Maandamano ya wahitimu wa darasa la awali yakiendelea kuelekea ukumbini.
Mahafali ya kwanza katika shule ya Awali na Msingi SHADE ‘Shade English Medium Pre and Primary School’ yamefanyika ambapo jumla ya wanafunzi 17 wavulana wakiwa 8 na wasichana 9 wamehitimu shule ya awali ‘Nursery’ tayari kabisa kwa kujiandaa na masomo ya darasa la kwanza mwaka 2023 katika Shule hiyo.
Mahafali hayo yamefanyika leo jumatano Decemba 7,2022 katika shule ya Msingi Shade (Shade English Medium Pre and Primary School) iliyopo katika mtaa wa Magobeko kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.
Akisoma Risala, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Awali na Msingi SHADE, Lazaro Agustino Sibale amesema shule hiyo imeanzishwa mwaka 2021 ikiwa na jumla ya wanafunzi 21 wa kike 9 na wa kiume 12 na walimu 2 katika eneo la Ushirika Mjini Shinyanga na mpaka sasa shule ina wanafunzi wengi kutokana na wazazi na walezi kuiamini shule hiyo na kuleta wanafunzi ambapo kwa sasa shule ina darasa la awali hadi darasa la pili.
Hata hivyo amesema shule ya Msingi SHADE inakabiliwa na ukosefu wa umeme ,maji pamoja na barabara mbovu ya kutoka Bugweto hadi Magobeko hasa nyakati za masika kwa kuwa na utelezi na matope mengi hivyo kukwamisha maendeleo ya shule kutokana na changamoto hizo.
“Ubovu huu wa barabara unasababisha magari kukwama na kuharibika na mbaya zaidi hali hiyo inahatarisha maisha ya wanafunzi na walimu wao kwa kuwa wakati mwingine imekuwa ikijaa maji kwenye maeneo korofi kama mvua ikinyesha kubwa kiasi cha magari kushindwa kupita”, amesema Sibale.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shade English Medium Pre and Primary School, Bw. John Isack Migila amesema lengo la kuanzishwa kwa Shule hiyo ni kutaka kutoa elimu bora na yenye kukaribia viwango vya kimataifa ikiwemo kuhakikisha mtoto anapata maarifa stahiki awapo katika mchakato wa ujifunzaji .
Amesema pia shule hiyo inatoa elimu bure kwa watoto wamakundi maalumu kama vile watoto wenye ualubino ,yatima nak.huku watoto wengine ambao wazazi wao wana uwezo wakilipa ada rafiki kwa ajili ya kuwezesha nakuendeleza kituo hicho.
Aidha amesema, katika kuhakikisha Shule inatoaelimubora wanafunzi wanalelewa kiroho bila kubagua dini maana watoto wadini zote wanapokelewa katikashule hiyo bila kujali dini zao.
Kwa upande wake afsa elimu taalumu Manispaa ya Shinyanga Wingwira Kitila ambaye alikuwa Mgeni rasmi wakati wa mahafali hayo amesema changamoto zilizo wasilishwa katika risala ya shule ataziwakilisha kwa mkurugenzi mtendaji wa Manispaa hiyo Jomary Satura ili awezekuzipatia
Kitila ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wazazi na walezi kulinda watoto na kufatilia maendeleo ya watotowao pindi wawapo shuleni na akiwasii kujenga utamaduni wa kuripoti matukio ya vitendo vya ukatili wanavyo fanyiwa watoto kwenye maeneo yao ili serikali iweze kuchukua hatua.
Mgeni rasmi Wingwila Kitila akizungumza na wazazi na walezi.
Mgeni rasmi Wingwila Kitila akizungumza na wazazi na walezi.
Maandamano ya wahitimu wa darasa la awali yakiendelea kuelekea ukumbini.
Maandamano ya wahitimu wa darasa la awali yakiendelea kuelekea ukumbini.
Maandamano ya wahitimu wa darasa la awali yakiendelea kuelekea ukumbini.
Wahitimu wakicheza pamoja na mwalimu wao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shade English Medium Pre and Primary School,Bw. John Isack Migila akijiandaa kukata utepe akiwa na wahitimu.
Mwalimu mkuu wa Shade ,mkurugenzi ,meneja wa shule pamoja na wageni waalikwa wakiwa kwenye picha ya pamoja wakiendelea na sherehe.
Baadhi ya viongozi wakifuatilia mahafali.