya kushiriki kwenye mafunzo ya uongozi kuwa wasikivu ili nao waweze kuacha alama bora na alama ya uongozi bora uliotukuka.“Tuwe viongozi ambao tutaishi na hata tutakapokufa tutaacha alama na kuwa mfano kwa wengine.

Aidha amesema kupitia mafunzo ya uongozi yanayotolewa kwa viongozi hao kuna mambo mengi wamejifunza na washiriki wameonesha kubeba yale yote yaliyoelezwa na wakufunzi huku akitumia nafasi hiyo kueleza wameingia kwenye mafunzo hayo kama wajumbe lakini watatoka kama viongozi .“Dhana ni ile ile ,Chama chetu ya Mapinduzi kimekuwa tanuru la kutoa viongozi.”
Share:

WANANCHI 710 WANUFAIKA NA KAMBI MAALUM YA UCHUNGUZI NA MATIBABU HOSPITALI YA MWANANYAMALA.

Daktari wa Binywa wa Magonjwa ya Ndani Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila akimfanyia uchunguzi Mwananchi aliyekuja kupata huduma ya uchunguzi na matibabu ya moyo katika kambi hiyo iliyodumu kwa muda wa siku nne. Baadhi ya wananchi wakisubiri kupata huduma Wataalamu wakiendelea kutoa huduma kwa wananchi waliofika kupatiwa kufanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu Daktari Bingwa wa Macho Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila Dkt. Yusta Mtogo akimfanyia uchunguzi mwananchi aliyekuja kupata huduma ya macho. Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala Dkt. Zavery Benela akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu walioshiriki katika zoezi la kutoa huduma na kufanya uchunguzi katika kambi hiyo.

*******************

Wananchi 710 wamenufaika na huduma za uchunguzi na matibabu kupitia kambi maalumu iliyoendeshwa na Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa kushirikiana na Madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala kwa muda siku nne.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikisha Dkt. Lulu Sakafu amesema kuwa lengo kambi ilikuwa ni kuwajengea uwezo wataalamu wa Hospitali ya Mwananyamala pamoja na kusogezea huduma za kibingwa na za kibobezi kwa wananchi waliopo mwananyamala na maeneo ya jirani.

“Lengo la Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila limefanikiwa kwa kiwango kikubwa, tunashukuru kambi ilienda vizuri ambapo wataalamu wetu wameshirikiana bega kwa bega na wataalamu wa mwananyamala katika kutoa huduma jambo ambalo limejenga ushirikiano endelevu” ameeleza Dkt. Sakafu

Aidha Dkt. Sakafu ametoa wito kwa wananchi kujiunga na bima ya afya kwa kuwa huduma za kibingwa ni ghali na si rahisi kwa wananchi wa kawaida kuzimudu kumudu kwa fedha taslimu.

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala Dkt. Aileen Barongo amesema kuwa muitikio wa wananchi umekuwa mkubwa



muitikio umekuwa mkubwa na wananchi wengi wamejitokeza kufanyiwa uchunguzi na kwa waliokutwa na matatizo wamepatiwa matibabu.

“Tumefanya uchunguzi kwa muda wa siku nne na mpaka sasa wananchi 710 wamefanyiwa uchunguzi, idara ambayo imepata wagonjwa wengi ni Idara ya Macho, ambapo wameona wagonjwa 270 wenye matatizo mbalimbali ya macho” ameelez Dkt. Barongo.

Kwa upande wake mmoja wa wananchi wa Mwananyamala Bi. Rahma Sharifu ambaye amefanyiwa uchunguzi na kupata elimu amewashukuru sana wataalamu wa Muhimbili-Mloganzila na Mwananyamala kwa kuwa kambi hiyo imenufaisha

Kambi hiyo imefanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwanayamala ilianza Januari 9 na kuhitimishwa Januari 13,2023. Huduma zilizotolewa ni uchunguzi wa magonjwa ya mfumo wa mkojo, mifupa, macho, kisukari pamoja na moyo.

Share:

RAPPA KANYE WEST AFUNGA NDOA NA MFANYAKAZI WAKE



Rappa Kanye West 'Ye' kwa sasa ni mume mpya mjini! Ameripotiwa kuwa amefunga ndoa hivi karibuni, kwa mujibu wa TMZ.


TMZ imeripoti kwamba Kanye West amefunga ndoa na mfanyakazi kwenye kampuni yake ya Yeezy, bibie Bianca Censori ambaye ni mbunifu wa usanifu kwenye Kampuni hiyo.


Chanzo cha karibu na Kanye West kimeuthibitishia taarifa hiyo TMZ, hii ni baada ya kupata picha ya kidole cha Kanye West kikiwa na Pete ya ndoa.


Aidha, Kanye West na bibie Bianca Censori mapema wiki hii waliripotiwa kuonekana pamoja sehemu mbalimbali wakipata chakula.
Share:

Picha : RAIS SAMIA AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 13 Januari, 2023.
Share:

POLISI SHINYANGA WAPANDA MITI KAMBINI, HOSPITALI MPYA YA RUFAA.... DC MBONEKO ASISITIZA "MARUFUKU KUKATA MITI OVYO, ILINDWE NA IKUE"



Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi (kushoto) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wakipanda miti.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

JESHI la Polisi mkoani Shinyanga, limepanda miti katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga iliyopo Mwawaza na Kambi ya Jeshi hilo, ili kuboresha mazingira pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Zoezi hilo la upandaji miti limefanyika leo Januari 13, 2023 na kupandwa miti 1000, ambapo katika kambi ya Jeshi la Polisi (FFU) imepandwa miti 200 na Hospitali ya Rufaa imepandwa miti 800 ya matunda na kivuli.

Akizungumza wakati wa kupanda miti, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amesema Jeshi hilo linaunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kampeni ya upandaji miti ili kuboresha mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

“Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga tumepanda Miti 1000, ambapo Miti 800 tumepanda hapa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa, na Miti 200 tumeipanda kambini, lengo ni kuunga mkono juhudi za viongozi wetu katika kampeni ya upandaji miti kuboresha mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi,”amesema Magomi.

Naye Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amepongeza Jeshi la Polisi kwa upandaji miti, huku akipiga marufuku ukataji wa miti hovyo bila ya kuwa na vibali, pamoja na wafugaji kupitisha mifugo yao kwenye miti na kuiharibu.

“Katika kampeni ya upandaji miti tunataka Shinyanga iwe ya kijani, na miti ambayo tunaipanda tunataka ilindwe na ikue, na tunatekeleza maagizo ya Makamu wa Rais ya kupanda Miti milioni 1.5 kila mwaka na Shinyanga tunakwenda vizuri,”amesema Mboneko.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga Dk. Luzila John, amesema hospitali hiyo ni mpya ambayo ipo Mwawaza na kushukuru upandaji huo wa miti ili kuboresha mazingira na kuahidi kuitunza miti hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza kwenye zoezi la upandaji miti.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akizungumza kwenye zoezi la upandaji miti.

Afisa Mazingira na Maliasili Manispaa ya Shinyanga Ezra Manjerenga akizungumza kwenye zoezi hilo la upandaji miti.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akipanda mti.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akipanda mti.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga Dk. Luzila John akipanda mti.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akipanda mti.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.
Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Askari Polisi wakiwa wameshika miche ya miti kwa ajili ya kuipanda.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JANUARI 13,2023













Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger